Watumwa walikuwa wanaamini wazungu wanawanunua ili kwenda kuwala

Enzi za utumwa hali ilikuwa ni mbaya sana. Mtumwa alikuwa ni mtu wa hogu kwenye safari yake yote. Nafikiri alipofika anapokwenda alipumua kwa ahueni baada ya kujua kuwa ameenda kulima.

Inasemwa kuwa mara tu walipofika pwani na kuona meli huzuni kuu iliwaingia. Macho yao yalionyesha kukata tamaa kabisa. Walijua safari ya kwenda kuliwa imefika. Mara meli ilipotingishika kuondoka, vilio vikubwa sana vilisikika.

Hii hadithi ilitumiwa pia na wafanyabiashara ya watumwa wa kiarabu. Wazungu walipopiga marufuku utumwa, na kuanza kuvamia misafara ya waarabu. Waarabu waliwambia waafrika kuwa wazungu wanawakomboa ili kwenda kuwala.
Hivi kipindi Afrika imeenda kutawala ulaya walijua Sisi tukaenda kuwafanya nin?..

Historia inasema Afrika ilitawala Ulaya kabla ya wao kuja huku.. Kwa bahati mbaya historia inayofundishwa mashuleni inafanya waafrika waonekane kama vile ni wanyonge yani

Inatakiwa tushtuke kama vile China iliamua kushtuka..
 
Mwafrika ndie aliyependa kuchukuliwa utumwani
Historia ya utumwa ipo hata katika Bibilia, Abraham na Lutu walisafiri na mifugo na watumwa wao. Utumwa wa enzi ya Abraham ulimtumikia bwana kwa muda fulani baada ya kile kipindi alikugaia sehemu ya mali yake na kukuacha uwe huru. Na wewe unatafuta watumwa wa kukufanyia kazi.

Capitalism ilibadili dhana hii ya utumwa na kuhakikisha faida yote inabaki kwa tajiri.
 
Kati ya wale waliowachua wenzao na kuwauza a hawa wanaotukata tozo na kununua tofari la saruji kwa 1800 wana tofauti kweli?.
 
Pumbavu zao waliokuwa wanafanya biashara ya utumwa kwa waafrika, wajaribu tena watakiona cha mtema kuni
Mkuu sasa hivi watatumia serikali, jeshi, mgambo, magereza nk.
Watawapa misaada ya pesa na silaha serikali na wanasiasa vichwa maji ili kuwaruhusu kukamata watu wanaowataka.
Watasingizia hao ni wahalifu wasiifaa kuwepo mitaani hivyo bora wauzwe( rejea wasiojulikana na utekaji).
Ikishindikana watatumia vikundi kama boko haramu,al shabab, mungiki, m23 nk.
Dunia ya sasa utumwa kuurudisha ni rhisi zaidi kuliko zamani.
Mtu atahongwa gari anaambiwa nilitee watumwa 100.
Dunia tunayoishi ina watu wa hovyo sana ila wanajifanta wema
 
Hivi kipindi Afrika imeenda kutawala ulaya walijua Sisi tukaenda kuwafanya nin?..

Historia inasema Afrika ilitawala Ulaya kabla ya wao kuja huku.. Kwa bahati mbaya historia inayofundishwa mashuleni inafanya waafrika waonekane kama vile ni wanyonge yani

Inatakiwa tushtuke kama vile China iliamua kushtuka..

Waafrika ni watu kulialia kila day hata aibu hawana 😁 siyo wote, wengine wanajitambua.
 
Fadhila zipo...ndomaana Nyerere Toto la chief lilipataa chance ya kwenda kusoma ulaya
Kinachoshangaza wako MACHIFU waliohusika kuwauza wenzao....je waliwatoa BURE?!!

Je hakuna familia zilizopewa fedha kutoa vijana wao waende wakafanye kazi huko "mbinguni kwa watu weupe"?!!!
 
Pumbavu zao waliokuwa wanafanya biashara ya utumwa kwa waafrika, wajaribu tena watakiona cha mtema kuni

Wazungu hawakuwa wa2 wazuri na adi leo wanachokifanyaa baazi ya nchi inackitisha,,refer iraq, Afghanistan, libya, syria, yemen n.k. wazunguu wanatanguliza masilahi mbele kuriko utu.
 
Dah Mimi Hilo shamba hata saivi ukinipeleka yakawe Maisha yangu fresh tu
kuna sehemu nilisoma wanasema USA kulikua na shamba la kuwafanya watumwa wazaliane hata ndugu kwa ndugu kama mtu anavyofuga nguruwe hivi jamaa anatupiwa hata mademu 40 awajaze mimba
 
Ukisoma hizi comments unajua kabisa TANZANIA inasafari ndefu sn na inahitajika juhudi kubwa sn otherwise Majanga makubwa mbeleni nayaona.
 
Pumbavu zao waliokuwa wanafanya biashara ya utumwa kwa waafrika, wajaribu tena watakiona cha mtema kuni

Siku watu wanajipeleka wenyewe bila kusagwa kama ng’ombe

Hivi meli ikitia nanga bandarini wakasema anaetaka kwenda Ulaya apande
Itajaa kwa mda gani

Kila enzi na zama zake
 
Bila shaka wafanyabiashara wakati ule walisimulia stori za kulingana na biashara sawa na leo, wakati ule stori za kutisha bidhaa (=watumwa) wasitoroke.
Nahisi kwenye hisia za watumwa ilikuwa kubwa huzuni ya kuachwa na kuuzwa na watu wa nyumbani (machifu, majirani) maana Waarabu "walivinda" watumwa mara kadhaa tu, haukuwa njia ya kawaida. Kwa kawaida machifu, viongozi au watawala jirani walikamata watumwa na kuwauza kwa Waarabu. Kila biashara huwa na mwuzaji na mnunuzi.

Basi historia haiendi jinsi tunavyopenda. Biashara ya watumwa ilikomeshwa na Wazungu, Waingereza hasa kuanzia mwaka 1800 hivi, waliokuwa watu walewale waliokuwa wafanyabiasharawakuu wa watumwa duniani hadi mwaka 1800.

Tusishangae
 
Pumbavu zao waliokuwa wanafanya biashara ya utumwa kwa waafrika, wajaribu tena watakiona cha mtema kuni
Babu zako walishindwa kuondoa utumwa wa wazi kabisa mpaka Walipositisha Wazungu wenyewe(Abolition of slave trade)

Leo kuna utumwa wa wazi kabisa na bado hakuna reactions zozote za Mtu mweusi.

Kama Wahindi wanaomiliki viwanda na maduka hapa nchini wanaweza kuwaajiri watanzania wazawa katika nchi yao wakafanya kazi usiku na mchana za kuchochea moto kiwandani na kuchanganya rangi za Nguo, na wengine vibega wa kubeba mizigo 24/7 na mwisho wa siku wanalipwa elfu 70 au 80 huo si UTUMWA wa wazi wa kimwili na kifikra?

Kama Muhindi Mo Dewji anadiriki kumwambia mtanzania kuwa sitaki umshabikie flani kwasababu sio yeye anayekulipa mshahara, huo sio Utumwa?

Utumwa upo na Ukoloni upo.

Sisi yetu maneno tu.
 
Back
Top Bottom