Watu walewale kuongoza CHADEMA wataleta mabadiliko?

Watu walewale kuongoza CHADEMA wataleta mabadiliko?

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,505
Reaction score
16,006
Ndugu zangu,

Nilitaka tujifikirishe kidogo; kumetokea mjadala ulioanzishwa na Mbowe na wafuasi wake eti Chadema sasa ina uongozi mpya, watu wenye ''kaliba'' mpya ambao wataleta mabadiliko kwenye siasa za upinzani.

Ili kutenda haki nitaweka majina ya uongozi huo ili sasa tupate wasaa wa kuwajadili kuwa wameingia lini Chadema na walikuwa na nyadhifa gani wakafanya nini na je sasa wataweza kuwa mawakala wa mabadiliko?

1. MWENYEKITI - Freeman Mbowe
2. MAKAMU MWENYEKITI ZANZ - Said Issa Mohamed
3. MAKAMU MWENYEKITI BARA - Tundu A.Lissu
4. KATIBU MKUU - John John Mnyika
5. NAIBU KATIBU MKUU BARA - Benson S. Kigaila
6. NAIBU KATIBU MKUU ZANZIBAR - Salum Mwalim

Katika orodha hapo juu bila kupepesa macho inatengenezwa na watu ambao wamekuwepo kwenye nyadhifa za juu Chadema kwa takribani muongo mmoja uliopita, hao ni watu waliofanya maamuzi mazito ikiwamo ''kutakatisha oil chafu''.

Wazungu wana msemo wao ''You can't teach an old dog new tricks'' wakimaanisha ''watu waliozoea kufanya mambo yao kwa njia fulani hawawezi kuacha tabia zao'' Je, viongozi hawa wa miongo kadhaa ndani ya Chadema wataacha tabia zao za kale? watafundishika?

Waswahili wanasema tabia ni kama ''Tabia ya mtu ni Kama ngozi ya mwili mwili wake. Kuibadili ni kazi kubwa sana. Ukilazimisha, utaendelea kupata matokeo yaleyale'', wengi mnamkumbuka Michael Jackson (Aliwahi kuwa gwiji la muziki, marehemu kwa sasa) alibadili ngozi lakini asili ikabaki palepale zaidi alipata maradhi na kifo, hakuwahi kufurahia ngozi ya kizungu, hata hawa viongozi wanaitwa ''wapya'' huenda wame-jichubua kitakachifuata ni maumivu kama ya Michael Jackson na hata kupelekea ''kufa kisiasa kabisa.

Huu ni mjadala wenye lengo la kuweka sawa watu, ifike pahala wanasiasa wasitumie usahaulifu wa wananchi kuwahadaa.
 
"Jiwe kushindwa ni somo tosha kwamba uzoefu ni muhimu ili kuongoza chama"

Hata mwenyekiti wa kijiji ujawai kuwa ila unakuwa mwenyekiti wa chama

Matokeo yake ndio utateka, utakimbia uchaguzi serikali za mitaa, utaua na kufunga kila mkosoaji wako!
 
Hivi kina Mkuchika, ni vijana wa miaka mingapi? /nawasikia watu wa aina hiyo ndani ya Ccm tangu 70s hadi leo
 
Unataka matusi toka kwa viwavi wa ruzuku wewe.

Zitto kwao ni CCM ila wanajinakifikisha tu.
 
Ninaamini sana watu kama Lissu na Mnyika wana mchango mkubwa wa kukisogeza mbele CDM, japo Mnyika alikuwa Naibu Katibu Mkuu hakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi kama atakaokuwa nao sasa hivi, hili ni sawa na kwa Lissu pia. Nikushauri tu mleta mada ufikishe ujumbe kwa wenzio wa lumumba mumhakikishie Lissu usalama wake ili aweze kurudi nyumbani kutekeleza majukumu yake mapya ndani ya chama chake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Jiwe kushindwa ni somo tosha kwamba uzoefu ni muhimu ili kuongoza chama"

Hata mwenyekiti wa kijiji ujawai kuwa ila unakuwa mwenyekiti wa chama

Matokeo yake ndio utateka, utakimbia uchaguzi serikali za mitaa, utaua na kufunga kila mkosoaji wako!
Nje ya mada kamanda, jielekeze kwenye hoja. ''can you teach old dogs new tricks?''
 
Unamaanisha kuwa CCM imekaa madarakani toka tupate Uhuru mpaka leo kwahiyo sasa lazima itoke madarakani kwasababu haina mbinu mpya za kuongoza nchi zaidi tu Inatumia vyombo Vya ulinzi Kubaki madarakani?
 
Back
Top Bottom