Watuhumiwa mauaji ya John Mwankeja wakamatwa!

Hongera sana polisi msisahau kuwakamata walowapiga risasi na kuwaua raia Arusha na Nyamongo risasi toka nyuma!
 
Ccm ndo wanachochea mauaji ya kisiasa bila kujua, wameruhusu rushwa kubwa katika uchaguzi, as a result wale waliotoa rushwa kubwa wakabwagwa na wanachi sasa wanawaua wale ambao hawakutoa pesa lakini vipenzi wa wananchi, kwa kuwa waliteketeza mitaji yao na uongozi hawakuupata na namna ya kurudisha mitaji hiyo ni ngumu. Mgombea diwani wa ccm kule mbezi luis eneo la mshikamano yeye aliuza gari, viwanja vya urithi akabwagwa na chadema, sasa akimwona yule diwani wa cdm mwili unasisimka kwa jinsi alivyolowea kwenye ulofa
 
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumewezekana kutokana na ushirikiano mkubwa uliotolewa na wananchi. Wananchi wa Kiwira walionyesha hasira yao ya wazi dhidi ya kila aliyehusika mauaji hayo, na kuanzia usiku ule ule ilipofahamika walianza kutoa ushirikiano kwa kuwataja kila waliyemshuku.

Muaji alifahamika muda mfupi, lilikuwa jukumu la polisi kumtafuta kwa sababu walielezwa hata mienendo yake na inasemekana ana biashara Tunduma na Uyole.

Iwapo polisi wasingemkamata ndipo wangewajua watu wa Mwankenja aka Kiwira ni nani, hasira yao ingeishia kwao. Hata unapongea na RPC unaiona hofu yao iwapo wasingewakamata, walitafuniwa kila kitu.
 
Kila kitu Tanzania kinawezekana ila hakuna uwajibikaji. Kama JK hasingesisitiza kukamatwa kwa hao watu, basi ingekuwa ni porojo tu. Nashindwa kuelewa ni kwa nini JK huyo huyo hasitoe huo huo mkazo kwa kukamatwa kwa wale waliofanya mauaji Tarime?
 
Ni kweli kabisa mkuu, huyu jamaa alikuwa mtu wa watu na hizo habari zilikuwepo pale msibani, kuwa alikuwa akijitolea sana kwa masuala ya watu wake wilayani.
Inasemekana kati ya walioua albino wengine walikuwa bado kukamatwa.
kama ishu ni albino,viongozi wa kisiasa wameingiaje,hasa yule mbunge mtarajiwa?
 
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumewezekana kutokana na ushirikiano mkubwa uliotolewa na wananchi. Wananchi wa Kiwira walionyesha hasira yao ya wazi dhidi ya kila aliyehusika mauaji hayo, na kuanzia usiku ule ule ilipofahamika walianza kutoa ushirikiano kwa kuwataja kila waliyemshuku.

Muaji alifahamika muda mfupi, lilikuwa jukumu la polisi kumtafuta kwa sababu walielezwa hata mienendo yake na inasemekana ana biashara Tunduma na Uyole.

Iwapo polisi wasingemkamata ndipo wangewajua watu wa Mwankenja aka Kiwira ni nani, hasira yao ingeishia kwao. Hata unapongea na RPC unaiona hofu yao iwapo wasingewakamata, walitafuniwa kila kitu.

Nakubaliana wewe Mkuu Nsesi.
Kwa emotions zilizokuwepo pale Kiwira(mji uliokuwa unaitwa Mwankenja miaka ya nyuma),emotions kali zilizochanganyika na hasira, serikali pamoja na kuona machungu ya wananchi imelishughulikia kwa kasi kubwa.
Kwa waliokuwepo pale Moravian Church "high table" iligubikwa na mchozi kwa yeyote aliyekuwepo wakati wanakwaya wanamlilia Mungu kwa mauaji haya.
Viongozi wote waliokuwepo waliahidi kuwa hawa maharamia wangekamatwa tu,iwe iweje.
Kilichowasononesha na kuwakasirisha watu wengi ni kuwa mauaji yalikuwa ya kinyama sana kwa mtu ambaye basically alikuwa honest and upright.
Zaidi ya yote huyu mtu alikuwa mkulima wa kawaida.
 
Nachelea kuwapongeza polisi ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza mauaji ya watu wasio na hatia kama John Mwankeja, kule tarime wameua watu 7 wauaji hawajakamatwa, tabora wameua 1 hawajakamatwa ni wapongeze kwa lipi wakati nao ni wauaji?
 
Inasemekana marehemu alikuwa ameweka maslahi ya taifa mbele juu ya Mashamba ya chai na mwekezaji wa kihindi.Wenye taarifa kamili watupe[/QU

inawezekana mauaji yaliyotokana na tamaa mbaya!kama ni kkweli nafikiri ni njia nzuri ya kurekebishana
 
Tunafarijika na hatua iliyofikiwa, wakimaliza hapo polisi wahamie Tarime, kule nako waliuliwa watu na hakuna aliyekamatwa hadi hii leo.
 
Angekuwa si kiongozi wa ccm hakuna ambacho kingefanyika.
Vp kesi ya tarime?
Vp Imran Kombe?
SIWAPONGEZI.
 
Mkuu dont panic nchi inaendeshwa kwa ushirikiano na serikali , na kukamatwa kwa watuhumiwa ni baada ya serikali kutoa wito wa kuomba habari zozote zinazohusiana na tukio hili kutoka kwa wananchi.
Wananchi waliitikia , tena kwa wingi sana.
Vinginevyo ukitaka kupambana na Polisi basi hapo mi sipo!
Kwa taarifa yako kati ya wanao tuhumiwa katika mauaji ya J Mwankenja ni wanaCCM wa eneo lake.
Cool down and think positively even in the worst of scenarios.

Haya mambo yanaumiza sana: watu watano wasio na hatia wanauwawa kule Tarime na mpaka sasa police waliotekeleza mauaji yale wako huru. Anauwawa mwanasiasa mwema kipenzi cha wengi wanakamatwa watu 11 wakituhumiwa kwa mauaji hayo. Polisi anaua raia asiye na hatia kwa makusudi kabisa lkn yeye si jambazi? mwingine anmuua mtu mwema asiye na hatia na huyu ndo jamabzi?. Kwangu mimi wote ni majambazi!
 
Inawezekana wamekamatwa watu kwa kosa la mauaji lakini si wenyewe. Polisi wa bongo wao ukamata kila mtu wanayekisia na kutoa taarifa vyombo vya habari kwamba wamekamata wauajina kesho utawaona mjini wakizurura. Hakuna ushahidi......Nyie subirini mtaniambia.......
 
kama ishu ni albino,viongozi wa kisiasa wameingiaje,hasa yule mbunge mtarajiwa?

Mkuu Kijallo, this is the One million dollar question.
Inabidi Polisi wa connect the dots, lakini kutokana na taarifa zilizo zagaa pale kijijini ni kwamba hawa wanasiasa kwa muda mrefu wamekuwa wakimuonea wivu na kumtukana wazi wazi Nd Mwankenja.
Connection ya majambazi na wanasiasa hawa ndio link itakayosaidia kutafuta motive.
Lakini kama mdau mmoja hapo juu alivyo comment Nd Mwankenja alikuwa anafuatilia majambazi walioua albino katika kata yake!
Na inasemekana wauaji wake ni kati ya walioua albino.
 
kama ishu ni albino,viongozi wa kisiasa wameingiaje,hasa yule mbunge mtarajiwa?

Inaelekea mauaji ya Mwankenja yanahusisha siasa za maji taka za chama cha magamba ndio maana kuna wengine kati ya hao watuhumiwa wanaitwa wabunge watarajiwa!! Kama hivyo ndivyo basi wanasiasa wa huko Rungwe lazima mkae na mtathmini jinsi mnavyoendesha siasa zenu na kama kweli kuchaguliwa kwenu kunaonesha mapenzi ya wananchi na si kuchaguliwa kwa ujanja ujanja wa kutumia pesa; msipofanya tathmini ya siasa zenu mnaweza kupukutishana kama majani na dalili ndio hizo!!
 
Polisi na Waliomwua John Mwankenja ni wale wale. Mara ngapi polisi wameuwa huko Mbeya? Mmesahau ya kesi ya kina Zombe? Mmesahau huko Nyamungo ambako zaidi ya watu 70 wameuwa na polisi tangu 2006?
 
Back
Top Bottom