Watoto wana haki ya kusikilizwa (i)

Watoto wana haki ya kusikilizwa (i)

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Posts
3,811
Reaction score
1,607
Baba alikuwa anamwambia mtoto wake "si ruhusa kusema wakati tunakula, hasa tukiwa na wageni".
Siku moja walipata mgeni, wakati wa kula mtoto akaanza "Baba..."
Jicho alilomtolea mwanawe lilitosha kuwa onyo.
Baada ya muda, "Baba..."
Baba kasoro amzabe kibao.
Dakika moja baadae, "Baba...."
"Shhhhhhhhhhhhhhh", baba ustahamilivu ulimwishia.
Baada ya mgeni kuondoka, "Si ninakwambia siku zote wakati wa kula usiseme? Enhe! Ulikuwa unasemaje?
Samahani baba, haina maana tena, nilitaka kukwambia tu kuwa mbele ya sahani yako palikuwa na mende".
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom