ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,758
- 9,592
Hi wanajamvi wenzangu
Kama ilivyo kawaida yetu kujumuika na kuleteana habari, mambo yahusuyo maisha na vichekesho vya hapa na pale na vilevile kutiana moyo, kurekebishana panapobidi, kujuliana hali na kupongezana kwa kila jambo tulifanyalo.
Leo tena nimeingia mzimamzima kuwaweka sawa ama kuwatia moyo, na kuwafariji ndugu, marafiki, wapendwa wenzangu kwa mambo makuu 2 ambayo ni muhimu katika nyanja, ngazi za maisha kwa mwanadamu.
mambo yenyewe ni
a) Kusubiri au kungojea kwa wakati wake
b) kutokukata tamaa kwa hali yoyote ile uipitiayo
Ndugu zangu na marafiki zangu ni vyema tukatambua kuwa tuliumbwa kwa makusudi na mpango wa Mungu na
ndiye aliyetuweka hapa duniani ili tuishi na kuiongeza nchi. Na ni vyema tukatambua kuwa vitu vyote vya hapa
duniani ndiye aliyeviumba ili sisi wanadamu tuvitawale vyote vya majini na nchi kavu. Kwanini nimeonelea niseme
haya hapa kwa sasa?. Kitu kilichonisukuma na kuandika hapa hii mada ni hayo mambo mawili niliyoorodhesha hapo
juu. Kwa kipindi hichi watu wengi wameshindwa kusubiri hususani vijana wengi wameshindwa kuwa na moyo wa subira
wao wanataka mambo ya haraka haraka (shortcut) ili mradi watimize haja za mioyo yao na matamanio ya nafsi zao. Wengi wao hawana tunda la uvumilivu na kusubiri hawataki kuwa watu wastahimilivu katika yale wanayojiwekea au
jipangia.
Mwonekano wa wengi wanataka vitu virahisi rahisi na sio kutafuta kwa nguvu na akili zao kuvipata hivyo wavitarajiao
wengi wao wanasema kwanini nisubiri nitasubiri mpaka lini na wakati maisha yenyewe ni mafupi, bora niingie kona hii nipate kwa haraka kuliko kusubiri. kwani nitasubiri milele na wala nisipate hicho ninachokitaka. Hayo ni mawazo mgando ya vijana wengi, wengi wao hawana haja kuishi wanaona bora leo niende temeke nikaibe sofa, kesho mbezi na sehemu kwingineko. Wengine wamejisajiri katika mashirika ya (freemason) iili tu watajirike kwa haraka na kupata yale waliojiwekea. Hawaoni kuwa huko ni kuhatarisha maisha yao. wana njia za panya za kutafuta riziki zao. Je wewe rafiki yangu unayesoma hapa ni mtu wa kusubiri nakungojea yale uliiyoyapanga kwa muda mrefu, Je umeona kuwa hayatimii hata moja ya yale uliyojiwekea.
Acha nikutie moyo kuwa mtu mvumilivu kwani mvumilivu hula mbivu na mngoja achoki ipo siku utapata yale uliyotarajia kuwa mtu mwenye subira kwani subira yavuta kheri. Kataa ahali ya kukata tamaa kwa kuona kuwa umesubiri kwa muda mrefu na wala hujaona kitu. Jijengee hali ya kusubiri kwani wakati wake utavuna na utapata usipozimia roho yako. Thubutu kuwa mtu mwenye kusubiri kwani unaweza hebu soma Warumi 4:13-14,
elewa kuwa wewe mtu wa kufanikiwa na unaweza kusubiri, kuwa na nia ya kuvumilia mpaka mwisho wa dahali.
TAMBUA KUWA PENYE NIA PANA NJIA NA IPO SIKU UTATOKA TU ACHA SHORTCUT SIO NZURI KABISA RAFIKI
Ciao
Copy: watu8, Mtambuzi, Bakulutu, (my cousin) charminglady, (kaka wa ukweli) Erickb52, Passion Lady, (mtani wa jadi) Filipo, Arushaone, Ruttashobolwa, ruttashubanyuma, Nivea, Asprin, Nicas Mtei, Excellent, Mentor, Madame B, Mamndenyi, Chimbuvu, Baba V, @mr rock, Donn, (msumbufu mkubwa) Agush, (mpiganaji mwenzangu) Smile, cacico, (aliyeadimika) nitonye, gfsonwin, snowhite, Zion Daughter, and all jf cc friendly

Last edited by a moderator: