Mh! Umenikumbusha mbali aisee! Kuna siku moja nilienda kunywa chai kwenye mgahawa mmoja nikaagiza chai,chapati na maharage! Wee acha tu, siku ile sitaisahau nilishinda kwa tabu sana! Nimekunywa chai na chapati ya kwanza vizuri tu nikachukua chapati ya pili ile nakaribia kumaliza chapati ya pili dah! nikachota kijiko cha maharage ile natafuna nikaona nimetafuna kitu laini kuliko maharage halafu kikubwa kuliko majarage na ladha tofauti na maharage duh! Nikashtuka nikatema mkononi kumbe ihiiii nimemtafuna mende tena yale makubwa aisee! Nilitamani kutapika lakini wapi, ikabidi nimuonyeshe mwenye mgahawa aibu ilioje ilibidi asinidai hata hela, ila mi siku hio nilishinda bila kula nilikuja kula usiku, usiombe utoko wa mende unaweza kulazwa hospitalini kwa kutapika.