A BITTER TRUTH: Kwanini watu weusi walishindwa kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu (Whites) kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu watanzania;

Kwanini watu weusi walishindwa kuwa wa kwanza kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

Kwanini wazungu/waarabu waliweza kuwa wa kwanza kuwaza kuja kuwazoa babu zetu na kuwafanya bidhaa?

Waafrika tulikosa nyenzo gani za kutufanya kuwa wa kwanza kwenda Ughaibuni kisha kuwazoa wazungu kuja kufanya kazi za kitumwa katika mashamba yatu?

Je, hii inadhihirisha ya kuwa wazungu/waarabu wana kitu cha ziada kwenye akili/bongo zao (highly intelligent) tangia zama za kale mpaka wakawaza kuja Afrika kwa mara ya kwanza?

HILI SWALI WADAU WENGI WANALIKWEPA
Je, kuna umuhimu wowote wa watu wa bara la Afrika kuendelea kulialia na kulalamikia biashara ya utumwa kama ni janga lililowarudisha nyuma kimaendeleo mpaka sasa?

fdfffgggf.jpg

NINAOMBA KUWASILISHA MADA HII FIKIRISHI. KARIBUNI SANA KWA MICHANGO YENU NDUGU ZANGU

KUMBUKA
: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TAFADHALI TIMIZA WAJIBU WAKOIPASAVYO.

Hadi imefikia kuwa weusi ni tusi. Marekani ukimwita mtu mweusi 'nigger' ambayo tafsiri yake ni 'mweusi' utazua ugomvi kama vile umemtukanaje sijui. Lakini mweupe anafurahia sana kuitwa white, na hata kuna weusi wanapenda waonekane au kutambulika kuwa ni weupe, na ukimwita 'mzungu' anafurahi kupita kiasi!
Jitu ukilisifia "huyu mzungu bwana" linakenua hadi basi, kufurahia sifa ya kuitwa mzungu. Ukimwambia ana mambo ya kiafrika anakasirika sana!
 
Sidhani kama waafrika tuna akili tofauti na watu weupe au wazungu. Nachoona ni wenzetu waliwahi kustaarabika na kuendelea kabla yetu na waliweza kugundua vingi kabla yetu hivi hapo ndipo walipotuzidi.

Ila kama ubaguzi usipokuwepo kabisa duniani na mtoto wa kiafrika na kizungu akakuzwa katika mazingira sawa utakuta akili zao zinafanya kazi sawa. Mfano ni mashirika kama FBI ambapo kuna watu weupe na weusi na wote wanapiga mzigo sawa sema kutokana na ubaguzi mweupe atafanywa awe kiongozi wa mweusi
 
1.Technology-mzungu na muafrica walikutana kwa mara ya kwanza mnamo karne ya 15 wakati huo mzungu yupo mbali kidogo katika teknolojia mfano silaha hivyo tusingeweza kuwateka kama tungeenda

2.Umasikini -Mzungu aliweza kufika huku kututeka kutokana na kwamba alikuwa na capital sasa kwa mfano mkwawa angeweza ku finance jeshi lake kwenda Ulaya ?

3.Kutokuwa na Wazo hilo- Mu Africa hakuwa na wazo la kumtawala mzungu kama mtumwa kwa sababu wazungu walimuitaji mtu mweusi kumfanya mtumwa kwenye mashamba ya Miwa nk lakini sisi tuliitajiana kufanyana misukule

4.SABABU ZA KIUTAWALA-Wazungu walikuwa na mfumo mzuri wa kiutawala kwa mfano Uingereza ilikuwa chini ya utawala wa kifalme pamoja na nchi zingine za Ulaya lakini huku kwetu tuliongoz kitemi kila kabila na mtemi wake hivo isingewezekana wote wakubaliane katika kwenda Ulaya na kuteka wazungu
 
Utumwa unaanzia kwenye FIKRA.

Kama una raisi anayehisi kila kitu anahujumiwa anaweza kusafiri kweli? kila kitu yeye ni kulaumu mabeberu, hata ndege akipanda kama haijatengenezwa Tanzania si ataogopa?

Ili kumfanya mtu mtumwa wako, kama UVCCM, wanavyofanyiwa na kuwa watu wa kusifia tu hata mtu akijamba, lazma umfanye awe rafiki yako
 
lakini sisi tuliitajiana kufanyana misukule
1.Technology-mzungu na muafrica walikutana kwa mara ya kwanza mnamo karne ya 15 wakati huo mzungu yupo mbali kidogo katika teknolojia mfano silaha hivyo tusingeweza kuwateka kama tungeenda
2.Umasikini -Mzungu aliweza kufika huku kututeka kutokana na kwamba alikuwa na capital sasa kwa mfano mkwawa angeweza ku finance jeshi lake kwenda Ulaya ?
3.Kutokuwa na Wazo hilo- Mu Africa hakuwa na wazo la kumtawala mzungu kama mtumwa kwa sababu wazungu walimuitaji mtu mweusi kumfanya mtumwa kwenye mashamba ya Miwa nk lakini sisi tuliitajiana kufanyana misukule
4.SABABU ZA KIUTAWALA-Wazungu walikuwa na mfumo mzuri wa kiutawala kwa mfano Uingereza ilikuwa chini ya utawala wa kifalme pamoja na nchi zingine za Ulaya lakini huku kwetu tuliongoz kitemi kila kabila na mtemi wake hivo isingewezekana wote wakubaliane katika kwenda Ulaya na kuteka wazungu


Sent using My COVID-19
 
Kwanini mzungu awe mbali kidogo? Huu ndio msingi wa swali langu. Ina maana wazungu wapo very intelligent tangia zamani sana na ndio maana wanatawala dunia mpaka sasa?
Mkuu tunajibu ki-shabiki lakini swali lako la ki-falsafa sana, natamani nikujibu ila maelezo ni marefu sana.

Imagine Phd-holder wa ki-zungu yupo maabara anatafuta dawa ya COVID-19, Phd wa Tanzania yupo msitu wa Pande na madagaska anakata mizizi kujifukiza ili apone Covid- tena kumbe kanyweshwa Juisi tu maana hata Rais wao Anaugua Corona !

PhD Mzungu akigundua hiyo dawa atauza dunia nzima, Phd wa Tanzania akipona, hajui ni jani lipi limemponyesha, na hana cha kusaidia wengine wala vizazi vyake!



UPDATE: Ile Juisi toka Madagaska iliishia wapi? Tuwape na Wenzetu Houston Texas wanakufa kweli kweli.
 
Bila kuathiri majibu ya watu wengine, sababu ya ziada ninayofikiri ni kwamba inawezekana Wazungu walikuwa na shida nyingi kuliko Waafrika. Kabla hawajagundua teknolojia watu wao wengi walikufa kutokana na mazingira magumu ya kuishi, ikiwa ni pamoja na baridi kali, njaa, magonjwa nakadhalika -- yaliyotokana na jiografia ya nchi zao. Ilibidi watumie akili za ziada kuishi. Wakajikuta wanatoka 'nje ya box' hadi kufika kwetu. Kwa upande wetu huku Africa, Mungu alitupendelea sana kwa raslimali nyingi, hali ya hewa nzuri n.k. ikawa huhitaji kutumia akili nyingi sana 'kusavaivu' Afrika. Tukabweteka. Bahati mbaya sana tunaendelea kubweteka hadi leo.
 
Mzungu aliweza kufika huku kututeka kutokana na kwamba alikuwa na capital
Hapana, tende taratibu, wao walitoa wapi huo mtaji?

wazungu walimuitaji mtu mweusi kumfanya mtumwa kwenye mashamba ya Miwa nk lakini sisi tuliitajiana kufanyana misukule
Umejibu kitoto sana

Wazungu walikuwa na mfumo mzuri wa kiutawala
Hii inawezekana lakini sio kwa ukubwa huo

Uingereza ilikuwa chini ya utawala wa kifalme pamoja na nchi zingine za Ulaya
Ufaransa je? german kuwa na kingship leadership sio hoja
 
Infantry Soldier,

Kwani kumfanya mtu mwenzako mtumwa ni kitu kizuri?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio. Kumfanya mtu mwenzako mtumwa ni kitu kizuri kama kina maslahi mapana kwa taifa. It's the survival of the fittest.

Slavery was the necessary evil just like wars, na wazungu (ambao ndio wametuletea dini) walijua fika ya kuwa hili si suala jema lakini wakalazimika kulifanya kwa maana lilikuwa na maslahi makubwa kwa mataifa yao
 
Back
Top Bottom