Mkuu Incredible, nikukumbushe masikitiko juu ya kisa cha mtindo huu, kwanza nikusahihishe kuwa vijana hawa wameiba pochi hawajaiba bali wamepora kwa kukwapua. Huyu dada alikuwa akitembea kando ya barabara kisha wakatokea hao majambazi wakiwa ktk pikipiki boxer wakakwapua mkoba na kukimbia. Style hii iliwahi kumkumba raia wa nchi za Scandnavia akiwa kabeba pack yale mabegi ya watalii eneo la Upanga, barabara ya Umoja wa Mataifa, kwa kuwa lile pack alikuwa amejifunga nalo mwilini yule jambazi alipokwapua halikumtoka mwilini yule mzungu na jambazi hakuliachia, pikipiki ikiwa kwenye mwendo mkali, yule dada aliburuzwa kuanzia S/M Muhimbili hadi maeneo ya Fire, Morogoro Road, alikuwa amefariki huku akiwa ameburuzwa baadhi ya sehemu ya mwili wake mifupa ikiwa nje. Nadhani umepata picha fulani ambayo hata dada huyu wa Tabata angeweza kukumbana nayo ikiwa tu hangeachia mkoba wake. Binafsi nimefurahi kuwa yaliyowakuta maana idadi ya majambazi imepungua.