Waumini wa Kakobe kutimuliwa alfajiri ya leo!!!

Waumini wa Kakobe kutimuliwa alfajiri ya leo!!!

hivi wale watu wanaolala pale hawana familia? wanawake wote wale ina maana hawana waume zao na watoto majumbani? wale wanaume hawana wake? Kakobe nae huwa anakesha pale?...watalinda mpaka lini? ni wote wanaaga nyumbani kwao wanaenda kulinda kanisa na wanatimiza azma hiyo? hakuna upotofu wa uaminifu katika ndoa za wakeshaji wale walinzi?na je kama tanesco wakija wao wanatakiwa kuwafanya nini tanesco?....kama kuna mtu ana majibu anisaidie kufahamu tafadhali
 
1. Nani alimpa kakobe kiwanja hicho?

2. Nani alimpa kakobe kibali cha kujenga?, je kibali kinasemaje kuhusu mipaka ya kujenga?.

3. Kama alijenga kimakosa kwanini aliachiwa kujenga mpaka kufika hapo alipojenga?.

Tumekuwa na watumishi wajinga sana ndani ya serikali na ndiyo wanaoitukanisha serikali yetu kwa wananchi. Jiji kama Dar es salaam lilitakiwa liwe na mpangilio madhubuti na unaoeleweka ili ujenzi holela usitokee.

Tumeshuhudia wananchi wengi ndani ya Dar es salaam wanavunjiwa majumba yao kwa sababu mbalimbali kama upanuzi wa barabara, airport, kambi za jeshi nk. Walikuwa wapi watu wa mipango (Planing) kujua mahitaji hayo kwamba yataongezeka (Mabarabara, airport nk) na kuzua kujenga katika maeneo husika?.
Kwanini wananchi wanapewa viwanja na hati ya kujenga katika maeneo kama hayo?.
 
Barabara wa Tanesco pamoja na kikwete ndo dili lao. misikiti haivunjwi, lakini kukiwa na kanisa tu, wanavunja kwasababu wakristo si watu wa jino kwa jino. kuna upendeleo mwingi sana na unyanyasaji kwa wakristo tangu kikwete aingie madarakani, ila kwasababu wakristo huwa hawalipukilipuki ndo maana hawa hatusemi. nashauri selikali iliendee suala hili kwa umakini na uangalifu, kwasababu doa moja likiwekwa ni vigumu sana kulifua kwa miaka mingi. ikumbukwe sisi sote ni watanzania, hata kama wengine ni walokole, ambao naona wengi humu mnawachukia just because ni walokole, tuna haki zetu pia kama watz, na tunayo sauti kubwa tu humu nchini. chatu simba akilala usifikiri amekufa...ukitaka ujue kama bado yu hai, gusa mtoto wake. period.
 
ingekuwa waislam hapo, wasingejisumbua kuumwa na mbu pale kila siku, wange andamana kufunga hadi barabara magari yasitembee, lakini kakobe wa watu amefanya non violent response kama vile. hivi mnataka afanye nini ili mjue yuko serious na haki yake anayodai?
 
Barabara wa Tanesco pamoja na kikwete ndo dili lao.

Hapo sijakuelewa una maana gani. Tafadhali kabla kwenda kwenye issue ya udini ni muhimu tukaangalia sheria zinasemaje kama nilivyouliza maswali hapo juu. Tusipende kumlaumu JK kwa kila upuuzi tafadhali.
 
Hongereni waumini mnaonyesha ni jinsi gani mlivu na uchungu na kanisa lenu haya jamni watanzania tuamke sasa kama tunataka maendeleo ya nchi yetu sio kuongea tu na kujifungia ndani!
 
mimi siziamini hizi dini mbili za mashariki ya kati, lakini najua athari zake. najaribu tu ku-imagine kama wahusika katika hili sakata wangekuwa waislamu, kwanza hadi sasa wengi wasingeshangaa sana kuhusu zamu za ulinzi pale, na pili tahadhari ya kuwaendea pengine ingekuwa ya umakini zaidi maana wale hawanaga utani na huwa hawaogopi chochote kuhusu kitu kinachogusa imani yao.

Nadhani serikali inahitaji kuwa rational zaidi katika maamuzi yake, na isisubiri mambo yafikie level kubwa hivyo ya mtafaruku ndipo ianze kutafuta consultants nk. Kwani hao TANESCO hawakuwa na strategic plan? Na je eneo hilo katika masuala ya mipango-miji halikuwa na plan? Nani kati ya TANESCO, JIJI na Kakobe aliyeingilia anga za mwenzie?
 
Tatizo ni kwamba, dini za kikristo, haswa walokole, huwa zinadharauliwa sana na selikali. ndio maana selikali inaweza kufanya lolote lile, na haiwaogopi, kwasababu ni watumishi wa Bwana (pamoja na kwamba wao nao ni wanadamu ambao wanaweza kugafirika sometimes). ungekuwa msikiti hapo, hakika wangeshafanya kingine, lakini kwasababu ni kanisa, tena ambalo haliko chini ya Pengo, basi, selikali hata hailijali, na wanatakakuamua lolote lile kulifanya. wajue kuwa, hao walokole ni wengi sana tz, hivyo selikali isipende kupandikiza chuki wa watu wengi hivyo, kwa ufupi, makanisa yote ya kilokole, nikianza na full gospel, waassemblies, efatha, agape, wapentecost, walutheran na wanauamsho wooote wanaomjua Mungu, wanakinyongo sana na jambo hili, na wanaona wanaonewa, mimi mwenyewe naona kuwa tunaonewa. naomba msituchokoze, pamoja na kwamba sisi hatutarusha jiwe, tunaweza kuomba kwa Mungu na Mungu atatusaidia. asanteni.
 
nakuunga mkono ubungo, hii nchi ni ya kwetu sote, kwa ufupi, hao waumini pamoja na mimi mwenyewe, TUNAITHAMINI ZAIDI IMANI YETU kuliko hicho kitu kinachoitwa selikali, msifikiri kuwa selikali au hata nchi ya tz ni ya thamani sana kuliko imani yetu ambayo itatupeleka mbinguni, hivyo mnapogusa mahali pa thamani kwetu, jueni kuwa hatuwathamini sanaana kuliko imani yetu. hivyo, mtuache na imani yetu, tunaomba mtuheshimu, muwe na adabu kwetu na kwa Mungu pia, hakika yake anayegusa watumishi wa Mungu anagusa mboni ya jicho la Mungu. wakristo wengine humu wamejaribu kuongea kuliponda kanisa la kakobe, kama hauna uhakika utumishi wa kakobe, nyamaza..mimi sisali pale lakini namheshimu. wengine wanamponda kwasababu tu wao ni wakatoliki na wanamuona kama yeye ni mpinzani wa kikatoliki, msipoteze muda, kama selikali inaona kweli ina ujasiri kuingilia imani zetu kwa kiasi cha kupitiliza, basi iiacheni iendelee, lakini matokeo yake yatakuwepo tu.
 
Halafu tunalalamika kuwa sisi ni watu maskini wakati muda tunauchezea tunavyotaka
wewe ndo masikini, kwani walikuja kuomba chakula kwako? kama wanalala pale, wao wanajua namna gani wanaendesha maisha yao, mbona kila siku pale unawaona wanaenda kanisani wasafi, wameulamba tai, wengine wanaendesha magari ya kifahari kuliko hata lako, unalalamika nini, wameamua kushinda pale, hawajakuja kuomba ruhusa kwako, waache, hayakuhusu.
 
Kwani Tatizo ni nini Hasa, nini Kiini cha Mgogoro Huu, maana naona Hapa kuna Mashabiki wa TANESCO na Mashabiki wa KAKOBE

Sasa Ningependa Mashabiki wa TANESCO waeleze ni kwa nini wanaona ni sawa kwa Nyaya za Umeme kupita pale

Na Mashabiki wa Kakobe waeleze ni kwa nini wanadahani Umeme haustahili kupita pale!

Tuache Ushabiki, tukiwa Bendera fuata Upepo tutakuwa Hatuzitendei Haki Elimu Zetu
 
ulikuwa wapi mzee wakati wa discussion miezi yote hii?

Nimefuatilia Thread zote nimeona Ushabiki tu na Watu kutouliza Maswali ya Msingi na Ndiyo Maana kila kukicha kuna Thread Mpya kuhusu hili Sakata

Sasa kama wewe uko katika moja ya hayo Makundi nijibu Maswali yangu
 
wewe ndo masikini, kwani walikuja kuomba chakula kwako? kama wanalala pale, wao wanajua namna gani wanaendesha maisha yao, mbona kila siku pale unawaona wanaenda kanisani wasafi, wameulamba tai, wengine wanaendesha magari ya kifahari kuliko hata lako, unalalamika nini, wameamua kushinda pale, hawajakuja kuomba ruhusa kwako, waache, hayakuhusu.

Niambie kwa nini Unafikiri Umeme haustahili kupita Pale?
 
Tatizo ni kwamba, dini za kikristo, haswa walokole, huwa zinadharauliwa sana na selikali. ndio maana selikali inaweza kufanya lolote lile, na haiwaogopi, kwasababu ni watumishi wa Bwana (pamoja na kwamba wao nao ni wanadamu ambao wanaweza kugafirika sometimes). ungekuwa msikiti hapo, hakika wangeshafanya kingine, lakini kwasababu ni kanisa, tena ambalo haliko chini ya Pengo, basi, selikali hata hailijali, na wanatakakuamua lolote lile kulifanya. wajue kuwa, hao walokole ni wengi sana tz, hivyo selikali isipende kupandikiza chuki wa watu wengi hivyo, kwa ufupi, makanisa yote ya kilokole, nikianza na full gospel, waassemblies, efatha, agape, wapentecost, walutheran na wanauamsho wooote wanaomjua Mungu, wanakinyongo sana na jambo hili, na wanaona wanaonewa, mimi mwenyewe naona kuwa tunaonewa. naomba msituchokoze, pamoja na kwamba sisi hatutarusha jiwe, tunaweza kuomba kwa Mungu na Mungu atatusaidia. asanteni.

sio vizuri ukamuhusisha katika hili,kwani angekubali kujadiliana si wangefikia muafaka, sio vizuri hao waumini wakatumia ubabe, na sio kweli waislam wanapendelewa hata kidogo hiyo ni imani yako POTOFU,kama ni mradi wa barabara watu wanafidiwa kama na msikiti unavunjwa wanajenga mwingine mfanao barabara ya mbagala, kama linge kuwa ni kanisa wangejenga, acha kutumia uislam na ukristu kutugawanya hapa,
 
Tatizo Nimegundua Watu wanajadili bila Kuuliza Maswali, ni Ushabiki Ushabiki Tu Nimemuuliza Mwana Wa Mungu swali hapo amengia kwenye Miti
 
Back
Top Bottom