Watu wa dini wanaamini wasichokijua

Watu wa dini wanaamini wasichokijua

Labda na wewe utaongeza kitu hapo chini.

1. Binafsi siwezi kuamini kitu ambacho sikielewi.

Watu wa Sayansi walikataa kuamini wakachagua kuelewa na ndio wameleta ustaarabu duniani. Hii ni tofauti na watu wa dini.

2. Dini ni Chombo cha kijamii(social agency) Chenye kazi ya kuhimiza Maadili, na Ushirikiano kwenye jamii. Kuhusu kumpata Mungu kupitia hizi dini zetu hizi napata wasiwasi maana hata dini zenyewe bado hazimjui Mungu, zinakinzana kuhusu Mungu.

Kila dini inamuelezea Mungu kwa njia tofauti. Hata amri na sheria za dini ni tofauti. Kila dini imechagua mungu wa kumuabudu.

3. Imani ya kiroho haifundishwi, hakuna haja ya kushawishi, kutisha, kulazimisha au kumshurutisha mtu aamini kama wewe unavyo amini, hiyo inakuwa sio spirtual inakuwa ni kama siasa na kampeni za uchaguzi.

Mambo ya kiroho ni automatic tu. Dini zetu hizi zimeingia kwa ushawishi, vita na vitisho napata wasiwasi zilikuja ili watu wamjue Mungu au kuna agenda za siri?🤔Aliyetufanya watumwa ndiye aliyetupa vitabu tunavyoviita vitakatifu😀😀

4. Tofauti yetu na wanyama ni utashi, Binadamu tunautashi mkubwa ila wote tunaongozwa na kanuni zinazofanana: wote tuna struggle for existence, kuna survival of the fittest and Natural Selection.

Binadamu tunauwana tukigombania resources, Madaraka n.k the same applied to wild animals.

Soma Pia: Huu ndio utofauti kati ya watu wa dini(Religion) na kiroho(spiritual)

Dini ipo kuhakikisha hatuvuki mipaka tunapo strugle for existence ndio maana unaambiwa usiibe, usiue, usitamani mali ya jirani yako n.k. Hizo ni sheria na amri za maadili.

5. Shetani je?😀 ni kiumbe cha kusadikika, imaginary creature kimeundwa na watu wa dini maalum kukutisha na ili usitoke nje ya box ndio maana utashangaa pamoja na huu utitiri wa dini uliopo ambao kazi yao kubwa ni kumkemea shetani ila hadi sasa hawajafanikiwa kwenye hilo..Why? Jibu ni kwamba wanakemea kitu ambacho hakipo.

6. Je, tunaweza kuwa na maadili bila uwepo wa dini?sheria za nchi hazitoshi? Au wewe unaonaje?

7.
8.

SIJAYASOMA MAELEZO YAKO KWA UNDANI ILA NAOMBA NIJIKITE KWENYE TITLE YA THREAD YAKO TU. NAOMBA UREKEBISHE TITLE YAKO ISOMEKE HIVI;

THEISTS AU WANAOMWAMINI MUNGU WA KWELI HUWA WANAANZA KWA KUAMINI WANACHOKIJUA, NA BAADHI YA MAMBO WASIYOYAJUA, HALAFU BAADAYE WANAKUJA KUJUA WALIVHOKUWA WANAKIAMINI BILA KUIKIJUA NA HATIMAYE KILE AMBACHO HAWAHITAJI KABISA KUKIAMINI.

YOU ARE BEING TOO BROAD KWA KUONGELEA DINI KWA SABABU HATA PAGANISM NI DINII PIA
 
Back
Top Bottom