safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 12,312
- 18,185
Kufikiri ndio kitu pekee ambacho mtoto anatakiwa apandikizwe kwanza kabla ya yote.Hujui kuwa genes zinaweza kuwa modified na thimking process
Kufikiri ndio kitu ambacho mtoto aliyezaliwa leo anatakiwa aanzwe kufundishwa.
Watoto wetu wengi wakiwa wachanga tunawaacha kabisa hatuwapi ile shughuli ama hatuwafanyii mambo ambayo yatawafanya wao wafikirie zaidi.
Unaweza kujiuliza mtoto mdogo anafikiri ? Ndio anafikiria.
Mfano mtoto mchanaga wa wiki kadhaa unaweza kuchezesha mkono wako akawa anauona hivi unaenda huku na kule anaufuata kwa macho,hiko kitendo cha yeye kuuona mkono anafikiria ni kitu gani hiki bila kujua kama na yeye anao huo mkono,lakini ile kuufuatilia basi anajiuliza sana kwamba hiki ni nini ?
Sasa ilw kujiuliza hiki ni nini huko ndo kufikiri sasa,kuna mambo mengi ya kuwafanyia watoto ambayo nahisi wazazi wengi hawajashtuka.
Mtoto mchanga unatakiwa uwe chizi ukicheza nae,tafuta kila mchezo ambao utamfanya yeye awe bize kuutizama,hiyo inamtengenezea umakini na kufikiri tokea utoto wake...