malisak
JF-Expert Member
- Mar 16, 2006
- 694
- 772
Jamani ndugu zangu wa Tanga kwani alietuloga nani? fursa tunazisikia ila hata hatushtuki wanakuja walowezi wanajizolea fursa na sisi tupo hapa hapa kweli, zinatangazwa zabuni mpo kimya mnakuja kukurupuka dakika za majeruhi watu wameshasafirikutoka mikoani mbali huko kukimbilia fursa.
Na hata mkipewa nafasi hamchangamkii mpk mnawapa watu nafasi ya kujipandikiza na kuwahia nafasi kupitia wachahce wenye nazo ambao ni waroho na wenye tamaa ya pesa. Halafu mnalalamika mji unazidi kufa wakati pesa zimekuja na zinaondoka kurudi mikoa mingin. Mradi wa ujenzi wa Jetty ungekuwa umetangazwa vizuri na vyombo vya habari vya hapa tanga na serikali kwa ujumla.
Huu mradi ungerudisha hadhi ya mkoa wetu kwa jinsi ulivyo na tija ila cha kusikitka hata wale waliofidiwa baada yakupisha eneo la ujenzi badala ya kuzungusha mrdini pesa wengi wamekwenda kuoa kuongeza wake wengine eeeehh Mungu baba. Nini shida?
Kunahaja kupaza sauti kurudisha mkoa kwenye chati yake, fikiria mkoa umeshakuwa jiji lkn ni kheri hata kipindi ulipokuwa mji. Wana Tanga tuamke jamani hali tete inaumiza. Viwanda vimebaki kama magofu, wagosi wa kaya wamechoka kupiga kelel wameamua kujiajiri nchi imewekwa bond.