Wauzaji wa simu muwe na huruma

Wauzaji wa simu muwe na huruma

Huko hakuna wezi ?; Ebay Aliexpress ni platform za wauzaji na wanunuzi unless ufanye due dilligence ya kuangalia comments na reviews za wanunuzi wengine..., angalau ongelea Amazon
Kote wezi wapo na kokote kule mtu unatakiwa kufanya due diligence. Lakini faida ya kununua mitandaoni ni kuwa mnunuzi una nafasi kubwa ya kulindwa endapo utakuwa umefanyiwa udanganyifu na muuzaji. Unaweza kurejeshewa fedha yako yote au kiasi au kubadilishiwa device nk tofauti na kariakoo, ndio sababu ya kusema ni bora ununue mitandaoni.
 
Assume nataka iphone zinazotoka EU au US?
Eu ndio, US ndo hayo mafamba Ya Dubai,

Ukiskia simu ni refurb ujue imetoka Us, China, Japan, Korea au Uk

Iphone Og kachukue kwa Certified store.

Kwa Tanzania
1. Elife system aka Tigoshop
2. Istore
3. Tech360

Hao pekee ndio wanatambulika
 
Eu ndio, US ndo hayo mafamba Ya Dubai,

Ukiskia simu ni refurb ujue imetoka Us, China, Japan, Korea au Uk

Iphone Og kachukue kwa Certified store.

Kwa Tanzania
1. Elife system aka Tigoshop
2. Istore
3. Tech360

Hao pekee ndio wanatambulika

Shida sio kununua hayo maduka tatizo ni kwamba muda ambao utanakua umejichanga ukapate walau ka 12pro tayari unakuta apple washatoa mzigo mwingine mfano 15 kwaiyo hayo maduka sasa hayawezi tena kuuza izo 12mini sijui 12 lazima waweke matoleo ya juu zaidi kuepuka hasara sasa hapo ndipo kuuziwa refurb kunapoanzia
 
Shida sio kununua hayo maduka tatizo ni kwamba muda ambao utanakua umejichanga ukapate walau ka 12pro tayari unakuta apple washatoa mzigo mwingine mfano 15 kwaiyo hayo maduka sasa hayawezi tena kuuza izo 12mini sijui 12 lazima waweke matoleo ya juu zaidi kuepuka hasara sasa hapo ndipo kuuziwa refurb kunapoanzia
Hapa refurb inakuhusu ndio kama Kitu hadi mwenyewe Apple hauzi unategemea nini. Inabidi tu uwe makini,

Zipo refurb ambazo ni certified na Manufacture sema hizi hadi uagizishie nje.
Refurbished iPhone Deals - Apple
 
Mimi naona cha muhimu watu waachane na flagship zilizotoka miaka zaidi ya mitatu nyuma. Ni kutafuta majanga kama huna uzoefu na simu.

Tena hiz samsung used zona overheat had kero ka pasi
..
Ka una ka laki sita kako badala ya kununua sijui S10+ plus used from Dubai bora udake hata A33 mpya....
 
Mie naona cha muhimu watu waachanae na flagship zolozotoka miaka zaid ya mitatu nyuma ni kutafuta majanga kama huna uzoefu na simu....

Tena hiz samsung used zona overheat had kero ka pasi
..
Ka una ka laki sita kako badala ya kununua sijui S10+ plus used from Dubai bora udake hata A33 mpya....

Bongo hatuendi sawa na muda yani mfano leo hii kuna watu bado wanaenda kununua samsung s9 amabyo inaishia android 12 sasa android saiv wapo 14 hiyo simu unategemea itapata features mpya?
 
Habari za muda wakuu poleni pia hongereni kwa harakati za kulijenga taifa. Okay bila kupoteza muda niende.
Kwenye mada husika

Je ni wangapi, wamewahi pigwa vifaa vya tech ikiwemo simu, Laptops na vinginevyo hapa bongo? Najua ni wengi sana imeshawakuta hii nita-share kidogo. Kilichonikuta huko nyuma maana naona baadhi ya watu bado hawana.

Elimu juu ya hivi vitu na na jinsi ya kupata kitu bora hapa Bongo. 2019 nilipata vijipesa nikasema niende sasa nikanunue simu unajua. Kuna raha yake kufunguwa mzigo ukiwa sealed na magandayae eeeh!?!

Nikaingia K/Koo duka fulani la wapemba. Simu nilio panga kuchukua ni S8+ lakini bahati mbaya sikufanikiwa muuzaji akanishauri nichukue S7edge nikalidhia lakini rangi nilioitaka haikuwepo jamaa akaniamba ngoja nikakuchukulie kwenye duka letu lingine aisee! kumbe hapo ndio nilifanya mistake.

Alivyorudi nikaikagua ile simu ipo fresh. Akaniandikia risiti nikarudi zangu home sasa nafika niichaji ili niitumie.
Huwezi amini simu inapata moto vibaya halafu kwenye notification chini. Inaonyesha mwanga hadi ndani.

Yaani inamaana simu ilishakarabatiwa. Nilivokuja kuiwasha dakika 20 simu imezima uichaji tena daah! Nilijilaumu Sana bora hata ningerudi na pesa yangu tu..

Najua humu humu kuna wauza simu wengi sana watanishambulia kuhusiana na hili ila kiukweli watu wanatafuta pesa kwa tabu mno angalau wapate kitu bora lakini mmekuwa watu wasio na huruma..

Mnadanganya watu simu ni used from Dubai, UK, US, Sijui wapi wapi ila wengi ni waongo simu refurbished hapa hapa bongo nina kesi nyingi sana za watu kupigwa mtu baadhi yenu si waaminifu kwa wateja hivi...

Mfano iphone 6plain ni ya 2014 huko. Lakini mtu anakuja kukwambia ni full box, sealed na iko Non active. Kweli inawezekana vipi muwe wakweli.

Halafu kinachoumiza ni mnauza midosho then kwa bei ya mbaya nimeacha kabisa kununua simu K/Koo

Sijui makumbusho maeneo ni balaaa. Sisemi hakuna maduka yanayo uza vitu genuine kabisa hapana wapo ila ni wachache walio waaminifu ushauri wangu ni kama umepata pesa usikimbilie kwenda kununua vitu hivi
Tuliza kichwa fanya research duka gani lina utapata bidhaa original Lakini sio kariakoo.

Usisite kuweka maoni au ku-share jambo lililowahi kukuta kama hili. Ili na wengine iwasaidie unaweza kuokoa hela ya mtu siku ya leo.
🤣🤣🤣 Hapa jamaa aliuziwa iphone afu ikawaka Samsung
 
Back
Top Bottom