Watu wala watu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
284,235
738,453
Huwezi kupata neno bora zaidi la kuwaelezea watu hawa wanaokula nyama ya binadamu wenzao tunawashangaa sana dini ya mashetani wanapokula nyama ya mtu kwenye ibada zao, lakini hawa ni cha mtoto

Hapo jirani yetu tu Uganda hawa watu wapo WATU WALA WATUna hii si Uganda ama Afrika tu bali ni kitu kinachofanyika sehemu mbali mbali za dunia, watu wala watu wako popote duniani

-kuna wale wala nyama mbichi
-kuna wale wala ya kuchoma ama kubanika
Kuna wale wala mchemsho.

Hawa wenye hizi tamaduni wamegawanyika katika makundi tofauti tofauti
-walao nyama ya maiti, wao hawamgusi mtu mpaka afe mwenyewe, hapa wanajivua dhambi ya kuua.... Wanaona bora wapate walau faida ya kitoweo kuliko kwenda kuzika na kuifaidisha minyoo
-walao nyama ya wageni, hapa wao kwa wao hawadhuriani ila akitokea mgeni kufika kijijini kwao, huyo hatoki salama na kama amekondakonda watamlisha chakula kizuri anenepe kwanza
-Kundi la mwisho ni mumiani na waviziaji... Hawa wako kwenye jamii mbalimbali zisizo fanya hayo mambo, lakini wao kwa siri na kificho hufanya, hawa huvizia watu kuwateka na kwenda kuwageuza asusa huwa nacheka kweli nikiona watu huku kwetu wanaambiana NA NIKIFA UNILE NYAMA ama AKIFA HUYU UTAMLA NYAMA..... jamani kama ni huko kwa wala nyama kweli hiyo ni ruhusa isiyo na mawaa
 
Nasikia na wale jamaa wa kwenye misitu minene pale Zaire wanakula sana Nyama za Watu, Ila hawalani wao kwa wao bali wakimuona mtu mrefu.
Kwa sababu wao mtu mrefu ni Kiumbe cha Ajabu.
 
Nasikia ni tamu sana eti zaidi ya kitimoto
tapatalk_1491766302810.gif
 
Kwenye kitabu cha Mbiki ..The Living Dead... ameongelea haya mambo kwa kiasi chake katika tamaduni za Afrika na hasa A. Mashariki mshana jr
 
Back
Top Bottom