Watu maarufu duniani waliofariki kabla ya kufikisha miaka 50

Chadwick Boseman amefariki akiwa na miaka 43 anakumbukwa zaidi alivyoigiza filamu ya Black Panther
 
Wameshamtaja Yesu wa Nazarethi?
Nahisi ni maarufu zaidi kushinda hao wote wengine. Alikufa alipokuwa na umri wa takriban miaka 30-33.
 
Stanslaus Katabalo, alikufa akitetea ardhi ya Wamasai Loliondo isigawiwe. Sina uhakika na age lakini itakuwa early or late 30s.
Loliondo gate na TBL gate nadhani kama sio gazeti la mfanyakazi basi lilikuwa gazeti la moto moto au heko sikumbuki uzuri
 
Ferdinand Magellan (41)- Huyu alikuwa mtu wa kwanza kusafri na kuizunguka dunia kwa mashua akathindisha kuwa dunia ni mduara. Navigation Satellites za Ulaya zimepewa jina lake
Hivi njombe pale sio duniani...??hiyo mashua ilipita tale au sangamela

Njombe kuna bahari?
 
Alikuwa anatoka Dodi Al Fayed billionaire wa Kiarabu aliyekuwa akiishi France yeye na familia yake ni wamiliki wa chain of Supermarkets na biashara nyingine Ulaya ,inasemekana "Eti" Princess tayari alikuwa na ujauzito wa huyo Billionaire na walikuwa ktk harakati za kufunga ndoa kitu kilichotafsiriwa km kashfa kubwa kwa Royal family.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hii niliisikia sana mwaka huo wa 1997 na 1998 kuwa baba yake Dodi ndiye aliewekeza sana kuhakikisha kijana wake anazaa na Diana. Kwa hiyo aligharimia raha nyingi sana kwa Diana kuliko alizokuwa akipata kwenye ufalme, na kuna wakati ambapo kijana huyo alitumwa kuwa anajimiana na Diana kwa karibu mwezi mzima bila kupumzika wakati wakiwa vacation huko Ugiriki kusudi mimba ipatikane. Sijui kama habari hizo ni kweli kwani ushshidi ulizimika nao; ila sasa hii conspiracy ya kumwua diana kutokana na hilo kweli huwa siliamini kwani ilikuwa ni accident iliyotokana na wao kwenda mwendo wa kasi kujaribu kuepuka mapaparazi
 
Emil von Zelewski (-37), aliyeshindwa na Mkwawa mwaka 1891 wakati wa ukoloni wa Ujerumani hapa; alikuwa mkuu wa jeshi la Kijerumani katika koloni alitaka kumvinda Mkwawa. Kumbe hakutegema Mkwawa anamsubiri tu aliongoza vikosi vyake moja kwa moja katika tego lililoandaliwa pale Lugalo. Angalau amepata baadaye jiwe zuri la kumbukumbu. Hata hivyo alikuwa mkoloni Mjerumani aliyeshindwa vibaya sana, hasa kutokana na azimio lake la kuachana na upelelezi wa njia aliyotumia.
(kwa undani zaidi: Wikipedia ya Kiswahili kuhusu Zelewski na Lugalo,
Zelewski's last stand (tovuti yenye habari za undani za mapigano, kwa Kiingereza)
 
Hii niliisikia sana mwaka huo wa 1997 na 1998 kuwa baba yake Dodi ndiye aliewekeza sana kuhakikisha kijana wake anazaa na Diana. Kwa hiyo aligharimia raha nyingi sana kwa Diana kuliko alizokuwa akipata kwenye ufalme, na kuna wakati ambapo kijana huyo alitumwa kuwa anajimiana na Diana kwa karibu mwezi mzima bila kupumzika wakati wakiwa vacation huko Ugiriki kusudi mimba ipatikane. Sijui kama habari hizo ni kweli kwani ushshidi ulizimika nao; ila sasa hii conspiracy ya kumwua diana kutokana na hilo kweli huwa siliamini kwani ilikuwa ni accident iliyotokana na wao kwenda mwendo wa kasi kujaribu kuepuka mapaparazi
Inawezekana Kuna ukweli, maana inasemekana Diana alikuwa na mimba baada ya taarifa kuufikia ukoo wa kifalme hawakutaka mfalme wa uingereza awe na ndugu waarabu toka misri maana wangekuwa mama mmoja baba mbalimbali.

Nadhani ni sahihi kwa Diana Kufa.
 
Kwenye hii list umemsahau aliyekuwa mpnz wa Complex marehemu Vivian Tilya a.k.a vi to the vy ,hakika huyu dada nilikuwa namkubali sana kwenye kazi yake utangazaji
Alikua anatangaza Clouds Fm,walipata ajali ya gari akienda kumtambulisha Complex Arusha
 
Back
Top Bottom