Ufalme wa Mwizi na hatma yake

Mvumbo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
3,444
11,942
Salaam

Leo nimekumbuka kisa cha ndugu yetu mwizi (kaka yangu mtoto wa mama mdogo) ambae alikuwa ameiva kwenye wizi hasa wa kutumia uchawi na mbinu kali za kitapeli.

Nyakati hizo nilikuwa naishi karibu kabisa na nyumba ya familia ya Babu mzaa mama, na mama yangu pamoja na ndugu zake walikuwa wanaishi hapo kwa baba yao.

Huyu kaka yangu alikuwa hajulikani anapoishi ila akiharibu anakuja hapo kwa mama zake kujificha mpaka mambo yatulie, ni mara nyingi amefungwa na kuachiwa, kupigwa na kuja hoi pale nyumbani na wahuni wenzake ambao walimuuguza kwa mitishamba na kumchua kwa majani ya mnyono mpaka atakapopona kwani waliogopa kwenda hospital.

Kuna siku nilifika pale nyumbani nikawakuta na wenzake kama sita hivi juu ya meza wamewasha mshumaa wanatumia madawa ya kulevya, baada ya salamu wakasema dah! Tuna majonzi sana, tumekwenda kuchukua mali mahali ila msala jamaa zetu watatu wale ambao tuliwahi kuja nao hapa...imekuwa bahati mbaya wamechomwa moto!

Jamaa wakisema hivyo huku wanapata vitu vyao kama hakujatokea kitu na wakipumzika siku mbili ujue wanaingia kazini tena.

Mimi binafsi nilishamkuta kwenye pikipiki yangu kubwa akiikata waya ili aiibe, na pia kuna siku niliingia nyumbani kwangu ile kuangalia Tv nikapitiwa na usingizi ilikuwa kama tano usiku, kushtuka nakuta jamaa kabeba deki na mwenzake king'amuzi! Hapo wakaanza kuzuga na kuniambia "hapa una connect vipi mdogo wangu tucheck movie?" Mpango wao ukafa.

Huyu jamaa hakuna aliyempenda wala kumtaka aje pale nyumbani ila hakuna wa kumfukuza maana pale panamuhusu ni kwa babu yake pia na mama yake mzazi yupo pale na babu ameshafariki.

Mimi ki upande wangu ilikuwa ni mdogo kwake na amenizidi sana umri, aliniheshimu na niliheshimika pia kulingana na kazi yangu kwenye jamii, hivyo niliposikia au kumuona amekuja pale nilikuwa siendi haswa baada ya kushamiri matendo yake ya ajabu.

Muda wote ana panga kiunoni au sime, ni jitu limepanda na genge lake lote katika wezi wa mji walimuita master maana hata wakiishiwa mipango, jamaa akiingia yeye basi ujue hela ndefu inapatikana muda mfupi kiasi cha kuzunguka tu na kumwambia mtu una matatizo na akitema mate ni nywele, na kuchukua vitu vyake vyote kwa hiyari kabisa.

Siku moja nilikwenda kwa mama pale na ndugu zangu tumekaa tunasubiria tuuone mwaka mpya na kipindi hicho jamaa hajaonekana zaidi ya miezi sita na tukajua yuko jela, kwani alikuwa akishikwa hamwambii mtu, kesi anafuatilia peke yake mpaka anafungwa na akitoka halaumu mtu wala hana nongwa na ndugu.
Basi ile tumekaa nje kama saa sita kasoro ghafla jamaa akaletwa na Defender na Askari kama nane wakiwa na bunduki, mabomu na marungu na kuambiwa aingie ndani aonyeshe mzigo alioiba jana yake katika duka walilovunja! Ghafla pale pale kuna jamaa mwenye kitambi nilikuja kugundua ndiye mwenye duka, akaropoka "hawa wawili pia walikuwepo tena walikuwa wananirushia mawe!"

Hapo akimaanisha mimi na ndugu yangu wa kiume ambae alikuja likizo!

"Simama juu" ilikuwa ni amri ya Afande mmoja wapo na tukachukuliwa moja kwa moja mpaka kituoni saba usiku.

Nikamtonya Askari mmoja wapo kuwa sisi hatuhusiki na mimi ni mtu na shughuli zangu za maana na dogo ni mwanafunzi, akasema ile ni oda hivyo ameikamilisha nisubiri wakuu niwaeleze asubuhi.

Mle ndani hewa ilikuwa nzito, chumba kidogo na kidirisha kipo juu sana na kidogo mno, nilijawa na mawazo na kufikiria najitoaje pale katika jambo zito kama hilo, na muda huo huo naisikia Radio Call toka kwa Afande inasema, ile kesi ya ujambazi wa kuvunja duka, tumekamata majambazi watatu bado wanne ovaaa!!!

Muda wote Bro kalala chini kwenye sakafu yenye mikojo bila wasi wasi wowote, akisema, mkiulizwa acheni kubisha bisha mambo yatachelewa, semeni tumechukua mzigo ili tukapumzike miezi sita tutarudi uraiani.

Inafika saa nani usiku akaletwa jamaa ambae kamtorosha binti wa Traffic, jamaa alipigwa sana mpaka akatupaka damu mle ndani na kutuaga kuwa anakufa...
 
Mambo ya nusu nusu hatutaki
 
Back
Top Bottom