Watoto wanasoma, dingi nasoma, nakomaje!

ndyoko

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
4,971
Reaction score
1,655
Hakika usiombe ukutane na haya masaibu ninakutana nayo sasa.
Huku kusoma uzeeni nako noma kweli.

Jamani wale watoto walokuwa wanagomba kila siku wamekuwa na
kwa sasa wanasoma....ila hawjaacha kuendelea kuchapana ila
walu kwa sasa wako bize kidogo na shule, nikuiona wanaanza
kuleteana mizengwe nawajazia home work wanakuwa bize fujo zinapungua.

Mwaka jana nami niliamua kwenda shule ila si mnajua shule za uzeeni, jioni
unarudi nyumbani unafanya 'assignment zako' na wao wako bize na 'home work'.
Kero niliyonayo ni mtinodo walionao wa kuchua 'stationeries' zangu. leo ukija na obama pen, nao
wanataka, ukija na executive pen, wanataka pia. Kuna wakati nikaanza kuwa
mnoko.......weeeeeeeeeeeeeee! Kelele za kuombwa zikapotea ghafla ila kituko ni
kwamba hizo 'stationeries' sasa zikawa zinapotea bila kujua zinaenda wapi
utadhani labda kuna jini ndani.

Siku nikaamua tu kufanya msako kwenye mabegi yao ya shule......nikagundua
kumbe 'stationeries' zangu zilikuwa zinapotelea kwenye mabegi ya hawa
wanafunzi wa kizazi cha dot.com cha english medium. Nilichofanya ni kukusanya
vyote vilivyo vyangu na kuviweka mezani ili wajue nimegundua vitu vyangu vinakoendaga.

Leo siku ya pili naona vimeanza kupungua tena nahisi wameanza tena 'kuniazima'
vitu vyangu ingawa nao wanavyo.....Jamani hebu nisaidieni kwanini hawa watoto
wako 'very possessive' na stationeries zangu wakati wao pia wanavyo kama hivyo?

Kids wanaboa sometime, class mwalimu anaona mi kilaza au pengine nina jeuri ya
uzeeni, nyumbani nakatwa stimu kufanya 'assignment zangu'.

Oooooooooh, nakomaje mwenzenu na hii shule ya uzeeni!
 
Nikajua utatoa comment zako zile za kushoto nimekujaje fastaaaa! Kumbe upo kwaresma! Kuna mtu kacomment KANIKOSHA MNO MNO MNO KITU CHA NOW OPEN! Nacheka tu kwa raha zangu! Mbavu zaniuma.
 
Nunua mi dozen ya hzo stationaries,afu uzigawanye kwa kila mtu anasesoma hapo kwako,afu usikilizie kama watakuchukulia vifaa vyako..pole sana
 
Yaani watoto ni wako, wewe mwenyewe! Unakatika stimu kwa sababu wanachukua obama pen zako? Hebu toka hapa. Ukinunua vitu ujue una wasomi wangapi, ukifika home weka mezani mgawane kabisaa kila mtu aruke na vyake. Tena kuzuia ukware, kila mtu aandike jina kwenye kikaratasi adumbukize kwenye kalamu yako for easy identification.

soma ufaulu, acha visingizio! Na kusoma uzeeni ndo mpango mzima, komaa.
 
Komaa kusoma uzeen yahitaji moyo.....
Mnunulie kila mtu chake ikifika home mnagawama kila mtu afe na chake ..
 
DAAAAAAAAAH!!!!....
mathematical_set_compass_28_60109.jpg
 
Nikajua utatoa comment zako zile za kushoto nimekujaje fastaaaa! Kumbe upo kwaresma! Kuna mtu kacomment KANIKOSHA MNO MNO MNO KITU CHA NOW OPEN! Nacheka tu kwa raha zangu! Mbavu zaniuma.

Hahahah lara1....umenfanya ni smile,.
 
hahahahahaaa mandyoko pole, mie hapa najiuliza siku nikirudi shule kuanza kusoma tena sijui itakuweje na vurugu ya watoto home. Ninachofanya sasa ni kuwajengea tabia ya kujisomea kila mtu kufanya homework yake kama hana asome kitabu cha nyumbani ambacho kila mtu nimemnunulia na wakichoka kila mtu kucheza hivo inapunguza muda wa kugombana na ukorofi. Sometimes watoto raha ila kuna muda unahitaji kuwa home bila kusikia wakiita mama u baba....
Ndo uzazi na ulezi huo furahia matunda ya viuno vyako heheheheheheee wakikua siku wanaoa uwasimulie yote hayo au siku wanagraduate chuo uwasimulie yote hayo watachekaaaa
 
Yaani watoto ni wako, wewe mwenyewe! Unakatika stimu kwa sababu wanachukua obama pen zako? Hebu toka hapa. Ukinunua vitu ujue una wasomi wangapi, ukifika home weka mezani mgawane kabisaa kila mtu aruke na vyake. Tena kuzuia ukware, kila mtu aandike jina kwenye kikaratasi adumbukize kwenye kalamu yako for easy identification.

soma ufaulu, acha visingizio! Na kusoma uzeeni ndo mpango mzima, komaa.

Hahahahahaaa. Leo lazima kuna kitu sio bure, ila angalia ntakuja kuikata hiyo milonjo, shauri yako. hata hivyo hiyo ya kutumbukiza jina kwa ndani ya peni umenikumbusha mbali sana. nakumbuka ili kuepusha shari kwa kina dada tuliokuwa tunawaibia pen zao primary school wakawa wanaweka vikaratasi vyenye majina. We boys tukawaambia isiwe taabu. tukaja na plan B ambayi ilikuwa ni kunyonya wino..........aisee umenikumbusha zamani sana, miaka ya 1980s, mweeee!
 
Hakika usiombe ukutane na haya masaibu ninakutana nayo sasa.
Huku kusoma uzeeni nako noma kweli.

Jamani wale watoto walokuwa wanagomba kila siku wamekuwa na
kwa sasa wanasoma....ila hawjaacha kuendelea kuchapana ila
walu kwa sasa wako bize kidogo na shule, nikuiona wanaanza
kuleteana mizengwe nawajazia home work wanakuwa bize fujo zinapungua.

Mwaka jana nami niliamua kwenda shule ila si mnajua shule za uzeeni, jioni
unarudi nyumbani unafanya 'assignment zako' na wao wako bize na 'home work'.
Kero niliyonayo ni mtinodo walionao wa kuchua 'stationeries' zangu. leo ukija na obama pen, nao
wanataka, ukija na executive pen, wanataka pia. Kuna wakati nikaanza kuwa
mnoko.......weeeeeeeeeeeeeee! Kelele za kuombwa zikapotea ghafla ila kituko ni
kwamba hizo 'stationeries' sasa zikawa zinapotea bila kujua zinaenda wapi
utadhani labda kuna jini ndani.

Siku nikaamua tu kufanya msako kwenye mabegi yao ya shule......nikagundua
kumbe 'stationeries' zangu zilikuwa zinapotelea kwenye mabegi ya hawa
wanafunzi wa kizazi cha dot.com cha english medium. Nilichofanya ni kukusanya
vyote vilivyo vyangu na kuviweka mezani ili wajue nimegundua vitu vyangu vinakoendaga.

Leo siku ya pili naona vimeanza kupungua tena nahisi wameanza tena 'kuniazima'
vitu vyangu ingawa nao wanavyo.....Jamani hebu nisaidieni kwanini hawa watoto
wako 'very possessive' na stationeries zangu wakati wao pia wanavyo kama hivyo?

Kids wanaboa sometime, class mwalimu anaona mi kilaza au pengine nina jeuri ya
uzeeni, nyumbani nakatwa stimu kufanya 'assignment zangu'.

Oooooooooh, nakomaje mwenzenu na hii shule ya uzeeni!
You are missed
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom