Wawekezaji waanza kujiondoa Tanzania

Mgodi wa tulawaka na resolute muda wao ulishakwisha kipindi cha kuvuna dhahabu sasa hivi wanakuambia wanamalizia malizia tu masalia.

Mfano mgodi wa tulawaka ulikuwa unategemea udumu kwa miaka mitano tu na usifikiri hao jamaa wanaondoka kwa sababu za kisiasa wameshaona kuwa siku za karibuni hawatakuwa wanapata tena dhahabu nyingi kama walivyokuwa wanazipata kupitia migodi hiyo na ndio wanaamua kuuza hisa kwenye hiyo migodi.

Migodi mingine kama GGM au KMCL ya kakola na NorthMara, bado wanavuna dhahabu za kutosha huko na kamwe hawawezi kuuza au kuondoka, chunguza vizuri kwenye hiyo migodi wanayoondoka production imeshuka sana sasa hivi na target yao ilishatimia siku nyingi.

Kitu ambacho kinawaondoa hawa jamaa, kama ni kweli nadhani ni suala la kodi. Hawataki kabisa kulipa kodi. Huu ni wizi kwa nchi yetu.
 
Ijumaa, Septemba 14, 2012 09:06 Mwandishi wetu


KUFUNGWA kwa migodi ya dhahabu ya Tulawaka Biharamulo, Resolute ya Nzega, na Barrick kuwa katika mipango ya kuuza zaidi ya hisa zake asilimia 70 kwa makampuni ya madini ya China yaitwayo China National Gold Group, ni ishara kwamba Tanzania itapoteza nafasi yake kama nchi ambayo kwa kipindi cha miaka zaidi ya ishirni, imeweza kuvutia mitaji mikubwa ya kuwekeza katika uchumi wa nchi.


Katika kipindi cha miaka 25 iliyopita Tanzania imeweza kupokea au kuingiza kwenye uchumi wa nchi vitega uchumi vyenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 433, kiasi kikubwa kimewekezwa kwenye sekta ya madini, sekta ya viwanda, usafirishaji, fedha na mawasiliano. Tanzania imekuwa na sera ya kufungua milango kwa ajili ya kuvutia wawekezaji kutoka nje. Nchi za Uingereza, Afrika ya Kusini, Canada, Kenya na India zinaongoza kwa kuwekeza vitega uchumi nchini. Ni ukweli usiopingika kwamba Tanzania imenufaika sana na uwekezaji kutokana na kupatikana ajira zipatazo zaidi ya 150,000 za wazi na za kuhudumia miradi.


Hata hivyo uwekezaji nchini Tanzania na katika nchi changa ulipungua sana kutokana na mtikisiko wa uchumi duniani ambao ulitokea kati ya mwaka 2008 na bado unaendelea. Miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na miradi ya uwekezaji ilisimama hapa Tanzania kama vile mradi wa madini ya Nickel wa Kabanga Ngara na mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi huko Mtwara ambao ulikuwa utekelezwe na Kampuni ya Artumas ya Canada. Hata hivyo Tanzania ilipita katika kipindi hiki kigumu kutokana na ukweli kwamba uchumi wetu unategemea uchumi wa dunia kwa kiasi na si kikubwa sana.


Sababu nyingine ambazo zimeanza kufanya wawekezaji wapunguze kasi yao kuwekeza Tanzania zinatokana na mpangilio wetu wa ndani hasa kuhusiana na malumbano ya kisiasa na jinsi sera na sheria za uwekezaji zinavyotazamwa na jamii nzima hasa vyama vya siasa na wanasiasa kwa upande mmoja na pia wanaharakati na mashirika ya kutetea haki za binadamu, pamoja na jinsi vyombo vya habari vinavyoandika masuala yanayohusu miradi ya uwekezaji.


Kwa muda wa miaka saba sasa vyombo vya habari, wanasiasa na hata Wabunge, kwa kiasi kikubwa wamechangia kuwaona wawekezaji kutoka nje kama wezi wa mali ya umma na rasilimali za nchi. Mtazamo huo umetokana na jinsi mikataba ya uwekezaji inavyokuwa ya siri, inavyokuwa na vipengele vinavyowapendelea wawekezaji na pia kiasi halisi ambacho nchi inapata kwa kipindi cha muda mfupi ambapo shughuli za uzalishaji au utoaji huduma zinapoanza.


Kwa namna moja au nyingine dhana ya mrahaba haikueleweka. Watu wengi walifikiri malipo ya mrahaba ndiyo malipo nchi inayoyapata kutokana na madini yanayochimbwa. Lakini dhana ya mrahaba ni tofauti na ufahamu wa watu wengi.


Maana ya mrahaba ni kiasi cha thamani ya madini (kati ya asilimia 2 mpaka 10) ambacho nchi inapata kwa ajili ya vizazi vijavyo ambavyo vitakuta madini yamemalizika. Hivyo kiasi hicho siyo malipo kwa madini ya nchi ambapo yanachimbwa bali ni kwa shughuli nyingine.


Kwa upande mwingine madini yana mikataba yake ambayo inatamka wazi masuala ya kodi na malipo mengine. Suala la mikataba ni suala la kitaalamu na uzoefu katika fani hiyo. Kutokana kwamba nchi nyingi hasa nchi changa hazina uzoefu na wataalamu wa kutengeneza mikataba yenye manufaa kwa nchi zao basi mikataba mingi imekuwa ya kinyonyaji na hivyo haileti faida kwa nchi husika.


Mikataba mingi ina vipengele ambavyo vinazifunga nchi zenye madini kutoweza kutumia enzi na haki za kisheria kufanya mabadiliko ambayo yataleta faida kwa pande mbili zinazokabiliana. Hivyo mikataba mingi ya uwekezaji katika madini ni kweli haina faida hasa kwa kuzingatia mapungufu katika miundombinu na pia mapungufu katika utoaji huduma za kitaalamu, kiteknolojia na kifedha.


Manung’uniko ya watu wengi kwa kiasi kikubwa yamewalenga wawekezaji wageni badala ya kutambua kwamba ni Watanzania wenzetu ndiyo wamesababisha misiba na rasilimali ya nchi kuondoshwa bila chochote tunachokipata. Hata hivyo tabia ya Watanzania kutojifunza haraka na kuchangamkia tenda hasa katika maeneo yale ambayo akili, nguvu na uwezo vinahitajika kwa madhumuni ya kudhibiti mazingira imewafanya Watanzania wengi wapende kufanya kazi za uchuuzi badala ya kufanya kazi za kutumia nguvu, akili na mahesabu kwa malengo ya muda mrefu lakini yenye faida kubwa.


Tukichukulia mfano wa nini mahitaji ya huduma katika migodi yetu, ni wazi chakula, huduma za usafiri, huduma za fedha, na huduma nyinginezo ni mambo muhimu ambayo yanagharimiwa kwa kiasi kikubwa cha fedha na makampuni ya migodi. Lakini Watanzania wanalalamika kwamba makampuni ya migodi yanaleta chakula na kutegemea huduma nyingine kutoka nje badala ya kuzipata huduma hizo kutoka ndani ya nchi.


Tukijiuliza kuna makampuni mangapi ya kutoa huduma kwa mahitaji ya makampuni makubwa ya migodi, ni makampuni machache ya watanzania yanayoweza kutoa huduma hiyo na pia kutokana kwamba watu wengi wamezoea kufanyia shughuli zao katika sehemu za mijini, ni makampuni machache yanaweza kuwa tayari kwenda kufanyia kazi huko maporini kwenye migodi.


Tukirejea katika Bunge na kwenye vyombo vya habari, mambo mengi yaliyokuwa yanasemwa na kuandikwa hayakuainisha matatizo ya mfumo na sheria dhidi ya matatizo ya hujuma ambazo zinafanywa na makampuni. Kwa namna moja au nyingine madai ya wizi, ufisadi na serikali kuonekana inashambuliwa kwamba imeshindwa kazi ni mambo ambayo wawekezaji wanayafuatilia sana na yanatabiri bila kuwa na uhakika kwamba Tanzania inawezekana ikakumbwa na machafuko. Kwa upande mwingine Wabunge wamekuwa wakitoa shutuma kali ambazo zinawafanya wawekezaji kutangazwa kama wezi ambao kazi wanayojua kuifanya vizuri ni kuziibia nchi changa kama Tanzania.


Kwa wataalamu wa masuala ya uwekezaji Tanzania ni nchi ambayo imejengewa na taswira kwamba huko mbeleni inaweza ikawa na machafuko. Waliojenga taswira hiyo ni Watanzania wenyewe ambao baadhi yao ni wasomi, wanasiasa na watu wengine walioko katika biashara na menejimenti ya viwanda.


Shirika la Barrick ambalo linaongoza katika uchimbaji madini ya dhahabu kwa kuamua kufunga virago na kuuza migodi yake wakati dhahabu ni madini ambayo thamani yake imepanda sana katika soko la dunia ni wazi kwamba kuna matatizo ya kimkakati ambayo Shirika la Barrick na wawekezaji wengine wamebaini.


Tanzania haina sababu ya kujivunia kuwa na wanasiasa wenye uwezo wa kulumbana. Tanzania tunapaswa kujivunia kuwa na watu wenye uwezo wa kuchambua hali na kutafuta majibu ya matatizo yetu ya ndani na matatizo ya nje. Suala hili la wawekezaji kupunguza kasi yao ya kuwekeza ni suala ambalo lazima tulifanyie kazi na kujua kwa nini yamezuka matatizo.

Nini unachotaka kujenga hapa!! Kuna mwizi ambaye hajui anachofanya ni uhalifu!? Hata kuwatumia vipofu ili kuiba ni wizi tu! Umejaribu kuelezea "mrahaba" umeshindwa hebu linganisha na mikataba ya nchi nyingine uweze kutoa ujumbe unaotaka kutoa. Hebu angalia mkataba wa mafuta ambao Kenya imeanza kuchimba TURKANA. Mjinga akierevuka mwovu huwa mashakani. Uoga uliowaingia hao jamaa ni dalili zote za kuondolewa madarakani kwa makuwadi wao! wanawahi.
Afadhali yabaki ardhini kuliko kuachiwa machimbo tupu na mazingira yaliyoharibiwa na UMASKINI uliopindukia!!. Wote tutafakari unataja faida za madini!! bila aibu!! Miye ukweli sipendi kuibiwa hata kama mali yangu sijui kuitumia ni mali yangu!! LET THEM GOOOOO!!! wajukuu na waje wayakute madini yetu!!
 
Tanzania futeni mikataba yote, hawa lazima mukianza kuwalipisha kodi tu wataondoka.

My take:Hawa jamaa wkija TZ muombe ushauri wao tu au hata kuununua sio kuwakabidhi ardhi.
 
Mwandishi wa hii makala ameacha hoja za msingi sana kuhusu uwekezaji kwenye sector ya madini. Mgodi wa Tulawaka unakaribia mwisho - financial viability. Kwa sasa Barrick kuendelea na huo mgodi hakuna tija kwa sababu dhahabu imepungua/karibia kuisha. Huu mgodi ulikuwa wa wazi (open pit) na miaka ya karibuni wakaenda underground kwa kiasi, hata hivyo financially, it does not make sense kuendelea nao.

Sasa, dilema inakuja, what to do na mashimo? Tukumbuke haya ni mashimo makubwa sana na ukisema yafukiwe itachukuwa miaka na gharama zake ni kubwa mno. So, practically speaking mashimo yatabakiwa wazi. Hata hivyo kuyaacha wazi kunaleta shida nyingine, wananchi watavamia hilo eneo na kuendelea kuchimba walau waambulie mabaki, huku watu wa mazingira nao wanalia, wakati huo huo dunia/activist wataanza kusema Barrick imeacha mashimo makubwa, na reputation ya Barrick itazidi kudorora. So what do you do? Unamuuzia Mchina amalizie viji-mawe vilivyobakia. Afukie mashimo au la, hayo ni Mchina na kama tujuavyo Mchina haguswi na kelele za mazingira, haki za binadamu or anything.

Ni ukweli usiopingika. Mzungu hataki kufidia baada ya kupata faida anaona kama ni kupunguza faida yake.
 
Haya majizi yanayoiba na kwenda kuficha uswisi na south africa,siyangekuwa yanainvest kwenye miradi km hiyo ili kutunusuru na haya majitu meupe!sasa wanapeleka huko wanafaidi watu wasiohusika kabisa.
Kwakweli kama wangekuwa wanaiba na kuinvest hapa na miradi inaondoa umasikini kwa walio wengi ingekuwa ni heri,tungekuwa tunaajiri experts tu tena kwa muda maalum.
 
My Friend. Maendeleo siyo kodi rafiki yangu. Serikali kupata kodi na mwananchi mmoja mmoja kuneemeka havina uhusiano mkubwa kiasi unachofikiri. Siyo kweli kuwa kodi inatumika vizuri kila wakati - siyo TZ tu, ni duniani kote.

Hii migodi hufungua fursa za ma-supplier kama Tanesco, makampuni ya ndege, wauzaji wa bidhaa mbalimbali, ajira kwa wafanyakazi wa rika zote na visomo vyote (kuanzia elimu ya msingi mpaka PhD), vyuo, mahoteli nk, nk. Hapa ndipo thamani ilipo kwa mwananchi wa kawaida, siyo kwenye kodi.

Hata serikali ichukue 100% ya mapato ya migodi kama kodi, hakuna siku atakuja ofisa wa serikali nyumbani kwako, na shangingi lake STK kavaa suti ya bei chafu, halafu akuambie - "Chukua hii cheki ya Shin Million Mbili, ni stahili yako kama mwananchi wa TZ kutokana na mapato tuliyoyapata kwenye kodi ya mgodi fulani".
Lakini ukijituma, ukafanya kazi kwenye huo mgodi, au ukawa supplier wao, si ajabu ukapata maradufu ya hiyo pesa - na ukiipata, utatengeza fursa kwa watu wengine ambao wewe utanunua huduma kwao (mafundi gari, wajenzi, mahausgelo, shule za wanao etc)

Unapowapiga vita wawekezaji wakubwa namna hii, ni sawa na ile hadithi ya Killing the Goose that Lays Golden Eggs.
naogopa kusema hujui faida ya kodi,kama serikali inakusanya kodi to the max na hakuna ufisadi kodi inaweza kubadilisha maisha ya watu,individually and as a nation(country,state,whatever you call it),what's the use kama unapata mamilioni kutoka ajira ya hao wawekezaji halafu unaendesha gari lako kwenye barabara ya mashimo au hakuna running water kwenye mansion lako,.kapitie tena public finance kwenye madesa yako kwenye shelves
 
2015 ukombozi ukishapatikana viongozi wa ccm na wengine wote wlioshiriki kuwaleta hawa wezi watapewa adhabu ya kufukia haya mashimo kwa mikono!

Haswaa mkuu,maana hii ni hatari,waende tu bwana tunachopata hakuna
 
naogopa kusema hujui faida ya kodi,kama serikali inakusanya kodi to the max na hakuna ufisadi kodi inaweza kubadilisha maisha ya watu,individually and as a nation(country,state,whatever you call it),what's the use kama unapata mamilioni kutoka ajira ya hao wawekezaji halafu unaendesha gari lako kwenye barabara ya mashimo au hakuna running water kwenye mansion lako,.kapitie tena public finance kwenye madesa yako kwenye shelves

Unajua uwezo wa kuelewa dhana ya kwamba kodi siyo alfa na omega, ni uwezo ambao either unao hau hauna. Hakuna eneo la katikati. Either unakuwa unaamini kwamba kodi ni suluhisho la kila kitu, au unaamini kuwa kodi siyo solution ya kila kitu.

Ili utoke kwenye mtazamo mmoja na kuenda kwenye mwingine, inabidi upitie kitu kinaitwa Paradigm Shift. Kwa lugha ya malikia ni EPIPHANY - "an experience of sudden and striking realization"

Napenda uamini kuwa migodi ilipoanza kuingia TZ, miaka ya 1997, nilikuwa naamini kama wengi wanavyoamini sasa hivi - ya kuwa mrahaba wa 3% ni unyonyaji. Nakumbuka kuwa nilikuwa nimejiaminisha kabisa mtazamo huo na usingeweza kunishawishi vingine.

Baadae katika kujishughulisha kwangu sana na hii tasnia, katika ngazi zilizoniwezesha kupata ufahamu wa dhati kinachoendelea, kuona ni jinsi gani hii migodi iinaleta fursa kwa watu wanaojituma, baada ya kuona jinsi mrahaba wenyewe unavyoliwa na akina Alex Stewart na baadae ma beauracrats, na baada ya kujichanganya na wanazuoni kutioka mataifa mbali mbali, nikapata hili li epiphany. Leo hii naangalia watu wanavyoshindwa kuelewa huu uwekezaji na huwa nasikitika kwamba na mimi nilikuwaga hivyo
 
Nakubaliana na wewe na isitoshe wamekua hawalipi kodi inavyotakiwa waondoke na airport tutawasindikiza.
 
Mwandishi amekosea kidogo. Uwekezaji katika migodi tu ni zaidi ya Dollar Billion 5. Hiyo 433 Million haitoshi hata kujenga mgodi mmoja mkubwa.

Inasikitisha sana kuwa wawekezaji wakubwa namna hii wanaodoka. Inasikitisha zaidi unaposoma mabandiko ya wana great thinkers yanayosema uwekezaji ni unyonyaji. Kwa mtindo huu tutaendelea kuwa omba omba huku tumekalia utajiri.

Dunia nzima ni hawa hawa akina Barrick, Anglogold etc wanaofanya hizi shughuli. Ni kwa nini ishidikane hapa TZ tu?

waende zao tu hakuna walichosaidia maana watanzania hata budget ya nchi bado tunategemea wafadhili wakati tuna madini
 
Nini unachotaka kujenga hapa!! Kuna mwizi ambaye hajui anachofanya ni uhalifu!? Hata kuwatumia vipofu ili kuiba ni wizi tu! Umejaribu kuelezea "mrahaba" umeshindwa hebu linganisha na mikataba ya nchi nyingine uweze kutoa ujumbe unaotaka kutoa. Hebu angalia mkataba wa mafuta ambao Kenya imeanza kuchimba TURKANA. Mjinga akierevuka mwovu huwa mashakani. Uoga uliowaingia hao jamaa ni dalili zote za kuondolewa madarakani kwa makuwadi wao! wanawahi.
Afadhali yabaki ardhini kuliko kuachiwa machimbo tupu na mazingira yaliyoharibiwa na UMASKINI uliopindukia!!. Wote tutafakari unataja faida za madini!! bila aibu!! Miye ukweli sipendi kuibiwa hata kama mali yangu sijui kuitumia ni mali yangu!! LET THEM GOOOOO!!! wajukuu na waje wayakute madini yetu!!

Thanks a million Mangikule. hawa jamaa hawaoni future ya kuiba tena. nasikitika wanatuachia mashimo.
 
washavuna sasa wanaondoka kuwaachia wenzao wavune wakichoka wawaachie wavuneeeee watuacgie mashimo
 
ukweli ni kwamba kuruhusu madini yetu yachimbwe na makampuni ya nje kama barrick na wenzake hakuna faida yoyote kwa uchumi wa tanzania, sikubaliani na dhana kuwa wamewekeza katika mitaji mikubwa hapa nchini, hii ni dhana ya kwenye vitabu vya wahasibu lakini hakuna fedha inayoingizwa nchini katika uwekezaji wa madini .
hawa wanaleta vifaa na machine zote kutoka njee, makampuni ya ndani huwa yana pata tenda za kujenga ndani ya migodi ila nao wanaa agiza vifaaa vyote njee ya nchi hivo hakuna kinachopatikana
  • madini yote yana uzwa nje bila ya taratibu na bila ya uwazi
  • tanzania haifaidiki kuwa na madini mfano ya dhahabu, kuchangia katika akiba yake ya dhahabu nje
  • fedha yote ya mauzo inabaki njee , inaletwa tanzania ni fedha kwa ajili ya matumizi ya ndani kama mishahara ya makabwela nk
hii migodi afadhali mara mia wachimbe walalahoi wetu , hawa watauza hio gold hapa hapa
fedha itapatikana kutokana na kuuza gold itarudi tz kwa asilimia kubwa
walalahoi watakao tajirika na gold watajenga hapa tz
fedha itaingia katika mzunguko hapa bongo na miradi mingi itaweza kufunguliwa kutoka na hawa wauza gold wetu
na kwa vile uchimbaji wetu utakuwa wa kiwango cha chini basi gold hio itabaki kwa muda mrefu(sasa hivi inachimbwa usiku na mchna )
soko letu la dhahabu litaongezeka na wanunuzi watakuwa wengi kutoka nje
banki kuu inaweza kuaanzisha utaratibu wa kununua dhahabu kwa ajili ya akiba
tunaweza kuwa na soko letu la dhahabu yaani sehemu maalum kama mjii mdogo ukajengwa amabpo ni sehemu maalum ya kuuzia dhaahabu .....waliofika dubai wanaweza kujua palle deira souk dhahab...
hawa wamanga hawana dhahabu lakini wana soko la dhahabu na mamia ya watalii wanafika dubai kununua dhahabu tu.
tuwache kukumbatia watu wa nje kwa ajili ya kuchimba dhahabu,na vito vyengine
mafuta hatuna ujanja kwani inahitaji utaalam ambao hatuna
 
hatuhitaji wawekezaji kama hawa, umefika wakati njia kuu zote za uchumi zitaifishwe ili tuanze upya. They can go to hell
 
Tatizo hapa ni kwamba serikali yetu haiwezi kufanya kazi yake kwa kiwango cha kujua kiasi halisi cha madini kinachopatikana.

Pili serikali haijaweza kuwasialiana kiasi cha kutosha kwa wananchi faida hasa za uchimbaji madini kwa wananchi kiasi kwamba watu wanaongea na kuzungumza vitu wasivovijua. Watu wanafikiri faida ya uwekezaji ni mrabaha tu.

Tatu: serikali haijafanyia kazi sheria za ufanyaji kazi kwa wageni kiasi cha kuwapa wazawa nafasi nyeti kwenye migodi. Nafasi nyeti kwenye migodi imebaki miaka na miaka kwa wageni na hata nafasi ambazo zinapaswa kuchukuliwa na wazawa zimechukuliwa na wageni pasipo sababu za kuridhisha na serikali imekaa kimya.

Nne: Tatizo letu wananchi tunafikiri wawekezaji ni maadui na wezi. Wezi wetu tunao serikalini na kwenye makampuni ya ndani yanayoshirikiana na viongozi kutuibia kwa kupandisha mara tatu au mara dufu bei ya miradi ya serikali na huduma zinazolipiwa na serikali.

Tano: Tabia zetu watanzania za udokozi na uwizi zinapelekea wawekezaji kuona usalama wao mdogo mbele ya jamii inayowazunguka. Hiki ni kitu kibaya na ndicho kinachofanya nchi yetu kila idara na kila sehemu kughubikwa na wizi na ufisadi. Na hapa kila mmoja anamlaumu mwenzake. Raia wanalaumu mafisadi wezi ambao wana tabia ya jamii. Jamii inalaumu wawekezaji. Jamii inaingilia shughuli za uwekezaji kwa kuiba na kuhalalisha kuchukua mali ya mwekezaji. Tunaachia wezi wanaingilia shughuli halali na kwa kuwa ni wawekezaji ndio wanaoibiwa wakati mwingine wezi hao wakiiba miuondombinu inayokinga usalama unakuta hawa wezi wanatetewa hata na wanasiasa (kesi ya Nyamongo). Kwa wanaojua mazingira ya uchimbaji ni wananchi mara nyingi wanaoingilia shughuli za wawekezaji hata kuharibu kinga za usalama, au kuumia hapo kwenye migodi; kuna kesi nyingi za vifo vya hawa wanaoingilia shughuli za migodi.

Tatizo kubwa kwetu kutopatikana msuli wa madini kwenye uchumi wa nchi yetu ni kuachia madini yaende nje yakiwa ghafi. Tunauza nje ajira kubwa kuliko tunayopata kwa wawekezaji. Inatakiwa viwanda vya kuchakata dhahabu na madini nyingine ziwepo hapa nchini kwetu badala ya kuvipeleka S. Africa. Zikitoka hapa zinaenda moja kwa moja kwenye soko la dunia.

Kwa yanayoendelea si ajabu wawekezaji wakaanza kufunga virango mmoja mmoja. Wasiojua wataanza kushangilia lakini bila kujua matatizo makubwa ni sisi na kutowajibika kwetu kuweka sheria za uwekezaji kwenye madini na gesi.
Na kwa nyeti inayoanza kujitokeza kwa mbali GGM wanaweza kuondoka Geita au kuuza mgodi wa Geita kuanzia mwakani 2013.
 
Williamson diamond limited(mwadui) from 1940 mpaka sasa, vipi mbona hapa hampagusi? Mi nashangaa watu dhahabu dhahabu,mbona hatuhoji hili la mwadui?

Kama gramu ya dhahabu ni elfu 80'000,na karat 1 (moja) ya almasi = 0.2gramu ni zaidi ya milion why hatuhoji haya?
Mwadui kuna mashimo? Pale hela ipo petradiamond wanakula mda huu kutoka kwa mrithi wake dibears!
 
Back
Top Bottom