Watu walewale kuongoza CHADEMA wataleta mabadiliko?

Watu walewale kuongoza CHADEMA wataleta mabadiliko?

CCM miaka 58 bila maendeleo wakati ni Nchi tajiri yenye rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani, Tanzania isingekuwa chini ya utawala wa CCM leo hii ingekuwa ni Nchi tajiri kuliko South Africa na hata Nchi za ulaya.
👍👍👍👍👍👍👍
 
CDM wameshafanya uchaguzi wao,tuwaombee wafanye kazi walizokubaliana ktk chama, kuzidi kuhoji ni ujinga, ulimbukeni na kukosa hoja za kuvuruga. Tuwaombee kwani 'mbwa mwitu' anawawinda kila uchwao.
 
Nje ya mada kamanda, jielekeze kwenye hoja. ''can you teach old dogs new tricks?''
Unafahamu kuwa Rais Magufuli kabla ya kuwa Rais alikuwa ndani ya baraza la mawaziri kwa takribani miaka 20? Unajuwa kuwa katika yote mazuri na mabaya ya Mkapa alikuwa sehemu ya maamuzi? Unajua amefanya kazi siku zote na Kikwete na mazuri na mabaya yake yeye pia anahusika kama waziri mwandamizi?
Sasa rudia tena swali lako!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafahamu kuwa Rais Magufuli kabla ya kuwa Rais alikuwa ndani ya baraza la mawaziri kwa takribani miaka 20? Unajuwa kuwa katika yote mazuri na mabaya ya Mkapa alikuwa sehemu ya maamuzi? Unajua amefanya kazi siku zote na Kikwete na mazuri na mabaya yake yeye pia anahusika kama waziri mwandamizi?
Sasa rudia tena swali lako!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni sahihi kubadili vyeo nimjuavyo kama angekosa urais angashastaafu siasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu,

Nilitaka tujifikirishe kidogo; kumetokea mjadala ulioanzishwa na Mbowe na wafuasi wake eti Chadema sasa ina uongozi mpya, watu wenye ''kaliba'' mpya ambao wataleta mabadiliko kwenye siasa za upinzani.

Ili kutenda haki nitaweka majina ya uongozi huo ili sasa tupate wasaa wa kuwajadili kuwa wameingia lini Chadema na walikuwa na nyadhifa gani wakafanya nini na je sasa wataweza kuwa mawakala wa mabadiliko?

1. MWENYEKITI - Freeman Mbowe
2. MAKAMU MWENYEKITI ZANZ - Said Issa Mohamed
3. MAKAMU MWENYEKITI BARA - Tundu A.Lissu
4. KATIBU MKUU - John John Mnyika
5. NAIBU KATIBU MKUU BARA - Benson S. Kigaila
6. NAIBU KATIBU MKUU ZANZIBAR - Salum Mwalim

Katika orodha hapo juu bila kupepesa macho inatengenezwa na watu ambao wamekuwepo kwenye nyadhifa za juu Chadema kwa takribani muongo mmoja uliopita, hao ni watu waliofanya maamuzi mazito ikiwamo ''kutakatisha oil chafu''.

Wazungu wana msemo wao ''You can't teach an old dog new tricks'' wakimaanisha ''watu waliozoea kufanya mambo yao kwa njia fulani hawawezi kuacha tabia zao'' Je, viongozi hawa wa miongo kadhaa ndani ya Chadema wataacha tabia zao za kale? watafundishika?

Waswahili wanasema tabia ni kama ''Tabia ya mtu ni Kama ngozi ya mwili mwili wake. Kuibadili ni kazi kubwa sana. Ukilazimisha, utaendelea kupata matokeo yaleyale'', wengi mnamkumbuka Michael Jackson (Aliwahi kuwa gwiji la muziki, marehemu kwa sasa) alibadili ngozi lakini asili ikabaki palepale zaidi alipata maradhi na kifo, hakuwahi kufurahia ngozi ya kizungu, hata hawa viongozi wanaitwa ''wapya'' huenda wame-jichubua kitakachifuata ni maumivu kama ya Michael Jackson na hata kupelekea ''kufa kisiasa kabisa.

Huu ni mjadala wenye lengo la kuweka sawa watu, ifike pahala wanasiasa wasitumie usahaulifu wa wananchi kuwahadaa.

Kwa yanayotokea katika chaguzi ni majibu tosha kuwa chadema ni kiboko ya ccm, hamuitakii mema cdm kiasi hicho. Mnajua fika hakuna uchaguzi wa HAKI. JARIBUNI KUFANYA UCHAGUZI WA HAKI MJUTE.
 
Kwa yanayotokea katika chaguzi ni majibu tosha kuwa chadema ni kiboko ya ccm, hamuitakii mema cdm kiasi hicho. Mnajua fika hakuna uchaguzi wa HAKI. JARIBUNI KUFANYA UCHAGUZI WA HAKI MJUTE.
Chadema ni kama "Punda anayekufa,hurusha teke la mwisho kwa kishindo......"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom