Mungu hatakutendea jambo: Ila anatenda jambo kupitia wewe

Mungu hatakutendea jambo: Ila anatenda jambo kupitia wewe

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
5,183
Reaction score
5,715
Kuna mtazamo fulani hatari sana wa kusubiri kuwa kuna wakati Mungu atakutendea jambo fulani na mtu unaamua kukaa kusubiri. Hakika hii ni hali ya hatari sana katika maisha yetu tulio wengi.

Tunaisahau Sheria muhimu sana ya kuwajibika " law of accountability". Ni sawa kuwa unaweza ukagundua kusudi lako, ukaona maono n.k lakini suala la kutimiza au kufikia uliyoyaona linahutaji kujikana/ nidhamu "discipline". Suala la kujikana Ili kufikia lengo fulani ni wajibu wa mtu binafsi na siyo nguvu nyingine kutoka nje.

Unajiweka katika mkao gani kupata unachokitaka? Swali hili siyo suala la kuombewa maombi na dua ila ni machaguo ya mtu binafsi na nidhamu yake.
 
Back
Top Bottom