Ndugu zangu wazanzibar,Ni muda mrefu sasa tumekua ktk manung'uniko kwamba serikali ya Muungano(Tanganyika) wanatunyonya.
Kumekua na rai nyingi sana za kutaka mamlaka kamili ya nchi Zanzibar ili tujiendeshe kama nchi nje ya Jamhuri ya Muungano.
Wapo wazanzibar walofika mbali zaidi na kusema sasa Muungano basi.
1.Napenda niwaulize ndugu zangu wazanzibar kabla hatujapaza yowe la kuukataa muungano huu je tumejiandaaje kujiendesha kama nchi kamili nje ya Muungano.
2.Niwajuze wazanzibar wenzangu kelele na manung'uniko yetu yamewaamsha watanganyika sasa wako mbioni kupata nchi yao nje ya muungano.wao wamejipanga tayari kwa hilo.
3.Ndugu zangu wazanzibar kama tulikua tunafanya utani wenzetu wapo serious,kiuchumi,kisiasa.
Wamejiimarisha ktk nyanja nyingi muhimu kama nchi.JE sisi tumejiandaaje!
Rai yangu kwenu mdundo huu wa kuvunja muungano usituleweshe naona mwisho wake tutakuja kuwapigia magoti watanganyika turudiane kuungana.
Upepo wa mabadiko
Upepo wa kisiasa
Lazima tuangalie tuna vyuo vikuu,vyanzo vya mapato zanzibar,ajira,n.k
Malalamiko na manung'uniko yasio na tija hayafai.
Enhe hebu nipe story kidogo, KISONGE pale mnakuwa mnalipwa ngapi? Mana naskia wenzenu lumumba wanalipwa buku 7 nyie ngapi? Maana maskani yenu pale kwa mipasho, kama Khadija Kopa.
1- Zanzibar haina haja ya kujiandaa kuiendesha nchi yake, tangu muungano unaanza visiwa ivi vinaserikali, sasa sijui kujiandaa vipi na sijui nani anatakiwa kujianadaa kati ya mwenye serikali na alokuwa hana ata wizara!
2- eti kelele zetu zimewaamsha watanganyika, labda zimewaamsha wana jf, sijasikiapo maandamano Bara wakidai nchi yao, naona maneno JF tu vitendo Zero. Kisha kauli ya watanganyika wapo mbioni kupata nchi yao, sio sahih, ulitakiwa useme wazanzibari wapo mbioni kutaka nchi yao, wao ndio walioamka, na wakawaamsha hao wenzako, wazanzibar ndio wanaodai nchi huru mpaka ndani wakawekwa, kwaiyo unatakiwa useme znz ipo njiani kupata uhuru wake!
3- wamejiimarisha vipi kiuchumi, kisiasa ata useme wapo serious? Siasa zenyewe sasa ivi zishachafuka, 2015 apo pana kumwagika damu, sisi tumeacha upuuzi wa kumwagana damu tulipoleta serikali ya mseto, tumepiga hatua, sasa wenzetu wanarudi nyuma, wakipigana mabomu mikutanoni, wakitukanana, sasa sijui nani wapo serious. Ukisema uchumi itabidi nikushangae, haya userious wao uko wapi? Tanzania ni ya kuwa maskini kweli? Almasi, dhahabu, tanzanite, gesi, maliasili tele kisha uchumi bado mbovu, na bado wanayataka mafuta ya zanzibar, heh, hii nchi kama ina laana vile, sasa sijui wameimarisha vipi, na obstacle kwa zanzibar kuendelea ni huu muungano hasa, kwamba kila kitu kimefanywa cha muungano. Habari ndo hiyo, haya kachukua chaki ukaandike ubaoni kwenu mipasho yenu.