Watu huchochea watu wengine watende mambo mabaya

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,459
17,268
Unaweza kua mtu mwema, unafanya mambo yako vizuri, unafurahia maisha lakini mtu ama watu wakasababisha ukafikiria kufanya kitu ambacho hujawahi kukifikiria.

Watu wanaweza kusababisha mtu ufikirie kutenda mambo mabaya sana kwenye maisha yao.

Kuna mtu nilifanya nae kazi, nikamfanyia kazi yake vizuri kabisa na makubaliano yalikua anilipe pesa yangu nyingi tu lakini baada ya kazi jamaa anajiona kama mjanja na mimi mjinga.

Nikifikiria kazi niliyofanya kwa uaminifu mkubwa na kwa kujitoa kwa moyo wangu wote kisha mtu baada ya kufanikiwa mambo yake anajiona mjanja ama ananiona mimi mjinga roho inaumia sana.

Nafikiria vitu vibaya sana sasa ambavyo sijawahi kuvifikiria kabisa, nafikiri getting a hitman or poison him with deadly poison or whatever ila he will get what is coming to him very soon.
 
Noo usifikiri vibaya hivyo kumbuka Dunia tunapita mkuu Mali , pesa tutaviacha na tutalala mavumbini , Cha kufanya wewe tulia Mungu ndo atakulipa remember malipo ni hapa chini ya jua adhabu kali ataipata kwa Muumba na wewe amini nakuambia Mungu hawezi kukuacha tu ivi lazima atakulipa kwa mema
 
Pole mkuu huyo usimumuwekee sumu kwani ikifahamika utaenda jela bure,, huyo dawa muendee kwa mzee makombo ya gari, anamtoa jipu la ulimi mchana kweupee.
 
Kila kitu ambacho unakifanya leo kiwe kibaya au kizuri baadae kinakuwa na matokeo
Watu wengi huwa tunalaumu kwa vitu ambavyo hatuna na tunasahu kwa vitu tulivyonavyo

Kuzulumiwa haki inauma sana lakini muombe MUNGU akusaidie haki yako ikaonekane bila ubaya wowote kufanyika

Kuna mtu mmoja amewahi sema ukiona umekosa kitu kizuri basi ujue kitu kizuri zaidi kinakuja piga moyo konde.
 
Pole sana mkuu...

Ukitendwa unaumia sana, katikati ya machungu unawaza hutomaliza simanzi yako,nataka kukuhakikishia utavuka mkuu, many have crossed that path before...utapona majeraha, just have some faith...
 
Mkuu The Underboss ukisema ulipe kisasi utaondoka na mzigo mzito sana. Na umeshafikiria ukisema ulipe kisasi, utakuwa unawalipa kisasi wangapi, maana dunia ya sasa ina watu wa hovyo haijawahi kutokea.
Cha msingi achana na mambo ya yeye kukuona mjinga, huo ni mtazamo tu. Mungu atakulipa kwa muda wake.
Nimefanyiwa ubaya na watu wengi sana, lakini ninajitahidi kusamehe na nisiwembaya kama wao. Kwa sababu ukilipa ubaya, unakuwa hauna tofauti na wao. Let it pass, kipindi hiki ndiyo unatakiwa kuwa calm, mawazo mabaya yatakuja na kuondoka lakini ubaya utabaki palepale kama utalipa ubaya.
 
Ubaya haulipwi kwa ubaya, bali ubaya hulipwa kwa wema. Ikitokea umekutana naye, msalimie kiroho safi kabisa, na ikitokea kapata matatizo, au kakwama, hana msaada wowote, na kwamba amekata tamaa, wewe jitokeze na umpe msaada. Hakika hapo utakuwa kama umemuunguza na kaa la moto, lakini wakati huohuo wewe unapata thawabu kwa Mungu.

Habari ya kulipiza kisasi achana nayo na wala usiifikirie kabisa. Kulipiza kisasi sio suluhisho, unaweza ukaongeza tatizo juu ya tatizo. Labda utauliza kivipi? Binadamu yeyote ameumbwa na roho ya huruma (hata awe jambazi). Sasa ukiamua kumdhuru kwa namna yoyote ile huyo mbaya wako, unaweza kumuathiri kiasi cha kuharibu viongo vyake au hata kifo. Umesema unatamani umpe hata sumu, je akifa, na pengine familia yake (mke, watoto, nk) wanamtegemea yeye, watoto wakianza kutaabika kutokana na kukosa malezi, huoni kama hili litakuathiri kisaikolojia? Utakuwa umejiongezea tatizo badala ya kupunguza!
 
Back
Top Bottom