Watumishi Chato watakiwa kujieleza kwa kutohudhuria sherehe za mazingira

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,876
Watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Chato wameagizwa kuandika barua ya kujieleza sababu za kutoshiriki maadhimisho ya siku ya mazingira duniani.

UTUALIZASS.jpg

Maadhimisho hayo mkoani Geita yalifanyika wilayani Chato na kupelekea shughuli hiyo kuhudhuriwa na watu wachache, ukilinganisha na maandalizi yaliyofanyika.

Maagizo hayo yametolewa na kaimu mkuu wa mkoa wa Geita Saidi Nkumba wakati wa hafla iliyofanyika shule ya sekondari Chato baada ya kuona maudhurio machache.

Chanzo: EATV
 
Hiv mbona inatumika nguvu kubwa sana kuifanya chato ionekane kuwa ni special place kumbe ni mji wa kawaida tu
Sio mji wa kawaida ndugu yangu..chato ndiko alikozaliwa rais wa awamu ya tano.. Chuma JPM..Mungu amlaze mahali pema peponi...
Lazima chato iwe special kwasababu imemtoa amiri jeshi mkuu..kupata hii bahati si mchezo ndugu yangu..
 
Sio mji wa kawaida ndugu yangu..chato ndiko alikozaliwa rais wa awamu ya tano.. Chuma JPM..Mungu amlaze mahali pema peponi...
Lazima chato iwe special kwasababu imemtoa amiri jeshi mkuu..kupata hii bahati si mchezo ndugu yangu..
kama ni hivyo butiama nako wafanye hivyo hivyo, kule alipotoka mkapa nako wafanye hivyo hivyo, kwa kina mwinyi nako wafanue hivyo hivyo.. kwa jk napo qafanye hivyo hivyo.
 
Ndio hivyo..hiyo Ni miji muhimu Sana kwa historia ya nchi yetu
nothing special. Ndio maana Mwalimu J.K Nyerere aliishi maish decent even after madaraka. angeweza kuifanya butiama very special place.. why hakufanya?
B.Mkapa?
Mwinyi?

Miji inayoingiza mapato makubqa nchini, miji inayochangia pato la taifa kwa asilimia kubwa, miji yenye mizunguko mikubwa ni special status.

hiyo mingine ibaki ya kuhistoria tu. lakin kama haina vigezo vikubwa kama miji mikubwa nchini basi hamna kitu.
 
Zile taa za kuongozea magari huwa zinaongoza;
Magari,
Ng'ombe,
Baiskeli,
Ndege,
Walevi,
Wanafunzi
 
Back
Top Bottom