Kweli jamani.
Halafu mateso kwa mtoto sio hadi umchape viboko, mi nakumbuka nilipokuwa mtoto walikuwa wananifungia ndani, hakuna kutoka nje. Tulikuwa hatuna housegirl na watu wote walikuwa na mishemishe kurudi hadi jioni.
Dah, wapeni uhuru watoto wenu jamani.
Kweli kabisa....kitendo tu cha kumnyima mtoto kua mtoto ni mateso tosha!!Pole mwaya!
Kweli jamani.
Halafu mateso kwa mtoto sio hadi umchape viboko, mi nakumbuka nilipokuwa mtoto walikuwa wananifungia ndani, hakuna kutoka nje. Tulikuwa hatuna housegirl na watu wote walikuwa na mishemishe kurudi hadi jioni.
Dah, wapeni uhuru watoto wenu jamani.
dah,lizzy acha tu dada yangu,mi nakumbuka utoto wangu nilikuwa napenda kweli kucheza mpira na kila ikifika muda wa ugali saa saba mi sina habari,hiyo ilikuwa mitaa ya sinza mwaka 1980,
basi huyo mdogo wake mama aliyekuwa ameletwa kutulea alikuwa anatutembeza kwa magoti kwenye foundation ya nyumba iliyokuwa jirani mpaka magoti yanachubuka kisha unaogeshwa na kuvalishwa suruali ili usionekane ulivyochubuka na kwa sababu ya utoto unalia kimya kimya tu ukiogopa kuwa nikisema kipondo cha kesho kitazidi,jamani tuwasaidieni hawa watoto kwa kuwa baadhi yetu tumepitia huko.
POLE SANA MKUU. NASHUKURU KUWA ULIWEZA KUVUMILIA HADI KUKUA MKUBWA. WENGINE HUTESWA WAKAISHIA ULEMAVU WA KUDUMU AU KUPOTEZA MAISHA KABISA.
Kila tulipo tujaribu kusaidia kuwafunza wazazi wenzetu juu la malezi bora ya mtoto. Adhabu kupindukia na mateso havimfunzi mtoto bali kumfanya awe sugu na akuchukie maisha.
mmhh Lizzy,
leo umenikumbusha mbali mpendwa.
ni kweli inakaa na wewe milele..
na inachangia sana na nini unafanya ukubwani..
mara nyingi unafanya vitu ajili ya hasira au uwoga..
mie sinta changia sana
ni hayo tu
bali asante sana mpenzi....