Watoto wawili wauawa Nzega, ng’ombe zachukuliwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879

watoto pc


Tabora. Watoto wawili wenye umri wa miaka kumi na mbili wameuawa na miili yao kuzikwa ndani ya nyumba baada ya kurubuniwa na kuchukuliwa ng'ombe walizokuwa wanachunga.

Tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki eneo la Ndala wilayani Nzega usiku wa kuamkia jana Jumapili Julai 11, 2021.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Safia Jongo amesema watoto hao wote wa kiume walikuwa wanachunga ng'ombe saba na kurubuniwa na kijana mmoja ambaye aliwapeleka kwa bibi yake.

"Ilidhaniwa watoto hao pamoja na ng'ombe kuwa wamepotea na jitihada za wananchi na polisi kuzaa matunda,"amesema.

Kamanda Jongo ameeleza kuwa walipata taarifa za kijana aliyewarubuni watoto na walipochunguza kwa bibi yake alipowapeleka watoto hao, waligundua kuwa aliwaua kwa kuwachinja kama kuku na kuwafukia ndani ya nyumba.

Amesema tukio hilo ni la kikatili huku akieleza kuwa baadhi ya watu wa Tabora ni wakatili sana kwani watoto hao wasingeuawa bali hata kufungwa kwa kamba.

Mwananchi
 
Walioiba ngombe na walioiba wote ngombe tu. Huwezi kuua binadamu kwa ajili ya ng'ombe
 
Kuna jamaii zina ukatili sana na siajabu hao ngombe wakauzwa kila mmoja 150k. Mazingira ya wizi hayakua na ulazima wa kuwaua na ukitegemea ni watoto wadogo sana.
 
Hawa waandishi wa habari wanaandika Kiswahili gani, mbona mwandishi ni kama mtu anayejifunza kuandika.
 
Back
Top Bottom