Watumishi hewa 169 wagundulika mkoani Kigoma

Watumishi hewa 169 wagundulika mkoani Kigoma

njoo huku BUNDA kuna jamaa kamaliza IMTU 2014 anaitwa CHARLESS MKOMBE Kahonga 8m AKAPEWA DMO kamili ndani ya miezi 4, mwezi unaofuata kahonga tena KWA HR anayoitwa MAGESA tayari jamaa akapata barua ya kwenda kusoma MPH , sasa huyo nin kama sio mtumishi hewa

Ahsante kwa taarifa.
 
Funga wote watakaobainika kula hizo pesa za haramu.

Tena mrudi bandarini Dar. Huko ndiko kunaongoza watumishi hewa. Pengine huko kuna mtu anakula mshahara wa Dau hadi hii leo na toka ahamishwe huko ni miaka zaidi ya 15.
 
sasa hivi upinzani badala ya kuungana na jpm wao wameanza kutetea ujinga kama huu
watumishi 169 hewa kwa mkoa mmoja tena wa pembezoni je kwa jiji kama DAR na ARUSHA ambako wakuu wengi wa IDARA NI wapiga dili sijui hali ikoje mpaka sasa
Utengeneze mwenyewe watumishi hewa halafu uje kuomba msaada kwa jirani kumtoa?
 
Utengeneze mwenyewe watumishi hewa halafu uje kuomba msaada kwa jirani kumtoa?
Utengeneze mwenyewe watumishi hewa halafu uje kuomba msaada kwa jirani kumtoa?
Utengeneze mwenyewe watumishi hewa halafu uje kuomba msaada kwa jirani kumtoa?
Utengeneze mwenyewe watumishi hewa halafu uje kuomba msaada kwa jirani kumtoa?
Utengeneze mwenyewe watumishi hewa halafu uje kuomba msaada kwa jirani kumtoa?
haa haa huo ndo ukweli. msababishaji mkubwa wa watumishi hewa ni serikali yenyewe.....
 
Tatizo la mishahara hewa linaweza kupatiwa jibu kama kutakuwa na updates za employees from time to time.
Mwajiri yoyote atakadanganya afunguliwe mashitaka na afungwe kisha afirisiwe mali zake ili kufidia huo upotevu.
Hatua Kali za kinidhamu na uwajibikaji zitasaidia kukomesha hilo tatizo
 
sasa hivi upinzani badala ya kuungana na jpm wao wameanza kutetea ujinga kama huu
watumishi 169 hewa kwa mkoa mmoja tena wa pembezoni je kwa jiji kama DAR na ARUSHA ambako wakuu wengi wa IDARA NI wapiga dili sijui hali ikoje mpaka sasa
Mkuu hii ni nchi ya kidemokrasia!

Haiwezekani wananchi wote wakakubaliana na kile anachokifanya Rais Magufuli wakati wengine wanahitaji madhaifu yake na serikali yake kama mtaji wa kisiasa!

La muhimu ni kwa Rais Magufuli kuwatumikia wananchi wote kwa faida ya wananchi wote.

Wahenga walisema, tenda wema usisubiri shukrani!

Hizi ndizo siasa!
 
Wanachofanya wakuu wa idara ni kupachika majina hewa na kuyafungulia akaunti,wakati wa ajira mpya,hivyo serikali iwe makini.
 
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mjeda dadadeki lazima Heshima irudi na ukaidi uishe, uzuri wa Wajeda ni kwamba wao hufundishwa uaminifu na utii tu siku zote!

1.jpg


Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Emanuel Maganga amewataka wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote waliopo katika halmashauri zote kutaja kiasi cha fedha kilichotumika kuwalipa mishahara watumishi hewa 169 kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Akiongea na waandishi wa habari, Brigedia Jenerali Emanuel Maganga alisema kuwa agizo hilo ni kufuatia agizo la Mheshimwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli la kufanya uhakiki wa watumishi katika halmashauri zote ili kuwabaini watumishi hewa wanaolipwa mishahara kinyume na utaratibu za utumishi.
Alisema katika hao watumishi hewa 169 waliowabainika wapo ambao walishafukuzwa kazi, wapo ambao wameshafariki na wengine hawana sifa za kuwa watumishi wa umma.

Mhe. Maganga alisema kuwa suala la kuwa na wafanyakazi hewa ni wizi ambao hauwezi kuvumilika na wizi wa kuibia wanyonge hauwezi kuvumilika.
"Hakuna anayeweza kuvumilia wizi wa waziwazi kiasi hiki unaofanywa na baadhi ya watumishi wasiowaaminifu, wale wote watakaobainika wajiandae kwani hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao"Alisema Maganga.

Alisema kuwa fedha walizokuwa wakilipwa watumishi hao hewa kwaajili ya mishahara zinatakiwa kurudi zote, pia wakurugenzi wawafute watumishi hao hewa kwenye orodha ya malipo.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa sasa hivi katika serekali hii ya awamu ya tano hakuna kufanya kazi kwa mazoea.
Alizitaja halmashauri zenye watumishi hewa kuwa ni halmashauri ya kasulu watumishi 78,halmashauri ya Kigoma 23,Manispaa ya Kigoma Ujiji 29,halmashauri ya Buhigwe 11,Uvinza 19,kibondo 5,ofisi ya Mkuu wa Mkoa 4 na halmashauri ya Kakonko hakuna mtumishi hewa.
 
Tuliakikiwa pale Iramba mpaka tulichina maana singida ndo tulikuwa case study kumbe wapo wengi eeeh!! Sasa tunasubiri kuona hatatua sisisi zikichukuliwa ili kukomesha tabia za kipiga dili hela za umma
Haya matatizo yako nchini kote!

Kwenye ofisi za Halmashauri ndio majanga!
 
nitie nukta chache tu humu
1. watajwe hadharani waliohusika na wizi huu wa kinyaa (mfano mtu amekufa wewe unatumia nafasi ya wafu kujinufaisha)
2. wafikishwe mahakamani mara moja na media ziipe coverage ya kutosha ili iwe fundisho kwa wengine
3. hela walizokwiba zirudi mara moja hata kama ni kwa kuwafilishi

angalizo
1. Anti-Zitto hawachelewi kuja kuanza kumlaumu humu kisa hayo ni mkoa wa kigoma

mwisho.
namuona mrembo wetu (V) kwa mbali anauza sura!
 
Tunakoelekea kuna mtu atapigwa risasi ya kalio na mkuu wa mkoa. Mkuu si kasema mbona rwanda hamna majambazi na hivi ndivyo kagame anachofanya, ukimbishia kadogoo anakuwasha.
 
Back
Top Bottom