sasa hivi upinzani badala ya kuungana na jpm wao wameanza kutetea ujinga kama huu
watumishi 169 hewa kwa mkoa mmoja tena wa pembezoni je kwa jiji kama DAR na ARUSHA ambako wakuu wengi wa IDARA NI wapiga dili sijui hali ikoje mpaka sasa
Punguza "ashkmajinoon" au kama vipi wahi Mombasa ukatulizwe,upinzani umeingiaje katika hii hoja iliyoletwa na MSEMAJI UKWELI?Upinzani ndiyo waliotoa ajira za hao watumishi hewa?
Hili si jukwaa linaloendeshwa kipropaganda,kama baadhi ya hoja ziletwazo hapa zinakuzidi kimo,chukua kistuli upande ili uweze kuzisoma vema na kuzielewa kabla ya kuchafua hali ya hewa hapa jukwaani.
Hoja iliyoletwa jukwaani ni watumishi hewa ambao wametapakaa katika sekta na Taasisi zote za Umma.Magufuli alipotembelea BOT nako alikutana na tatizo hili la watumishi hewa,je kwa nakisi yako ya ubongo usioweza kujaa hata kisoda,watumishi hao waliajiriwa na Mh.Mbowe?
Yawezekana huwa inafikia mahali hadi ccm inashangaa aina ya watu iliyonao,ukereketwa wa aina yako hauna tija hata kwa chama chako.Msaada pekee anaoweza kupewa Magufuli ni kuambiwa Ukweli kama Msemaji Ukweli alivyohoji kuwa imekuwaje hadi ofisi ya mkuu wa mkoa nayo iwe na watumishi hewa?
Visaidieni vyama vyenu kwa kuviambia Ukweli na si kwakuzifanyia propaganda kila hoja zenye mwelekeo wa kulikomboa Taifa.
Tatizo la watumishi hewa katika Halmashauri nyingi linaweza kuwa ni Tatizo la kimfumo,ikumbukwe hapo awali taarifa zote za watumishi zilikuwa zinatunzwa na Masijala.Mfumo huu wa kutumia mafaili mara nyingi huwa unakuwa mgumu kufuatilia jina la mtumishi aliyepoteza sifa za kuendelea kuwemo kwenye mafaili ya Masijala zetu.
Suruhisho la hili ni kuzipatia Halmashauri zetu wataalamu wa teknolojia ili taarifa zote za watumishi wake ziwekwe kwenye database,badala ya kuendelea kutumia mafaili ambayo huchelewesha zoezi la ufuatiliaji wa taarifa na kumbukumbu za watumishi wa idara zetu.