Wawekezaji wenye mafanikio makubwa kwenye majengo ya kupangisha wanakuwa hivi

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Mafanikio yanaanzia kwenye akili yako. Leo ninakushirikisha mambo mawili ambayo yanaweza kukuumiza. Endapo yatakuumiza pole na utanisamehe kwa hilo. Kusudi kuu la makala hii ni kuonyesha njia ya kweli ya kujenga utajiri kupitia ardhi na majengo.

Tofauti 2 Za Wawekezaji Wenye Mafanikio Makubwa Na Wale Wasio Na Mafanikio Makubwa.

Moja
Aina Ya Upendo/Matamanio
Wawekezaji wasio na mafanikio makubwa. Sifa zao ni kama vile;

✓ Hupenda umiliki wa nyumba ya kuishi kuliko ya nyumba ya uwekezaji.

✓ Hununua au kujenga aina yoyote ya nyumba bila kujali changamoto anaweza kukutana nazo mbeleni.

✓ Hufurahia sana umiliki wa nyumba ya kuishi hata kama atakuwa amepanga mkoa wa mbali na nyumba yake ilipo. Utasikia anavyotamba mbele ya wafanyakazi wenzake mpaka wamkome.

✓ Hawajawahi kufikiria kupangisha nyumba hiyo wanayoipambania.

✓ Hutumia kiasi kikubwa sana cha fedha kwenye ujenzi kuliko hata kinachotakiwa. Mfano; atahitaji paa ya nyumba yake iwe imeinuka sana sana kuliko nyumba yoyote iliyowahi kujengwa kwenye mitaa ya karibu. Atabuni geti la gharama kubwa sana hata kama halina sio imara ili tu awashinde kwa sifa majirani zake. Wawekezaji Wenye Mafanikio Makubwa Huwa Na Sifa Hizi.

✓ Kipaumbele cha kwao cha kwanza ni kutengeneza kipato endelevu au kutengeneza faida baada ya kuuza.

✓ Kipaumbele cha pili kwao ni wapangaji bora au wanunuzi bora. Hapa hufanya utafiti kwanza wa uwepo wa wapangaji bora kabla ya kujenga nyumba.

✓ Kipaumbele cha tatu kwao ni nyumba yenye kukidhi mahitaji ya wapangaji. Wawekezaji wenye mafanikio makubwa sana wanajali sana mahitaji ya wapangaji. Kwao wapangaji ni kipaumbele cha pili baada ya kipato endelevu.

Kwa mfuatano wa vipaumbele hivi, wawekezaji wenye mafanikio makubwa hujiwekea vigezo vyao vya kiuwekezaji. Vigezo ambavyo vinakuwa ni barabara ya kumiliki na kusimamia nyumba ya kupangisha inayolipa sana.

Mbili

Vigezo vya uwekezaji.

Wawekezaji wa kawaida hawana vigezo vyovyote vya kiuwekezaji. Kwao nyumba yoyote ambayo inafaa kwa ajili ya makazi au biashara ni kununua au ni kujenga. Kwao sifa ya umiliki wa nyumba ndiyo kipaumbele chao cha kwanza.

Wawekezaji wenye mafanikio makubwa sana hufokasi kwenye vigezo bora vya uwekezaji kwenye ardhi na majengo. Hufokasi vigezo ambavyo vimekaguliwa na mshauri mbobezi kwenye ardhi na majengo kama nifanyavyo mimi Aliko Musa.

Bila kuwa na vigezo bora vya kiuwekezaji, utajenga nyumba ya kupangisha na hutapata wapangaji bora kwa wakati.

Bila vigezo bora vya kiuwekezaji, utanunua hosteli ya wanafunzi na hutaingiza kipato kikubwa na endelevu kwa kila mwaka.

Bila vigezo bora vya kiuwekezaji, huwezi kumiliki nyumba nyingi za kupangisha kwa sababu nyumba ya kwanza tu itashikilia kiasi kikubwa sana cha mtaji fedha uliowekeza.

Bila kuwa na vigezo bora vya kiuwekezaji, utatumia kiasi kikubwa sana cha nguvu na fedha kwenye usimamizi wa nyumba yako ya kupangisha.

Bila kuwa na vigezo bora vya kiuwekezaji, utatumia fedha nyingi sana za kutangaza nyumba yako unayotaka kuuza isipokuwa kama utakubali kuuza kwa bei ya hasara sana.

Wengi waliamini kuwa baada ya kumiliki nyumba ya kwanza maisha yao yangebadilika kabisa. Lakini imekuwa kinyume chake.

Nyumba Ya Biashara.

Rafiki yangu mpendwa, historia ya zaidi ya miaka 100 iliyopita imeonyesha kuwa nyumba za biashara zina hatari nyingi za kiuwekezaji ukilinganisha na nyumba za vyumba vichache za makazi.

Kuwa makini sana unapowekeza kwenye majengo makubwa (zaidi ya vyumba 20) ya biashara. Hii ni kwa majengo hayo yakikosa wapangaji hukosa kabisa thamani.

Nyumba yoyote ya biashara inakuwa na thamani kubwa sana mbele ya benki, wakala wa bima, serikali, endapo tu itakuwa na mkataba wa muda mrefu wa upangishaji.

Ni kosa kumiliki nyumba kubwa ya biashara bila kuwa na mikakati mizuri ya mikataba ya upangishaji, kuwafikia wapangaji bora na kadhalika.

Huu ni uwekezaji ambao unahitaji mipango mikakati inayofanya kazi. Usikubali makosa yako yakurudishe nyumba nyuma kwenye safari yako ya uwekezaji.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.

Njoo uungane na FAMILIA YA TZ REAL ESTATE TEAM. Ukiwa hapa huwezi kukosa maarifa sahihi ya kujikwamua kwenye hali uliyonayo.

Nitumie ujumbe usemao NYUMBA ZA KUPANGISHA...
 
Nimekuelewa mkuu. Ulichoandika ni kweli. Mimi nilipambana Sana kujenga nyumba ya kuishi. Mambo mengi yalisimama, hela yote ilikua inaenda kwenye ujenzi. Kwasasa nina nyumba moja tu. Hii ni hasara.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom