so sad vidagaa vinachomwa moto Mapapa wanaachwa
Ajabu kweli watu mnashabikia tukio hili? Ni hukumu gani mtu akiiba achomwe moto? Mbona tunachukua majumu mazito?
Acha tu wizi, utarudi salamaduh!dunia ya sasa ukitoka na kurudi nyumbani salama ni kushkuru mungu.
Safi sheria imechukua mkondo wake.
haya bana mkuu kwa hiyo mie mwizi.ila namaanisha hv,hata we unaweza kutoka kwako salama ila ukikutana nao tu anza kusali mana watakuchukulia ulicho nacho na kukuua juu.mie mwenyewe cku hz nikipishana na bodaboda yenye wanaume wawili kiukweli nachanganyikiwa kwa uogaAcha tu wizi, utarudi salama
Hao hao wakiachwa kesho wanakomaa na kuibuka na mbinu mpya, baba wa watu wamemtoa roho mlimani city pale, yanauma ngoja yakukute tu ndio utajua jinsi gani yanavyouma. Ni haki yao kufa kwa kuwa wamepitiliza kwenye ubinadamu hawapo tena.
Nasikia ni mwanamke na mwanaume sasa huyo mwanamke ni kawaida yake kukodi pikipiki na kupeleka ilipo timu ya wezo ni kundi lipo mahali dada akishafika wenzie wanapora wanakimbia kumbe jamaa wamemjua dada wamemuwekea mtego na jana ikawa mwisho wake .RIP wezi.
ngoja tuone ikiwafikia hao vigogo nao maana ni miaka mingi tumekuwa tukisubiria......
Nimesoma kwenye Michuzi blog ya leo tarehe 24 August, 2014 kwamba vijana wawili wameuawa kwa kuchomwa moto kule Tabata Liwiti. Kisa cha vijana kuuawa ni baada ya kuiba pochi ya mwanamke mmoja.
Nimesikitika sana kuona jinsi wananchi walivyochoshwa na utendajikazi wa jeshi la polisi kiasi kwamba wanajichukilia sheria mikononi.
Wizi wa pochi unakatisha uhai wa mwanadamu.
Itafika mahala hata viongozi wa serikali ambao wanaiba mali ya umma nao watakuja fanyiwa haya haya. Kwasasa wanadhani haya yataishia huku uswazi na ndo maana hawachukui hatua za kuboresha jeshi la polisi.
Itafika muda wezi wakubwa watatendewa hivi hivi. Tunao wezi kama vile
- Vibali vya kuua tembo
-Twiga waliopelekwa Qatar na ndege ya kijeshi
-Pesa za rada
-Epa
-Kagoda
ngoja tuone ikiwafikia hao vigogo nao maana ni miaka mingi tumekuwa tukisubiria......