Watu wa Tanga nawaita hapa

Watu wa Tanga nawaita hapa

Vijana Tanga wote wamekimbilia Dar,wamebakia wazee,ila twende mbele turudi nyuma Tanga pazuri sana.Ukitaka kuifaidi Tanga uwe na Baiskeli au Usafiri wako binafsi,halafu uanze kutembelea mitaa unayotaka wewe ,isiwe ni boba au Taxi,ni mji mzuri kiasi chake.....
Mji ni mzuri sawa, lakini tatizo la Tanga huwezi kuishi mtu mpambanaji lazima upachukie sana.

Tanga wanaamka saa nne alafu biashara zafungwa saa 9 alasiri.....
Weekend yaanza alhamisi sheihk.
Panaboa sana....
 
Mahali palipo na uchawi na uganga ni ngumu sana watu kuwa na maendeleo...
Hakuna mikoa mzito kama Dar kwa Uchawi logwa ndio utaelewa ukipona Malaika wako WA ulinzi wakali saba
 
Yaani Gofu juu Industrial Area imebaki Magofu magofu matupu kama jina lake labda jila limeleta laana sasa wanafanya ofisi za baadhi ya taasisi za serikali kama TANroads, Temesa etc yaani ni huzni kubwa
umesahau kiwanda cha sabuni ya mbuni
Kiwanda cha mablkanket
MAmlaka ya mkonge ndio inafufuka sasa
Kiwanda cha foma
Kiwanda cha mashuka cha CIC na somaia Group
Vyote vilikuwa na tija na vilitoa ajira nyingi sana. Kiwanda cha mbolea kimeuzwa imekuwa Depot ya mafuta ya Kampuni ya GBP ni huzuni kitambo sijaja nimekuja naona mtu mmoja unakutana nae mjini mara sita kwa siku jinsi ambavyo hakuna watu
Alielipa lile eneo jina la gofu juu ana asili ya unabii maana limekuwa magofu hasa serikali ndio imekurupuka na kuanza kufungua baadhi ya maofisi Yao kule. Na Watu wengi sasa hivi NI wageni
 
Tanga hakuna project ya maana ya serikali. Mimi nilienda 2019, yaani hawana chochote wanajenga tangu Nyerere alimaliza. Mkoa zimebaki alama tu kwamba palikuwa na bandari. Yenyewe juzi hapa Magufuli ndio kaifufua.
Rudi kusoma tena habari za tanga. Project ya bomba la mafuta la afrika mashariki Kwa sehemu kubwa zaidi ya asilimia 50 mradi unatekelezewa tanga na hata bandari imefungwa wamepisha ujenzi WA Jet load off facility Kuna terminal construction na Tanks EPC, AGI na PPL,barabara ya sadani -pangani na pangani tanga,uwanja wa TFF academy na haujaisha bado,EACOP ikimalizika wanakarabati bandari shida wazawa ndio wamekufa kimaarifa halafu wanalalamika. Hiyo ni baadhi ya miradi ndg hujafanya research muda mrefu inaelekea, rudia tena.
 
...Inahuzunisha Sana ! [emoji45] Ukikumbuka Tangold iliyotoa Juisi ya Embe iliyokuwa Nzito na Tamu Sana!
Kiwanda Cha Sabuni kilichotoa Mbuni na Gardenia.
Kiwanda Cha Chuma.
Kiwanda Cha Mbolea
Kiwanda Cha Plastiki Amboni zilikotoka ndoo na mabeseni Bora vya Plastiki.

...vyote vimebaki Historian TU.

Tanga kunani palee ?
Acha ni huzuni kwakweli kiwanda Cha chuma kimefufuliwa ila naona wanzalisha misumari tu
 
Maamuzi yote ya serikali nyingine mbwembwe tu wala hamna cha maana basi mbona Dodoma inakuwa kwa kasi?

Acheni ushamba kuna watu wanaishi Dar huko kwao wamekimbia, waha kibao ni wafanyabiashara hapa Dar kwao kigoma choka mbaya ila ni wachapakazi na wana pesa hapa mjini.

Watu wanafuata fursa bila ya bandari na mashamba ya mkonge pengine pasingekuwa na mkoa wa Tanga, sasa hivyo kama base ya mkoa vimekufa unatakaje sasa?😅

Peleka fursa sehemu, ukiangalia sehemu nyingi majengo ni sehemu za biashara kama mahotels, malls za kisasa, kumbi za mikutano, vyuo, sehemu za huduma za kijamii kama hospital, ofisi za kupangisha pamoja na majengo ya wizara mbali, je uliona wapi mkoa ulioendelea hapa bongo pakawa hata na storey buildings za floor 5 ambazo ni nyumba ya mtu binafsi? Labda zipe apartments za biashara. Hao majengo ndo yanaletq mvuto kwenye miji yote hapa Tanzania wala sio life standard ya watu kwa nyumba mtu binafsi.

Unaweza kwenda kweny mji umeendelea ukakuta jengo kubwa ni ofisi ya posta 😅😅au hotel eti ndio maendeleo ya Bongo.
Rudia kusoma post Kwa kina
 
Back
Top Bottom