Mafunzo ya USAID-Afya Yangu kwa vijana yawanufaisha vijana wa Wilaya ya Kaliua

Feb 17, 2024
1
0
Nilidhamiria kutoka Mwanza na kwenda kupiga kambi katika Mkoa wa Tabora. Katika Manispaa ya Tabora, hakuna daladala katikati ya mji, kitu ambacho kilinishangaza, watu wengi hutumia bajaji na boda boda katikati ya mji, na daladala zinatumika zaidi kwenda sehemu za nje ya mji.

Nilipata nafasi ya kukutana na Melesiana Charles, binti machachari mwenye umri wa miaka 21 katika Wilaya ya Kaliua-Tabora. Melesiana alipata mafunzo mwaka 2023, mafunzo hayo yalikuwa ya siku 9, kupitia mradi wa USAID-Afya Yangu na katika mafunzo hayo, somo la stadi za maisha lilimkuna vilivyo. Baada ya mafunzo hayo, Melesiana aliamua kutunza pesa kidogo aliyoipata kutoka kwenye mafunzo (per-diem) na kuamua kurudi nyumbani na kuomba kuongezewa mtaji na wazazi wake. Alichokifanya, alikwenda sehemu ya jirani kwa fundi cherehani anayeitwa Dorethea alimaarufu Mama Isa na kuomba kufundishwa namna ya kushona, ambapo alimlipa fundi huyo kiasi cha tsh. 20,000 kwa mwezi kulipia mafunzo, na kujifunza kwa miezi mitatu, Melesiana alifungua ofisi yake katika soko la hapa Igagala namba 5 Kaliua na kununua cherehani iliyomgharimu kiasi cha tsh. 260,000.

Ni takribani miezi 9 tangu Melesiana afungue biashara yake, ambapo kwa mwezi anajiingizia kipato kati ya tsh. 50,000-100,000 Melesiana anawasaidia vijana kama yeye walio katika eneo lake kufahamu kuhusu afya ya uzazi, uzazi wa mpango, kujitambua na masuala ya kiuchumi. Hakika Melesiana ni kijana wa mfano!

Andiko hili limeandikwa na: Celina Baragwiha, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Amani Girls Organization.

Kuhusu USAID-Afya Yangu: https://www.usaid.gov/sites/default/files/202212/USAID_Afya_Yangu RMNCAH_Factsheet.pdf
 
Back
Top Bottom