Watu wanaiongelea ndege ya B-2 “Spirit” ya US inavyofanya mashambulizi huko Iran, unajua ina balaa gani?

Watu wanaiongelea ndege ya B-2 “Spirit” ya US inavyofanya mashambulizi huko Iran, unajua ina balaa gani?

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
31,139
Reaction score
88,800
Sio mara ya kwanza hivi karibuni umeona sehemu mbalimbali kwamba Marekani kutumia B-2 Spirit Stealth Bomber kufanya mashambulizi ya “precision” dhidi ya Iran. Lakini je, tunafahamu B-2 ni nini? Inaweza kufanya nini? Ina gharama kiasi gani? Na je, kama taifa kama Tanzania, tunaweza hata kuifikiria?
IMG_0695.jpeg

Historia Fupi ya B-Series Bombers
Marekani imekuwa ikitengeneza ndege za kubeba mabomu tokea kitambo sana. Hizo chuma wamekua wakiziita kwa herufi B ikimaanisha Bomber.

Baadhi ya izo ndude ni pamoja na:

B-17 Flying Fortress – Zilizotumika vita vya Dunia vya Pili, kwa sasa zipo retired.
IMG_0688.jpeg

B-52 Stratofortress – Hizi chuma zipo hadi leo, na zina uwezo wa kubeba mabomu ya nyuklia, hii sifa kuu ni destruction ila stealth capability ndogo.
IMG_0689.jpeg

B-1B Lancer – Hizi ni za supersonic, inasafirisha bombs kwa speed kubwa sana.
IMG_0690.jpeg

B-2 Spirit – Stealth bomber hizi ndio topic kuu ya leo, sifa kuu ni kutoonekana kirahisi na radar.
IMG_0691.jpeg

B-21 Raider – Ndege mpya ya stealth, bado ipo kwenye majaribio kwahiyo ni more advanced kuliko B-2.
IMG_0692.jpeg


Turudi kwenye topic:
IMG_0699.jpeg

B-2 Spirit ndiyo iliyovunja rekodi kwa teknolojia ya “stealth” iliyopelekea uwezo wa kuingia anga la adui bila kugundulika na radars.

Sifa Kuu za B-2 Spirit:

Size: Upana karibia mita 52, urefu mita 22 na kimo mita 5.
IMG_0698.png


Crew members: Wawili tu (2), Rubani na mission commander.
IMG_0703.jpeg

Maximum Speed: Inaenda hadi 1,010 km/h

Umbali bila kuongeza mafuta: Approx 11,000 km pia ikiishiwa mafuta inafanyiwa in-air refueling kwa kutumia ndege kama KC-135 au KC-10, na hivyo kuongeza range hadi zaidi ya 19,000 km.
IMG_0693.jpeg

Combat Radius: Approx 5,000 km

Mzigo wa mabomu inayoweza kubeba: Approx 18,000 kg (inaweza kubeba mabomu ya kawaida au ya nyuklia)
IMG_0694.jpeg


Taking Off Distance: Approx 2,400 m

Landing Distance: ~1,800 m

(Ndio maana izi haziwezi kutua katika Aircraft carriers kama Jets nyingine).
IMG_0696.jpeg


Bei ya B-2 Spirit ni habari nyingine:
Ingawa haziuzwi, ni mali ya USAF ila bei ya kutengeneza moja: $2.1 bilioni, ni sawa na zaidi ya TSh 5.4 trilioni

(Mara 2+ ya bajeti ya Wizara ya Ulinzi ya Tanzania 2024/25: TSh 2.4 trilioni ($960 milioni))

Hao US wenyewe wametengeneza jumla 21 tu, moja ilianguka 2008 mara tu baada ya kutakeoff (watu wa utabiri wa hali ya hewa walizingua).

IMG_0700.jpeg
moja ipo kwaajili ya training na 19 zipo mzigoni standby.
IMG_0702.jpeg


Kwanini B-2 haionekani kirahisi na rada hata za kisasa:
  • Muundo wa “Flying Wing” – haina fuselage au tail na engine imefichwa kwenye mabawa (cheki matundu unayoyaona kwaajili ya airflow kuingia kwenye engine)
    IMG_0704.jpeg
  • RCS (Radar Cross Section) iko karibu sawa na ndege ya kawaida au ndege isiyo na rubani
    IMG_0697.jpeg
  • Surface materials zinaabsorb mawimbi ya rada badala ya kuyareflect ili yarudi kwenye radar.
    IMG_0705.jpeg

Kama nchi, Tanzania, tunaweza imiliki?
Kwa sasa, HAIWEZEKANI kwa sababu:
  • Gharama ni kubwa mno kwa bajeti yetu, kuanzia kununua na running cost.
  • Hatuna infrastructure ya kuiendesha
  • Issue ya mafunzo ya kuendesha
  • Sera yetu ya ulinzi si ya mashambulizi ya kimataifa
  • Ni ndege ya “strategic offense” zaidi ya “defensive deterrent”
Mbadala wake sasa?

Badala ya kuota ndoto za B-2, Tanzania tunaweza kuwekeza katika:
  • Fighters wa kati kama JF-17, L-15, au Su-30
  • Drones kwa upelelezi na ulinzi wa mipaka
  • Radar systems za kitaifa
  • Defense electronics – kama EW, signal jamming, na surveillance
  • Kuanzisha viwanda local vya kijeshi kwa matengenezo na assembly ya vifaa vyetu.
Sema tuzidi kuombea Amani na utulivu aya mambo tuyasome Jukwaa la Kimataifa tu.
 
Huyo ndo US, pamoja na li B2 linatikisa dunia ila yupo anajaribu jingine kubwa lake.

Alafu anatoka Ayatollah mmoja shimoni huko kavaa pajama na gauni+kobazi anasema death to America

Sisi acha tuendelee kubonda kokoto na tofali siku ya uhuru tu
Watu wana underestimate uwezo wa mmarekani sana.
 
Hii kitu kama nishawahi kuona filamu moja ya Hollywood inaelezea hii idea. Jina nimeisahau. Ilikuwa ni Sci-fiction film ya kufikirika

Kwa sasa wanahofia kuyaweka huko angani kwa sababu kitu kilichotokea mwaka 1962, ikitokea tu handling yake imeenda vibaya basi tunaweza tukarudi stone age...

US ilifanya test ya kulipua bomu la nuclear mita 400 toka uso wa dunia juu ya kisiwa kinaitwa Johnston...

Aftermath yake ilikuwa ni kuvurugwa kwa mifumo ya mawasiliano kwa sababu ya kuzalishwa kwa EMP (electromagnetic pulse)...
 
Huyo ndo US, pamoja na li B2 linatikisa dunia ila yupo anajaribu jingine kubwa lake.

Alafu anatoka Ayatollah mmoja shimoni huko kavaa pajama na gauni+kobazi anasema death to America

Sisi acha tuendelee kubonda kokoto na tofali siku ya uhuru tu
TRump asongemzuia Neta leo Tehran ingekua magofu na ayatollah angekuwa anazikwa leo na wenzake
 
Back
Top Bottom