Wazalishaji wa viroba walalamika kupewa muda mfupi na waziri mkuu, January Makamba awajibu

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,058
January Makamba amesema operesheni ya kutokomeza viroba itaanza Machi 2 kufuatilia agizo la utekelezaji wa agizo la serikali mikoa yote likiratibiwa na kamati za ulinzi na usalama na kamati za mazingira.



Wanaodai katazolimekuja ghafla kuwawaziri mkuu ametoa muda mfupi January Makamba amesema katazo hilo lilishatolewa May 2016 siku ya mazingira duniani na gazetila mwananchikuandika 'Serikali yashusha rungu pombe za viroba' na kuwa pombe hizo zilikuwa zimekatazwa ifikapo January 1 2017.

kwa hiyo kama kuna mtu aliendelea kuchukua mkopo, malighafi na uzalishaji wa muda mrefu basi atakua ameidharau serikali.

Amesema pia watakaoingiza viroba nje ya nchi watatozwa faini isiyopungua milioni 5 au kifungo kisichopungua miaka 2 au vyote, kuzalisha ni faini isiyopungua shilingi milioni 2, kifungo cha miaka 2 au zaidi, kuuza kuhifadhi au kusambaza faini isiyopungua laki moja, kifungo kisichopungua miezi 3 au vyote, ukikutwa ukinywa faini 50,000 kifungo miaka 3 au vyote.

Mpaka sasa hawajapokea taarifa ya kupelekwamahakamani
 
20170301_073917.jpg
[
Naona Konyagi wamejiongeza badala ya kukalia kulalamika. Shida huleta maarifa.

Mega Trade wameuza sana Kiroba Original na ndo kimewatoa fulu. Japo KVant pia kwa sasa inafanya vizuri sokoni walilemaa sana kuipromoti wakidhani viroba vingedumu.
 
Yani kiutani utani viroba vinakuja kupotea? Vip waliokuwa na ajira kwenye viwanda vya viroba? Vip wale biashara yao ilikuwa ni viroba?

Naona kma vle gongo kuanza kurudi kwa kasi. Sababu viroba vilikuwa ni mbadala wa gongo.
 
Wauza viroba zamu yetu kuisoma
yote kwa yote nitaipongeza serikali iwapo itafanikiwa kutokomeza janga la viroba
 
Nimesikitika sana.

Yaani viroba wanavipiga marufuku kabisa kabisa?

Wengine ndo starehe zetu hizo sasa sijui wanataka tuanze kunywa yale mapombe machafu ya vilabuni...

Wahshi kabisa.
 
Baada ya ngada,miraa,jani na viroba kuwa jinai sasa ugoro,gundi,sigara nyota zitapata sana wateja bila kusahau machozi ya simba yale ya asili
 
Pembeni ya January namuona Profesa Kamuzora, safi sana baba! ulinijengea uwezo niko fiti hapa nilipo
 
Back
Top Bottom