Watuhumiwa mauaji ya John Mwankeja wakamatwa!

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Nov 5, 2008
4,726
2,255
Kundi la watu 11 wanaosadikiwa kupanga na kutekeleza maujai ya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rungwe na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Ndg. John Mwankenja wamekamatwa.
Kwa mujibu wa habari za Radio One mchana wa leo , bunduki , risasi 30 zlizosalia, face mask na kofia iliyotumika katika mauaji hayo vile vile vimepatikana.
Katika kundi hili inaaminika wamo wanasiasa waliopanga mauaji hayo na majambazi waliotekeleza.
Kuna jina la muuaji linalojitokeza kutoka Kiwira lakini linahifadhiwa mpaka litakapotolewa rasmi na Polisi.
Mimi binafsi nawapongeza Polisi na Idara zote za Usalama kwa kuitikia kilio kile cha pale kanisani Kiwira Moravian Church, kilio kilichokuwa na simanzi kubwa, kwa wote waliokuwepo.
Pamoja na mafanikio ya Polisi Mkoani Mbeya Wananchi vile vile walijitolea sana katika kupatikana kwa wauaji hawa-moja ya mafanikio ya Polisi Jamii.
 
hongera Polisi Tanzania
 
Pamoja na kulipongeza, hawa jamaa wanatakiwa waende 1 step ahead kwa kusikia maandalizi ya mauaji kabla ya tukio. Pamoja na kuwa tunawapongeza bado uhai wa ndugu Mwankenja umetoweka kikatili kabisa.
 
Hongera...lakini nachelea kutoa hongera wakati wauaji wa prof Jwani Mwaikusa wanakunywa gahwa na kupanga mauaji mengine

Wauaji wa wakazi wa mbezi ambao chanzo cha vifo ni 'ushindani wa kibiashara' japo wanajulikana wanapeta kama kawaida

Wauaji wa countless innocent victims wako hai na wanaendeleza mauaji mengine bila shaka yoyote, mh kikwete ulipochukua nchi miezi ya mwanzo ulipambana sana na majambazi, mbona sasa hivi Mbezi Kimara, Mbezi Beach watu wanaishi roho mkononi ???

Kwa mbinu mliyotumia kwa mauaji ya Mbeya endelezeni uzi huohuo nchi nzima...wananchi mpaka tunataka kuwa wakimbizi nchini
 
Inasemekana marehemu alikuwa ameweka maslahi ya taifa mbele juu ya Mashamba ya chai na mwekezaji wa kihindi.Wenye taarifa kamili watupe
 
Mkuu sina uhakika na hili lakini wengi pale msibani waliwalaumu sana wanasiasa uchwara pale Kiwira kwa kupanga mauaji haya.Sababu zilizojitokeza sina uhakika vile vile, lakini wivu wa kupindukia kwa Nd.John Mwankenja ambaye alikuwa akipendwa sana na wananchi,imeonekana kuwa sababu kubwa ya kuchochea wivu huo.
Ndg J Mwankenja alikuwa mkulima wa kawaida na wengi walimsifu kwa upole na ukimya wake-hata hivyo sababu hizi hazikuwazuia wauaji wake.
 
Mimi nilivyo sikia alikuwa anafuatilia kesi ya albino aliye uwawa,na alikuwa na ushahidi mzuri.
Lets wait and see.
 
Kundi la watu 11 wanaosadikiwa kupanga na kutekeleza maujai ya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rungwe na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Ndg. John Mwankenja wamekamatwa.
Kwa mujibu wa habari za Radio One mchana wa leo , bunduki , risasi 30 zlizosalia, face mask na kofia iliyotumika katika mauaji hayo vile vile vimepatikana.
Katika kundi hili inaaminika wamo wanasiasa waliopanga mauaji hayo na majambazi waliotekeleza.
Kuna jina la muuaji linalojitokeza kutoka Kiwira lakini linahifadhiwa mpaka litakapotolewa rasmi na Polisi.
Mimi binafsi nawapongeza Polisi na Idara zote za Usalama kwa kuitikia kilio kile cha pale kanisani Kiwira Moravian Church, kilio kilichokuwa na simanzi kubwa, kwa wote waliokuwepo.
Pamoja na mafanikio ya Polisi Mkoani Mbeya Wananchi vile vile walijitolea sana katika kupatikana kwa wauaji hawa-moja ya mafanikio ya Polisi Jamii.

UPUUZ MTUPU!!!! MwanaCCM mmoja kuuwawa Rais alikimbilia wakamatwe haraka!! vip wale mamia waliouwawa Tarime miaka yote hiyo, na wa Arusha JE?? au sababi sio wanaCCM,wanakuwa sio binadamu!! Polis na ****** walikuwa wapi?? SHIT!!!!!

SIPONGEZI HUUU NI UPUUZI NA UNAFIKI MKUBWA!!!
 
Mimi nilivyo sikia alikuwa anafuatilia kesi ya albino aliye uwawa,na alikuwa na ushahidi mzuri.
Lets wait and see.
Ni kweli kabisa mkuu, huyu jamaa alikuwa mtu wa watu na hizo habari zilikuwepo pale msibani, kuwa alikuwa akijitolea sana kwa masuala ya watu wake wilayani.
Inasemekana kati ya walioua albino wengine walikuwa bado kukamatwa.
 
Hata Zombe alipongezwa baada ya kuua wafanyabiashara wasio na hatia ya kustahili kifo. Ni mapema sana kutoa pongezi kwa polisi hawa wanaofanya kazi kama marobot!
 
UPUUZ MTUPU!!!! MwanaCCM mmoja kuuwawa Rais alikimbilia wakamatwe haraka!! vip wale mamia waliouwawa Tarime miaka yote hiyo, na wa Arusha JE?? au sababi sio wanaCCM,wanakuwa sio binadamu!! Polis na ****** walikuwa wapi?? SHIT!!!!!

SIPONGEZI HUUU NI UPUUZI NA UNAFIKI MKUBWA!!!

Mkuu dont panic nchi inaendeshwa kwa ushirikiano na serikali , na kukamatwa kwa watuhumiwa ni baada ya serikali kutoa wito wa kuomba habari zozote zinazohusiana na tukio hili kutoka kwa wananchi.
Wananchi waliitikia , tena kwa wingi sana.
Vinginevyo ukitaka kupambana na Polisi basi hapo mi sipo!
Kwa taarifa yako kati ya wanao tuhumiwa katika mauaji ya J Mwankenja ni wanaCCM wa eneo lake.
Cool down and think positively even in the worst of scenarios.
 
Wawapeleke kwenye vyombo vya sheria maana hukawii kusikia wamewaua kwa majibizano ya risasi kana kwamba polisi ana ruhusa ya kuua raia
 
Hakuna lolote (rip) mwa lakini polisi hawana lolote wanabebana tuuu,wameua watu hovyo na bila haya wala soni! Wanabambikia watu kesi a.hivi zombe si aliua af tkamwona mitaani?wanapindisha sheria hawa!, siungi mkono hoja
 
Wawapeleke kwenye vyombo vya sheria maana hukawii kusikia wamewaua kwa majibizano ya risasi kana kwamba polisi ana ruhusa ya kuua raia
Demokrasia ni nzuri sana maana ina upande wa pili wenye hoja nzito tu!
 
Vipi polisi jamii? Inafunction baada ya mauaji? Intelijensia iko wapi?
We all wish ingekuwa hivyo kwa huyu mwezetu J Mwankenja, na wengine wengi wanaopoteza maisha katika hali kama hii.
Cha muhimu si kuwa antagonistic na wanausalama wetu lakini kutoa taarifa za kupre-empt matukio kama haya.
 
Mkuu dont panic nchi inaendeshwa kwa ushirikiano na serikali , na kukamatwa kwa watuhumiwa ni baada ya serikali kutoa wito wa kuomba habari zozote zinazohusiana na tukio hili kutoka kwa wananchi.
Wananchi waliitikia , tena kwa wingi sana.
Vinginevyo ukitaka kupambana na Polisi basi hapo mi sipo!
Kwa taarifa yako kati ya wanao tuhumiwa katika mauaji ya J Mwankenja ni wanaCCM wa eneo lake.
Cool down and think positively even in the worst of scenarios.

Mkuu heshima mbele,

Unachosema ni sahihi kabisa.Ila tatizo la Serikali ya CCM hua inareact postively kwenye mambo ya CCM.Ebu fikiria wanachi waliouwawa Tabora,Tarime,Arusha,Mbarali lakini rais hakusikika akitoa amri kali.Fikiria mauji ya prof.Mwaikusa.Kuna mapungufu makubwa sana katika utendaji wa jeshi la polisi kwangu nachelea kuwapa pongezi naona wametimiza wajibu wao.

RIP Mwankenja sababu namfahamu amenipa support kubwa katika majukumu yangu ya kila siku wakati nafanya kazi Tukuyu,alikuwa mpole,mtu asie na papara.
 
TOPIKI INGEKUWA: WATU KUMI NA MOJA WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA MAUWAJI YA MWA. Ingetosha...
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom