Waweza dhani upo peke yako kumbe mpo wengi

Waweza dhani upo peke yako kumbe mpo wengi

Ngwananzengo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2012
Posts
1,911
Reaction score
1,322
Kuna kijana yeye ni jirani yangu na ni injinia.

Kapanga mwaka kesho atavuta jiko.

Kwa unyenyekevu mkubwa alimfuata mjomba wake kwa ushauri.

Pamoja na Mengi aliyoshauriwa aliambiwa kama huyo binti familia yake wameokoka basi amchunguze kwa umakini kwani sehemu hii imekuwa kichaka cha kuficha waovu.

Baada ya kupewa ushauri huo alikuja kunipa taarifa kwa kuniambia, "inashangaza mawazo yako yamekuwa na mlengo sawa na mjomba wangu".

Binafsi nimekuwa nikijipambanua kutokuwa upande wa wale wote wanaojifanya kuzishika "IMANI" za dini barabara.

Tafsiri yangu huu ni sawa na ulevi mwingine kwa maana hiyo ni vizuri tahadhari ikachukuliwa.

Nimefarijika kuona kumbe Kuna wengine wenye fikra kama zangu.
 
Sasa ni yupi afaae kati ya huyo mwenye element za ushika dini na yule asiyekuwa nazo kabisa?
Nadhani sifa namba moja ya mke ama mme ni yule mwenye hofu ya Mungu hapo haijalishi ni dini gani.
Wacheni kuchunguza sana kila mtu utamwona hafai maana kama alitoka kwenye familia ya kilokole atachunguzwa kwa maovu je akipata alietoka familia ya kiganga kabisa atapewa ushauri gan?
 
Utakua mpumbavu na lofa iwapo ukiingia kwenye ndoa kwa kuangalia imani ya mtu bila kumchunguza yeye kama binadamu....pia kutafuta mchumba kwenye nyumba za ibada ni hatari ...
 
Sasa ni yupi afaae kati ya huyo mwenye element za ushika dini na yule asiyekuwa nazo kabisa?
Nadhani sifa namba moja ya mke ama mme ni yule mwenye hofu ya Mungu hapo haijalishi ni dini gani.
Wacheni kuchunguza sana kila mtu utamwona hafai maana kama alitoka kwenye familia ya kilokole atachunguzwa kwa maovu je akipata alietoka familia ya kiganga kabisa atapewa ushauri gan?

Pengine hujaelewa bayana, binafsi mtu mwenye "mahaba" na mambo ya kiimani au kwa tafsiri nyingine mtu mwenye kuishika dini kwa hisia kali hua namchukulia kwa tahadhari kubwa. Jambo hili husababisha wengi kutokufikiri kwa "mantiki". Mtu ambae ameishika dini kawaida pasina "mahaba" huyu kwangu ni sawa kwani kuna akili kaiacha "reserve" ili imsaidie kufikiri kwa mantiki.
 
Teh teh..Mi bora niwe na mwanamke mwenye mambo mengi awe ananirusharusha roho hata akija kuzingua moyo unakuwa ushazoea kushtuka... kuliko kuja kufanyiwa sapraiz

Aiseee sapraiz n mby sana mm nmesababjshiwa napata presha mapenz haya mabaya sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom