Watumishi hewa 169 wagundulika mkoani Kigoma

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Emanuel Maganga amewataka wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote waliopo katika halmashauri zote kutaja kiasi cha fedha kilichotumika kuwalipa mishahara watumishi hewa 169 kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Akiongea na waandishi wa habari, Brigedia Jenerali Emanuel Maganga alisema kuwa agizo hilo ni kufuatia agizo la Mheshimwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli la kufanya uhakiki wa watumishi katika halmashauri zote ili kuwabaini watumishi hewa wanaolipwa mishahara kinyume na utaratibu za utumishi.

Alisema katika hao watumishi hewa 169 waliowabainika wapo ambao walishafukuzwa kazi, wapo ambao wameshafariki na wengine hawana sifa za kuwa watumishi wa umma.

Mhe. Maganga alisema kuwa suala la kuwa na wafanyakazi hewa ni wizi ambao hauwezi kuvumilika na wizi wa kuibia wanyonge hauwezi kuvumilika.

"Hakuna anayeweza kuvumilia wizi wa waziwazi kiasi hiki unaofanywa na baadhi ya watumishi wasiowaaminifu, wale wote watakaobainika wajiandae kwani hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao"Alisema Maganga.

Alisema kuwa fedha walizokuwa wakilipwa watumishi hao hewa kwaajili ya mishahara zinatakiwa kurudi zote, pia wakurugenzi wawafute watumishi hao hewa kwenye orodha ya malipo.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa sasa hivi katika serekali hii ya awamu ya tano hakuna kufanya kazi kwa mazoea.

Alizitaja halmashauri zenye watumishi hewa kuwa ni halmashauri ya kasulu watumishi 78,halmashauri ya Kigoma 23,Manispaa ya Kigoma Ujiji 29,halmashauri ya Buhigwe 11,Uvinza 19,kibondo 5,ofisi ya Mkuu wa Mkoa 4 na halmashauri ya Kakonko hakuna mtumishi hewa.

Chanzo: Blog ya Jamii
 
Kwa mtaji huu haishangazi kuona nusu ya makusanyo kitaifa yanatumika kulipia mishahara ya watumishi wa serikali wakiwemo watumishi hewa.

Hata wale ambao sio watumishi hewa, kazi wanazozifanya zinakuwa sio value for money. Muda mwingi kwenye ofisi wanautumia kupiga soga na kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii.

Kinachosikitisha zaidi ni kuona mpaka kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa kulikuwa kuna watumishi hewa!

Hii nchi ina maajabu na vituko!

Kazi iliyoko mbele ya Rais Magufuli ni pevu. These are high pressure situations and he has to keep a cool, calm and collected head, otherwise he'll go nut.

Nchi hii ni majanga!
 
sasa hivi upinzani badala ya kuungana na jpm wao wameanza kutetea ujinga kama huu
watumishi 169 hewa kwa mkoa mmoja tena wa pembezoni je kwa jiji kama DAR na ARUSHA ambako wakuu wengi wa IDARA NI wapiga dili sijui hali ikoje mpaka sasa
 
Tuliakikiwa pale Iramba mpaka tulichina maana singida ndo tulikuwa case study kumbe wapo wengi eeeh!! Sasa tunasubiri kuona hatatua sisisi zikichukuliwa ili kukomesha tabia za kipiga dili hela za umma
 
Aiseee, kwa mtindo huo!

Watumishi hewa wanaweza fika 10,000, kila mwezi tunapoteza hospital 10! Tungekuwa mbali sana
 
sasa hivi upinzani badala ya kuungana na jpm wao wameanza kutetea ujinga kama huu
watumishi 169 hewa kwa mkoa mmoja tena wa pembezoni je kwa jiji kama DAR na ARUSHA ambako wakuu wengi wa IDARA NI wapiga dili sijui hali ikoje mpaka sasa
Mkuu jitihada ni njema sana, ila napata wasi wasi na hawa wasaidizi wa JPM ktk kufanikisha zoezi hili kama kweli wana nia ya dhati. Niki rudi nyuma kidogo, swala la watumishi hewa limekuwepo muda mrefu sana na limekuwa orchestrated hasa tangu Mwigulu alipo teuliwa kuwa naibu waziri wa fedha, tangia kipindi hicho uhakiki wa watumishi hewa umefanywa kwa kujirudia rudia ndani ya muda mfupi kutoka uhakiki mmoja hata mwingine. Mara zote wanapo hakiki hukuta watumishi hewa!!, tatizo ni nini??, au ni tatizo lisilo tatulika??,
 
Hayo ya watumishi hewa yalifanywa na serikali sikivu ya CCM .Kwa maana nyingine CCM inatumbua yenyewe majipu yake hayatuhusu sisi. Sisi tunafuatilia yanayofanyika nyuma ya pazia ambayo ni double standard!

QUOTE="TRUVADA, post: 15670426, member: 196104"]sasa hivi upinzani badala ya kuungana na jpm wao wameanza kutetea ujinga kama huu
watumishi 169 hewa kwa mkoa mmoja tena wa pembezoni je kwa jiji kama DAR na ARUSHA ambako wakuu wengi wa IDARA NI wapiga dili sijui hali ikoje mpaka sasa[/QUOTE]
 
Swali la kujiuliza ni kwamba hao watumishi mishahara yao inawafikia au inaishia kwa wakuu wa idara?
Wapiga hizo dili ni wengi na mikoa mingine ijitahidi kufanya hivyo kuokoa hizo hela
 
sasa hivi upinzani badala ya kuungana na jpm wao wameanza kutetea ujinga kama huu
watumishi 169 hewa kwa mkoa mmoja tena wa pembezoni je kwa jiji kama DAR na ARUSHA ambako wakuu wengi wa IDARA NI wapiga dili sijui hali ikoje mpaka sasa
Kwani Arusha siyo mkoa wa pembezoni mwa nchi? Fikiri vizuri
 
Kwa mtaji huu haishangazi kuona nusu ya makusanyo kitaifa yanatumika kulipia mishahara ya watumishi wa serikali wakiwemo watumishi hewa.

Hata wale ambao sio watumishi hewa, kazi wanazozifanya zinakuwa sio value for money. Muda mwingi kwenye ofisi wanautumia kupiga soga na kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii.

Kinachosikitisha zaidi ni kuona mpaka kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa kulikuwa kuna watumishi hewa!

Hii nchi ina maajabu na vituko!

Kazi iliyoko mbele ya Rais Magufuli ni pevu. These are high pressure situations and he has to keep a cool, calm and collected head, otherwise he'll go nut.

Nchi hii ni majanga!
Watumishi hewa wapo Ofisi zoote za umma Nchini ni vigumu kuwabaini Kwa sababu Yule aliyepewa jukumu la kuchunguza ni mmojawapo wa wale wanaoifaidi hiyo pesa ya Watumishi hewa hata wakiambiwa walete list lazima wataacha baadhi ili waendelee kutafuna pesa .
 
Kwa mtaji huu haishangazi kuona nusu ya makusanyo kitaifa yanatumika kulipia mishahara ya watumishi wa serikali wakiwemo watumishi hewa.

Hata wale ambao sio watumishi hewa, kazi wanazozifanya zinakuwa sio value for money. Muda mwingi kwenye ofisi wanautumia kupiga soga na kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii.

Kinachosikitisha zaidi ni kuona mpaka kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa kulikuwa kuna watumishi hewa!

Hii nchi ina maajabu na vituko!

Kazi iliyoko mbele ya Rais Magufuli ni pevu. These are high pressure situations and he has to keep a cool, calm and collected head, otherwise he'll go nut.

Nchi hii ni majanga!
Mbona hata wewe upo kwenye mitandao? Au ndio ile ajira alizowapa makamba na kikwete?
 
Back
Top Bottom