Wauzaji wa simu muwe na huruma

Itscharlie

JF-Expert Member
Apr 15, 2022
3,794
15,772
Habari za muda wakuu poleni pia hongereni kwa harakati za kulijenga taifa. Okay bila kupoteza muda niende.
Kwenye mada husika

Je ni wangapi, wamewahi pigwa vifaa vya tech ikiwemo simu, Laptops na vinginevyo hapa bongo? Najua ni wengi sana imeshawakuta hii nita-share kidogo. Kilichonikuta huko nyuma maana naona baadhi ya watu bado hawana.

Elimu juu ya hivi vitu na na jinsi ya kupata kitu bora hapa Bongo. 2019 nilipata vijipesa nikasema niende sasa nikanunue simu unajua. Kuna raha yake kufunguwa mzigo ukiwa sealed na magandayae eeeh!?!

Nikaingia K/Koo duka fulani la wapemba. Simu nilio panga kuchukua ni S8+ lakini bahati mbaya sikufanikiwa muuzaji akanishauri nichukue S7edge nikalidhia lakini rangi nilioitaka haikuwepo jamaa akaniamba ngoja nikakuchukulie kwenye duka letu lingine aisee! kumbe hapo ndio nilifanya mistake.

Alivyorudi nikaikagua ile simu ipo fresh. Akaniandikia risiti nikarudi zangu home sasa nafika niichaji ili niitumie.
Huwezi amini simu inapata moto vibaya halafu kwenye notification chini. Inaonyesha mwanga hadi ndani.

Yaani inamaana simu ilishakarabatiwa. Nilivokuja kuiwasha dakika 20 simu imezima uichaji tena daah! Nilijilaumu Sana bora hata ningerudi na pesa yangu tu..

Najua humu humu kuna wauza simu wengi sana watanishambulia kuhusiana na hili ila kiukweli watu wanatafuta pesa kwa tabu mno angalau wapate kitu bora lakini mmekuwa watu wasio na huruma..

Mnadanganya watu simu ni used from Dubai, UK, US, Sijui wapi wapi ila wengi ni waongo simu refurbished hapa hapa bongo nina kesi nyingi sana za watu kupigwa mtu baadhi yenu si waaminifu kwa wateja hivi...

Mfano iphone 6plain ni ya 2014 huko. Lakini mtu anakuja kukwambia ni full box, sealed na iko Non active. Kweli inawezekana vipi muwe wakweli.

Halafu kinachoumiza ni mnauza midosho then kwa bei ya mbaya nimeacha kabisa kununua simu K/Koo

Sijui makumbusho maeneo ni balaaa. Sisemi hakuna maduka yanayo uza vitu genuine kabisa hapana wapo ila ni wachache walio waaminifu ushauri wangu ni kama umepata pesa usikimbilie kwenda kununua vitu hivi
Tuliza kichwa fanya research duka gani lina utapata bidhaa original Lakini sio kariakoo.

Usisite kuweka maoni au ku-share jambo lililowahi kukuta kama hili. Ili na wengine iwasaidie unaweza kuokoa hela ya mtu siku ya leo.
 
Kununua hizo simu za brand kubwa kariakoo kuna asilimia kubwa sana ya kupigwa.

Kule ni kwa kununua simu za kichina hizi, tecno, infinix, redmi,itel nk
Hizo nyingine ni bora uagize ebay, aliexpress nk

Kununua hizo simu za brand kubwa kariakoo kuna asilimia kubwa sana ya kupigwa.

Kule ni kwa kununua simu za kichina hizi, tecno, infinix, redmi,itel nk
Hizo nyingine ni bora uagize ebay, aliexpress nk

Ni afadhali ebay na amazon mkuu alie express sijui alibaba unapigwa kama kawa huko ndo wamejaaa matapeli.
Na wanaongoza kwakuuza vitu feki..
 
Hivi hawa majamaa wanaouza simu ila ukienda sukani unakutana na macover na charger tu badala ya simu, je kuna usalama au ndio ukijichanganya unapigwa?

Usalama upo mdogo sababu ukiulizia simu fulani kama hawana wanakwambia subiri kidogo kuna duka letu lingine lipo hapo mbele nikakuchekie ukiruhusu akakuchekie hapo ndo umeumia.
 
Mtapigwa sana!!


20230209_141942.jpg
 
kama ujui kununua chochote tafuta mtaalamu wa kununulia.ijalishili simu,gari,nyumba,ardhi na mengine.
ujuwaji unaponza sana .
kuna kipindi nilijifanya nataka kununua gari kilichonitokea niliuza bila kupenda tena bei ya chini

Kama umepata pesa na ulikuwa na plan za kununua kitu nashauri utulize kichwa unaweza kujikuta unanunua kitu ambacho kinakiwa out of your plans na baadae unajutia kwanini usinge bakiza pesa yako tu.
 
Tatizo lako mleta mada uliruka stage kwenyebkujifunza namna ya kuishi.

Kwenye maisha unatakiwa ujuane na watu ili upate mambo mazuri.

Unajijua utakuja kijenga nyumba kuwa karibu na mafundi wanaosifika kwa ubora baadae hutapata tabu.

Unajijua utakuja nunua gari jenga mahusiano na watu wenye uzoefu na magari.

Usikubali kufanya kitu kama kipofu hapo hapo kkoo watu wananunua simu kali safi na og kwa mtonyo mzuri tu ww unakwama wapi.

Sikushauri kuwa mjuaji ila jitahidi uongee na watu vizuri.


Mfano mimi nikitaka simu hata leo navuta uzi mmoja tu simu inaletwa mpka kigamboni lakini hii inatokana na kujenga mahusiano mazuri na wauza simu wanaoaminikana kujali kazi zao.

Alafu jambo jingine ukienda kununua kitu chochote kipya au unachokipenda punguza matamanio jiamini chukua muda wako kukichunguza.

Imagine mtu ananunua simu hajaribu hata kupiga ajue iko nzima haweki hata chaji aone inafanyakazi yeye akikabidhiwa ni mwendo hii si sahihi maana maduka mengine garantii ni mgongo wako ukigeuka tu na garantii imekwisha.
 
Aisee humo K/Koo, chukua simu used iliyo uchi.

Kamwe usidanganywe na mabox utalia, kuna watu humo wanafunga frem wanahudhuria sala zote 5 lakini linapokuja swala la kukupiga hawaangalii hayo, wanakuumiza tu.

Kuna ki iphone 6s nilinunua 2021 jamaa akanambia hiki ni used from amerika kiko uchi tu, aisee kile kidude kilikuwa poa bana BH 75% ilikuwa inakaa charge.

Hiyo mi full box hakuna kitu ni kutoka hapo dubai imefanyiwa repair wanakuja kuifungwa ktk mabox hapa hapa.
 
Ni afadhali ebay na amazon mkuu alie express sijui alibaba unapigwa kama kawa huko ndo wamejaaa matapeli.
Na wanaongoza kwakuuza vitu feki..
Ni kweli mkuu. Manunuzi ya online ni kuwa makini, kuzingatia bei pamoja na rate za muuzaji. Kama alivyosema Chief-Mkwawa ali express ni vyema kuitumia kwa vitu vya kichina, hizi simu brand ukizikuta aliexpress bei yake tu inakushtua maana ni kubwa kuliko hata zilizopo Bongo Tanzania.

Ebay kumenyooka maana wazungu wakweli sana, wanasema condition ya simu na kutuma picha jinsi ilivyo, tofauti na wachina wanaweka picha zile za graphics za kwenye mabango.
 
Back
Top Bottom