Watu wa dini chukueni credit kwa Corona!

Kuna mataifa makubwa mawili
Iran (Muslim)

Italy (Roman’s) Corona inawatesa kupita kiasi. Dini ni imani ya mtu, kuna watu wamezoea kila jambo kusema tunamuachia Mungu au Mungu ndio anaejua, hizi kauli zikitumika tutaangamia wote. Nchi kama China na mataifa mengine wanajua kusali peke yake ni upuuzi hakutaondoa hili janga na kuchukua counter measures mapema ikiwemo watu kukaa majumbami kwao na nchi nyingine pia wamechukua hatua kama hizo.

Imedhihirisha maombi hayawezi kusaidia kuondoka kwa ugonjwa huu bali ni juhudi na nguvu za kuungana pamoja na kutafta kila mbinu kuweza kuuzuia usiingie sehem ambazo bado haujafika pia kuwatenga wale ambao wameathirika,

kwa upande wangu dini ziliweka ili ziweze kumpa mtu hofu au uwoga wa kufanya jambo fulani bata katika jamani pia ni kama njia ya kukupa imani na nguvu (hope) katika maisha yako lakini dini sio tiba ya magonjwa, migogoro, njaa wala vita.

Corona imedhibitisha ulimwengu kua wanasayansi wanahitajika zaidi kuliko maombi.

8bebd0ef-e9a6-4f9c-b03f-12b7a2ec2d29.jpg
7c84ab51-dcec-4dfa-9e97-567542116287.jpg
5a0ea0d6-51f6-43c6-a31d-a07bca3199fe.jpg
2bb0ac86-324f-4d77-8584-879d76ca9605.jpg
49a9463e-3b72-4d94-8a75-8f472c3c66dd.jpg
489d1dd6-53a0-4227-884d-1ed61db2fd72.jpg
 
Dini haijafeli, bado dunia haijafikia hapo mkuu. Madaktari wanaopambana na wagonjwa wa corona watakuwa wanasali isiwapate. Mama, baba na ndugu zao wanasali wawe salama. Trust me, ukipata tatizo la kiafya utaombewa sana tu. Inawezekana hata utakapokufa watu wakakuombea huko uendako. Dini ipo, na ipo active sana.

Wewe ndio unasema wanasali sana. Lakini wao wanahakikisha wanavaa kwa makini Protective Gears kuhakikisha wanajikinga. Hilo swala la kusali itakuwa ni lako wewe.
 
Wewe ndio unasema wanasali sana. Lakini wao wanahakikisha wanavaa kwa makini Protective Gears kuhakikisha wanajikinga. Hilo swala la kusali itakuwa ni lako wewe.
Ni langu ndio, hakuna sehemu nimesema si langu. Naamini wanasali, hata wakivaa vyuma bado wataona haitoshi watasali kila mtu na imani yake. Binadamu wapagani ni wachache sana. Naamini Tukiwajumlisha hamfiki hata robo ya binadamu wote sababu kiuhalisia kutokujua siri ya uhai kunatufanya tuamini katika MUNGU
 
Hapa ndipo utajua kumbe habari za dini ni storiea tu.

Sent from my typewriter using Tapatalk
Cha ajabu maeneo yanayojifanya yana dini sana ndo watu wanakufa balaa.

Satellite za CNN zimegundua Iran inapanua maeneo ya makaburi kisa vifo kuongezeka! Aeatolah kalala tu hamuiti Allah!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ndipo utakapojua kuwa habari za dini ni stori za kutunga tu hazina kweli yoyote
Sayansi ndio Kila kitu na inaposhindwa dunia itaangaamia
 
Ni langu ndio, hakuna sehemu nimesema si langu. Naamini wanasali, hata wakivaa vyuma bado wataona haitoshi watasali kila mtu na imani yake. Binadamu wapagani ni wachache sana. Naamini Tukiwajumlisha hamfiki hata robo ya binadamu wote sababu kiuhalisia kutokujua siri ya uhai kunatufanya tuamini katika MUNGU

Umejuaje Mungu unayemuamini ni Mungu sahihi uliyepaswa kumuamini ?
 
Jumong S, Mungu hawezi kuthibitishwa na uwepo au kutokuwepo kwa ugonjwa wa Corona.

Ata kifo chenyewe hakitoshi kuthibitisha kutokuwepo kwa Mungu.

Maana maandiko yanasema wazi kuna watu vifo havikuwa kitu kwao mfano HENOKO mwanzo 5:1... hakuonja hayo mauti, pia Elia ila mwisho wa yote MWAMBA JESUS KRISTO, yeye kashuka kuzimu na kurudi kishujaa kabisa.

Mwisho tangia leo, ujue kabisa Mungu anayehubiriwa si Mungu miili na mambo yanayoambatana na hofu za kimwili maana kwa walio wake wanahofu ya kufa kiroho na si kimwili.

Utambue pia watu zaidi ya 170k ila vifo ata elfu 10000 bado kwanini usijiulize kila anayepata alitakiwa kufa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom