Wawekezaji waanza kujiondoa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wawekezaji waanza kujiondoa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 17, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]Ijumaa, Septemba 14, 2012 09:06 Mwandishi wetu
  [​IMG][​IMG][​IMG]

  KUFUNGWA kwa migodi ya dhahabu ya Tulawaka Biharamulo, Resolute ya Nzega, na Barrick kuwa katika mipango ya kuuza zaidi ya hisa zake asilimia 70 kwa makampuni ya madini ya China yaitwayo China National Gold Group, ni ishara kwamba Tanzania itapoteza nafasi yake kama nchi ambayo kwa kipindi cha miaka zaidi ya ishirni, imeweza kuvutia mitaji mikubwa ya kuwekeza katika uchumi wa nchi.


  Katika kipindi cha miaka 25 iliyopita Tanzania imeweza kupokea au kuingiza kwenye uchumi wa nchi vitega uchumi vyenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 433, kiasi kikubwa kimewekezwa kwenye sekta ya madini, sekta ya viwanda, usafirishaji, fedha na mawasiliano. Tanzania imekuwa na sera ya kufungua milango kwa ajili ya kuvutia wawekezaji kutoka nje. Nchi za Uingereza, Afrika ya Kusini, Canada, Kenya na India zinaongoza kwa kuwekeza vitega uchumi nchini. Ni ukweli usiopingika kwamba Tanzania imenufaika sana na uwekezaji kutokana na kupatikana ajira zipatazo zaidi ya 150,000 za wazi na za kuhudumia miradi.


  Hata hivyo uwekezaji nchini Tanzania na katika nchi changa ulipungua sana kutokana na mtikisiko wa uchumi duniani ambao ulitokea kati ya mwaka 2008 na bado unaendelea. Miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na miradi ya uwekezaji ilisimama hapa Tanzania kama vile mradi wa madini ya Nickel wa Kabanga Ngara na mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi huko Mtwara ambao ulikuwa utekelezwe na Kampuni ya Artumas ya Canada. Hata hivyo Tanzania ilipita katika kipindi hiki kigumu kutokana na ukweli kwamba uchumi wetu unategemea uchumi wa dunia kwa kiasi na si kikubwa sana.


  Sababu nyingine ambazo zimeanza kufanya wawekezaji wapunguze kasi yao kuwekeza Tanzania zinatokana na mpangilio wetu wa ndani hasa kuhusiana na malumbano ya kisiasa na jinsi sera na sheria za uwekezaji zinavyotazamwa na jamii nzima hasa vyama vya siasa na wanasiasa kwa upande mmoja na pia wanaharakati na mashirika ya kutetea haki za binadamu, pamoja na jinsi vyombo vya habari vinavyoandika masuala yanayohusu miradi ya uwekezaji.


  Kwa muda wa miaka saba sasa vyombo vya habari, wanasiasa na hata Wabunge, kwa kiasi kikubwa wamechangia kuwaona wawekezaji kutoka nje kama wezi wa mali ya umma na rasilimali za nchi. Mtazamo huo umetokana na jinsi mikataba ya uwekezaji inavyokuwa ya siri, inavyokuwa na vipengele vinavyowapendelea wawekezaji na pia kiasi halisi ambacho nchi inapata kwa kipindi cha muda mfupi ambapo shughuli za uzalishaji au utoaji huduma zinapoanza.


  Kwa namna moja au nyingine dhana ya mrahaba haikueleweka. Watu wengi walifikiri malipo ya mrahaba ndiyo malipo nchi inayoyapata kutokana na madini yanayochimbwa. Lakini dhana ya mrahaba ni tofauti na ufahamu wa watu wengi.


  Maana ya mrahaba ni kiasi cha thamani ya madini (kati ya asilimia 2 mpaka 10) ambacho nchi inapata kwa ajili ya vizazi vijavyo ambavyo vitakuta madini yamemalizika. Hivyo kiasi hicho siyo malipo kwa madini ya nchi ambapo yanachimbwa bali ni kwa shughuli nyingine.


  Kwa upande mwingine madini yana mikataba yake ambayo inatamka wazi masuala ya kodi na malipo mengine. Suala la mikataba ni suala la kitaalamu na uzoefu katika fani hiyo. Kutokana kwamba nchi nyingi hasa nchi changa hazina uzoefu na wataalamu wa kutengeneza mikataba yenye manufaa kwa nchi zao basi mikataba mingi imekuwa ya kinyonyaji na hivyo haileti faida kwa nchi husika.


  Mikataba mingi ina vipengele ambavyo vinazifunga nchi zenye madini kutoweza kutumia enzi na haki za kisheria kufanya mabadiliko ambayo yataleta faida kwa pande mbili zinazokabiliana. Hivyo mikataba mingi ya uwekezaji katika madini ni kweli haina faida hasa kwa kuzingatia mapungufu katika miundombinu na pia mapungufu katika utoaji huduma za kitaalamu, kiteknolojia na kifedha.


  ManungÂ’uniko ya watu wengi kwa kiasi kikubwa yamewalenga wawekezaji wageni badala ya kutambua kwamba ni Watanzania wenzetu ndiyo wamesababisha misiba na rasilimali ya nchi kuondoshwa bila chochote tunachokipata. Hata hivyo tabia ya Watanzania kutojifunza haraka na kuchangamkia tenda hasa katika maeneo yale ambayo akili, nguvu na uwezo vinahitajika kwa madhumuni ya kudhibiti mazingira imewafanya Watanzania wengi wapende kufanya kazi za uchuuzi badala ya kufanya kazi za kutumia nguvu, akili na mahesabu kwa malengo ya muda mrefu lakini yenye faida kubwa.


  Tukichukulia mfano wa nini mahitaji ya huduma katika migodi yetu, ni wazi chakula, huduma za usafiri, huduma za fedha, na huduma nyinginezo ni mambo muhimu ambayo yanagharimiwa kwa kiasi kikubwa cha fedha na makampuni ya migodi. Lakini Watanzania wanalalamika kwamba makampuni ya migodi yanaleta chakula na kutegemea huduma nyingine kutoka nje badala ya kuzipata huduma hizo kutoka ndani ya nchi.


  Tukijiuliza kuna makampuni mangapi ya kutoa huduma kwa mahitaji ya makampuni makubwa ya migodi, ni makampuni machache ya watanzania yanayoweza kutoa huduma hiyo na pia kutokana kwamba watu wengi wamezoea kufanyia shughuli zao katika sehemu za mijini, ni makampuni machache yanaweza kuwa tayari kwenda kufanyia kazi huko maporini kwenye migodi.


  Tukirejea katika Bunge na kwenye vyombo vya habari, mambo mengi yaliyokuwa yanasemwa na kuandikwa hayakuainisha matatizo ya mfumo na sheria dhidi ya matatizo ya hujuma ambazo zinafanywa na makampuni. Kwa namna moja au nyingine madai ya wizi, ufisadi na serikali kuonekana inashambuliwa kwamba imeshindwa kazi ni mambo ambayo wawekezaji wanayafuatilia sana na yanatabiri bila kuwa na uhakika kwamba Tanzania inawezekana ikakumbwa na machafuko. Kwa upande mwingine Wabunge wamekuwa wakitoa shutuma kali ambazo zinawafanya wawekezaji kutangazwa kama wezi ambao kazi wanayojua kuifanya vizuri ni kuziibia nchi changa kama Tanzania.


  Kwa wataalamu wa masuala ya uwekezaji Tanzania ni nchi ambayo imejengewa na taswira kwamba huko mbeleni inaweza ikawa na machafuko. Waliojenga taswira hiyo ni Watanzania wenyewe ambao baadhi yao ni wasomi, wanasiasa na watu wengine walioko katika biashara na menejimenti ya viwanda.


  Shirika la Barrick ambalo linaongoza katika uchimbaji madini ya dhahabu kwa kuamua kufunga virago na kuuza migodi yake wakati dhahabu ni madini ambayo thamani yake imepanda sana katika soko la dunia ni wazi kwamba kuna matatizo ya kimkakati ambayo Shirika la Barrick na wawekezaji wengine wamebaini.


  Tanzania haina sababu ya kujivunia kuwa na wanasiasa wenye uwezo wa kulumbana. Tanzania tunapaswa kujivunia kuwa na watu wenye uwezo wa kuchambua hali na kutafuta majibu ya matatizo yetu ya ndani na matatizo ya nje. Suala hili la wawekezaji kupunguza kasi yao ya kuwekeza ni suala ambalo lazima tulifanyie kazi na kujua kwa nini yamezuka matatizo.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Waache waondoke... Kwanini wanataka wachimbe mashimo nchi nzima na bado kutuacha MASIKINI?

  Waondoke Madini hayaozi humo ndani ARDHINI
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Barrick wameshachuma vya kutosha, miaka zaidi ya kumi na tano bila kulipa kodi si kidogo. Pia nadhani wanaangalia hali ya siasa. Wametambua huenda CCM isiwepo madarakani daima kuwakingia kifua. Wenzetu huangalia mbali zaidi ya pua zao.
   
 4. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi ndo inaanza kwa matokeo ya kutoa raslimali bila kufuata taratibu au ile 10% inaanza kufanya kazi.
   
 5. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,534
  Likes Received: 10,452
  Trophy Points: 280
  wameshapima upepo. Walijua watatunyonya miaka yote kasi ya M4C imewachanganya sana.!
   
 6. Kakende

  Kakende JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 2,734
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Waende zao, hatuwataki, acha tuendelee na umasikini wetu. Tutachimba wenyewe, why not Tanzanians? we can. Wakiondoka wote tutashangilia
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mwandishi wa hii makala ameacha hoja za msingi sana kuhusu uwekezaji kwenye sector ya madini. Mgodi wa Tulawaka unakaribia mwisho - financial viability. Kwa sasa Barrick kuendelea na huo mgodi hakuna tija kwa sababu dhahabu imepungua/karibia kuisha. Huu mgodi ulikuwa wa wazi (open pit) na miaka ya karibuni wakaenda underground kwa kiasi, hata hivyo financially, it does not make sense kuendelea nao.

  Sasa, dilema inakuja, what to do na mashimo? Tukumbuke haya ni mashimo makubwa sana na ukisema yafukiwe itachukuwa miaka na gharama zake ni kubwa mno. So, practically speaking mashimo yatabakiwa wazi. Hata hivyo kuyaacha wazi kunaleta shida nyingine, wananchi watavamia hilo eneo na kuendelea kuchimba walau waambulie mabaki, huku watu wa mazingira nao wanalia, wakati huo huo dunia/activist wataanza kusema Barrick imeacha mashimo makubwa, na reputation ya Barrick itazidi kudorora. So what do you do? Unamuuzia Mchina amalizie viji-mawe vilivyobakia. Afukie mashimo au la, hayo ni Mchina na kama tujuavyo Mchina haguswi na kelele za mazingira, haki za binadamu or anything.
   
 8. L

  Leodgard Member

  #8
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waondoke tuuuuuuu! Wanyonyaji hao
   
 9. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  kwa muono wangu ni kuwa hao wawekezaji wameona mmhh, 2015 makamanda wakiingia hatuna chetu tena bora tusepe mapema. ni hilo tu,nothing else.
   
 10. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Badirisha Title uandike "Wezi waanza kujiondoa Tanzania"
   
 11. z

  zamlock JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  swali la msingi dhahabu imebakia? Au wachache wamekula na wawekezaji? huu ni upuuzi wa hali ya juu tunaachwa na umasikini ule ule eti tanzania iliweza kutoa ajira 150,000? Kati ya watu milion 45? Wewe mkapa na wewe kikwete hii nchi itawalilia sana
   
 12. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,992
  Likes Received: 1,046
  Trophy Points: 280
  Resolute (T) Limited, uliopo Nzega, Km 18 nje ya Mji barabara iendayo Shy kutokea Dar. Menejimenti yao nasikia ime-hamisha moja ya mito iliyokuwa ikipita jirani na Mgodi huo na kuuelekezea kwenye Main-PIT. Lengo lao ni hilo SHIMO (PIT) liwe Bwawa na wananchi waanze kutumia maji hayo as from this masika.

  Taarifa toka huko Nzega zinasema jamaa wanaondoka this year 2012......

  Tofali la kwanza la Mgodi huo wa Resolute lilitengenezwa hapo 1999 na Mr. Clean ndo alifungua Mgodi huo.
   
 13. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Nenda mwanakwenda! Wasingeuza shares, warudishe kwa serikali. Tutengeneze sera nzuri za kutunufaisha wote. Network yao imeanza kuwa halijojo eeh!
   
 14. J

  Jozdon Member

  #14
  Sep 17, 2012
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ninaomba kama inawezekana hizi comments zetu zihifadhiwe na tuje tusome tena kujitafakari baada miaka kama mitano hv ya khali hii!
   
 15. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 882
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  Mwandishi amekosea kidogo. Uwekezaji katika migodi tu ni zaidi ya Dollar Billion 5. Hiyo 433 Million haitoshi hata kujenga mgodi mmoja mkubwa.

  Inasikitisha sana kuwa wawekezaji wakubwa namna hii wanaodoka. Inasikitisha zaidi unaposoma mabandiko ya wana great thinkers yanayosema uwekezaji ni unyonyaji. Kwa mtindo huu tutaendelea kuwa omba omba huku tumekalia utajiri.

  Dunia nzima ni hawa hawa akina Barrick, Anglogold etc wanaofanya hizi shughuli. Ni kwa nini ishidikane hapa TZ tu?
   
 16. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mchango wowote toka kwa Ole Naiko?
   
 17. m

  makeda JF-Expert Member

  #17
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Yaleyale leo sheraton,kesho movenpick,etc.
  Tangu lini wazungu wakahofia atakachofanya mwafrica?si ndo huwa wanacelebrate kuwa atlist tutapata damu ya kutoa sadaka,kwa garama yoyote.watawasupply silaha.leo imekuaje mnajali watakachofanya watu weusi huko mbeleni?
  washavuna wameridhika au ni zamu ya mtu mwingine,mana wanavuna kwa zamu.
  kuna nchi ukitembea tanzanite imezagaa utasema njugu leo mnajifanya eti....
  Wakiondoka au wakiendelea kuwepo yote sawa mana viongozi tulionao ni walewale tu waliokuwa wanauza mababu zetu kwa vipisi vya sigara n.k kuwafanya watumwa,sjaona tofauti.
   
 18. papason

  papason JF-Expert Member

  #18
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Wasiruhusiwe kuondoka adi wafukie mashimo yalio chimba na wasafishe maji ya mito, maziwa, mabwawa waliyo ya contaminate kwa hizo cynide solutions (radioactive) na arsenic !

  Dhahabu watuuibie alafu watuachie sumu na mahandaki?

  Kwa hata hao wachina wanatapeliwa bure tuu, sidhani kama wanajua kuwa wacho kwenda kununua ni community conflict rather than a normal business!

  Kuna haja ya wanaharati kuingilia kati na kuwaelimisha hawa wachina!
   
 19. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #19
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Yansozaaaaaa??? Boraa yesheeeee!!
   
 20. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #20
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hawa wazungu na ripoti zao za kujisifia juu ya uwekazaji wao wa kinyonyaji unakera. Hiyo faida ya uwekezaji kwenye madini iko wapi. Inabidi Sub Committee ya bunge inayohusu mambo ya uchumi, fedha na madini, wafanye critical assessment juu ya hili swala la 'faida ya uwekezaji kwenye madini'...
   
Loading...