Watu waliokufa kipindi ambacho hata dini ya ukristo na uislam hazijaanzishwa wako wapi kama tunajiaminisha kwa kusema dini humfanya mtu kuona pepo?

Dini ilianza kabla ya mwanadamu.

Nabii Aadam Alayh salaam alikuwa muislamu na wote waliofuata walikuwa waislamu.

Ama kuhusu ukristo ni dini za watu hasa warumi ndio dini yao wala hata mungu haijui
Unaweza thibitisha Adam alikuwa muislamu?
 
tunasema Mungu anapenda haki sasa hiyo inawezekanaje mkuu?

Inavyosemekana, binadamu akifa hawezi kurudi tena na kurekebisha chochote alichokwisha fanya kipindi cha uhai wake...

Endapo alikufa kabla ya ujio wa dini, na baadae sana dini zikaletwa, automatic hakuna kinachomuhusu na msamaha unapitishwa kwake moja kwa moja...

Cc: mahondaw
 
Dini ilianza kabla ya mwanadamu.

Nabii Aadam Alayh salaam alikuwa muislamu na wote waliofuata walikuwa waislamu.

Ama kuhusu ukristo ni dini za watu hasa warumi ndio dini yao wala hata mungu haijui
aah kumbe?? Sasa ilikuaje dini hiyo ianze fahamika baada ya muhamadi kuja na si kabla yake?
 
Kipindi gani hicho ambacho dini hazijaletwa? labda utakuwa unakusudia haya majina uislamu na ukristo ndio pengine hayakuwepo kipindi hicho,ukisoma hivyo vitabu vya dini vinaanza kuelezea toka kuumbwa kwa binaadamu wa kwanza.
 
ukiambiwa nini maana ya hayo majina ukristo na uislam utasemaje? na sawa ipo hivi vinaelezea historia ya uumbaji lakini si kwamba zenyewe zilikuwepo
 
Hili jibu lako linamfanya mungu aonekane kama mtu asiyejua anachokifanya kwa maana anaumba mtu na kumtaka huyo mtu amfuate yeye lakini anamnyima huyo mtu njia ya kumfikia yeye.
 
Hili jibu lako linamfanya mungu aonekane kama mtu asiyejua anachokifanya kwa maana anaumba mtu na kumtaka huyo mtu amfuate yeye lakini anamnyima huyo mtu njia ya kumfikia yeye.

Miaka ya nyuma kabisa enzi hizo kabisa, palikua hakuna mahakama za kuhukumu watu kwa utaratibu wala sheria...

Na watu walikua wanaendesha mambo yao kwa namna ilivyo nyakati hizo...

Maana yangu kwamba mambo ya kale huwezi kuyaleta leo... yaliyopita sii ndwele...

Cc: mahondaw
 
Kwa maana nyingine unakubali kuwa dini siyo njia pekee ya kumfikia mungu?
 
ukiambiwa nini maana ya hayo majina ukristo na uislam utasemaje? na sawa ipo hivi vinaelezea historia ya uumbaji lakini si kwamba zenyewe zilikuwepo
Kinachokufanya useme hazikuwepo ni kipi? nimekwambia hivyo vitabu vya dini vimeanza kuelezea toka maisha ya binaadamu wa kwanza,ukisoma humo utaona kuwa kulikuwa na waliyokuwa wakifanya kazi kama walizofanya Yesu na Muhammad na kulikuwa na vitabu, Ingekuwa vizuri mkuu kama ungeanza kuelezea ni kwanini unasema hazikuwepo?
 
Kwasababu Quran imekuja mwaka 610 Baada ya Kristo haiwezi kuwa na jibu la swali hili nzito.

Kwanza mtoa post inaonekana huwa husomi Biblia.

Kwa mjibu wa Biblia watu walio kufa hawaendi popote zaidi ya kuwa kwenye kaburi 1Thesalonike 4:13-18
Wote wanasubiri ufufuo wa kwanza wakati Yesu kristo atakapokuja mara ya pili.

Swali lako lingekuwa hivi.
Waliokufa kabla Injili haijafika maeneo yao je watahukumiwa kwa namna ipi au kwa sheria ipi? Hapo ningekujibu
 
nikikuuliza Elia au Yesu walipaa kwenda wapi utajibu nini? Na pia katika maandiko kinachokufa ni mwili na si roho na pia Yelu mwizi aliyeahidiwa na Yesu pale msalabani(mtini) kuwa hakika leo utakuwa nami kwa BABA mbinguni unataka kuniambia hadi leo hajafika tu peponi(mbinguni) kwa maana si umesema wote wafao wako kaburini hadi sasa?
 
Hahaa.. Huyo Mungu mchoma watu moto if angekuwa anaishi duniani... Angesha shtakiwa ICC
hakuna cha motoni wala hakuna cha peponi

#ila kuna kaburi, jeneza na mchwa..

hivi ulishawahi kuwaza kuwa je, Mungu ukituchoma motoni yeye atafaidika nini haswa?
 
Shetani ni hasimu wa mungu ?
kiumbe chako kinakua hasimu wako aisee ejipange
 
Na maswali yangu juu ya maelezo yako
1.mungu yu ajua yote ,je alipowachagua wayahudi hakujua watamsaliti ?
2.kwamba shetani aliudanganya ulimwengu? mungu alikuwa wapi ? Hakujua shambulio la ghafla?
3.Unaposema waafrica walikuwa na miungu yao na haikuwasumbua hadi mungu aliposalitiwa na vipenzi vyake israel ? Je mungu wa ibrahimu alikuwa unfair kuingilia watu na miungu wao ambao yeye hakuwachagua ?
4.unasema wanadamu wakiongozwa na adamu,adamu amewahi kuwa kiongozi wa wanadamu wote?maana wanaotakiwa waadhibiwe ni hao aliowaongoza.
ukiona huna jibu ya haya jiongeze wajinga ndio waliwao
 
hivi unawezaje mhukumu mtu bila sheria mliokubaliana akiwa na akili timamu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…