Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,728
- 2,259
Kundi la watu 11 wanaosadikiwa kupanga na kutekeleza maujai ya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rungwe na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Ndg. John Mwankenja wamekamatwa.
Kwa mujibu wa habari za Radio One mchana wa leo , bunduki , risasi 30 zlizosalia, face mask na kofia iliyotumika katika mauaji hayo vile vile vimepatikana.
Katika kundi hili inaaminika wamo wanasiasa waliopanga mauaji hayo na majambazi waliotekeleza.
Kuna jina la muuaji linalojitokeza kutoka Kiwira lakini linahifadhiwa mpaka litakapotolewa rasmi na Polisi.
Mimi binafsi nawapongeza Polisi na Idara zote za Usalama kwa kuitikia kilio kile cha pale kanisani Kiwira Moravian Church, kilio kilichokuwa na simanzi kubwa, kwa wote waliokuwepo.
Pamoja na mafanikio ya Polisi Mkoani Mbeya Wananchi vile vile walijitolea sana katika kupatikana kwa wauaji hawa-moja ya mafanikio ya Polisi Jamii.