Mfahamu Pata Seca: Kutoka kuwa Mbebesha Mimba mpaka Alama ya Ukombozi

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,590
2,088
Habarini Wanajukwaa!

Uzalishaji wa watumwa ulikuwa ni jambo la kawaida sana kutokea haswa kuanzia miaka ya 1619, jambo hili lililotokea huko Marekani, ambapo wamiliki wa watumwa wangezalisha Waafrika waliokuwa watumwa kwa madhumuni ya kuongeza thamani yao ya kiuchumi kama sehemu ya utendaji wa kazi. Kitendo hiki kilikuwa na athari kubwa kwa jamii ya watu weusi, kwani kilisaidia kuendeleza taasisi ya utumwa na kuendeleza dhana kwamba watu weusi walikuwa duni na wasio wa chembe za kibinadamu.

1702378785556.png


Miaka michache iliyofuata marufuku ya uingizaji wa watumwa nchini Marekani ilikuwa enzi ya kilimo cha watumwa. Baada ya 1808, kazi ya utumwa na watumwa walikuwa ni bidhaa adimu nchini Marekani. Hiki kilikuwa ni kipindi ambacho kilitangaza kuporomoka kwa biashara yenye faida kubwa ambapo hisa zilizouzwa zilikuwa ni wanadamu (waafrika) ambao maisha yao yalikuwa ya kuharibika kama majani ya mti kwa msimu wa vuli.

1702378858864.png


Lakini wamiliki wa watumwa walikuwa wafanyabiashara wazuri tena wenye ushawishi mkubwa, watu kama Isaac Franklin pamoja na John Armfield walijua kuwa hakuna biashara inayosalia na mipaka imefungwa kwa vifaa, hivyo walielekeza nguvu zao kwenye biashara hii. Wafanyabiashara hawa watumwa walifanya kile ambacho kila mfanyabiashara mzuri angefanya, walipata njia mbadala ya ugavi - uzalishaji wa watumwa zaidi ili kupata nguvu kazi na bidhaa kwa ajili ya biashara.

1702378956684.png

Isaac Franklin

Usikutane na kaka wawili, Jordan Arterburn pamoja na Tarlton Arterburn walikuwa na roho za kipuuzi sana kiasi kwamba mtumwa hakwepi kuuzika, Aaron Forrest na hata John Crenshaw wote hawa na wenzao walikuwa wakifanya biashara hii bila uonga wowote.

1702379123268.png

Pata Seca, alizaliwa huko Sorocaba, São Paulo, sambamba na wanadada Mariana Morais pamoja na Júlia Mende kutoka mji wa Instagram.
1702379734229.png

Jina lake halisi ni Roque José Florêncio ila alipokuwa utumwani alipatiwa jina la Pata Seca, Bwana Pata alizaliwa Brazil mwaka 1828 huku tarehe na mwezi husika ikiwa ni ngumu kufahamu haswa. Pata Seca ani mmoja ya watu wenye mchango mkubwa sana katika harakati za kupigania utumwa.

Mwanaume mmoja mwenye umbo kubwa na urefu wa 7’2″, yaani alikuwa na urefu zaidi ya Shaquille O'Neal, Pata Seca aikuwa na urefu sawa sawa na Kareem Abdul-Jabbar, watu kama Dirk Nowitzki, Wilt Chamberlain, ama Pau Gasol wote walikuwa ni wafupi kwa mwamba huyu ambaye alikuwa na kilo zaidi ya 136.
1702379153161.png

Kazi aliyopewa Pata Seca akiwa utumwani ilikuwa sio kufanya kazi nzito, ei kubeba mawe, au kukata miti ama kuchima mashimo makubwa kwa ajili ya kufukia taka, bali Pata Seca alipewa jukumu moja tu, alitakiwa kulala na watumwa wa kike na kuwabebesha mimba ili wapate kuzaa Watoto wenye vinasaba kama vyake, yaani Watoto wenye ushupavu kama baba yao. Maumbile yak endo yalimpa alama nyingi sana mbele ya watumwa wengi, kwa sasa wanawake wangesema kuwa Pata Seca alikuwa Mwanaume mashine.
1702379206242.png

Kitu mbaya ni kuwa Pata Seca alikuwa akiishi maagizo ya mmliki wake, na alitakiwa kutii maagizo ya kuzalisha kadri mmliki anavyotaka, kitu pekee yeye ni kula mzigo tu. Pata Seca alipata kipaumbele kuliko watumwa wote, alipatiwa chakula kizuri cha kujenga mwili, matibabu na pia alichunguzwa afya yake na endapo akikutwa na ugonjwa basi anatibiwa chap ili baadaye kazi iendelee.

Wanadhiri wawili Prof. John Ashworth pamoja na Dr. Jane-Marie Collins kutoka Chuo Kikuu cha Nottingham walionesha kuwa Pata Seca alikuwa akionekana kama mashine ya uzazi, kwani wanawake wote watumwa hawakupaswa kubeba mimba kutoka kwa mwanaume mwingine zaidi ya Pata Seca, na punde tu wanawake wakipata hedhi basi mwanaume Pata Seca anaandaliwa kwa ajili ya kuongeza nguvu kazi kupitia kizazi chake. Pata Seca alipatiwa hakimiliki ya shamba kutoka kwa mmiliki wake mara baada ya kutomeshwa kwa utumwa mwaka 1888 nchini Brazili.
1702379282771.png

Baada ya kupata uhuru wake, Pata Seca alipata upendo na urafiki kwa mwanamke anayeitwa Palmira, ambaye alimuoa, wawili hawa waliishi pamoja na walipata baraka ya watoto tisa, na kutengeneza msingi wa familia yao wenyewe, waliishi kwenye ardhi aliyopewa na bwana wake wa zamani, Pata Seca alijitolea kujenga maisha mapya kwa familia yake.

Walakini, maisha ya Pata Seca hayakuwa marefu kama Watoto wake kwani alipata maambukizi ya ugonjwa wa pepopunda ama kwa lugha tuliyozoea tetanus mara baada ya kukanyaga msumari kwa bahati mbaya. Jeraha hili lilitosha kumpatia ugonjwa wa pepopunda, mnadhiri Emmanuel K. Akyeampong kutoka Chuo Kikuu cha Havard Idara ya Historia, alidai kuwa hali ya Pata Seca ilikuwa ambaya kutokana na kukosa huduma sahihi kutoka kwa wataalamu wa afya, kwani walimpeleka kwa mganga wa jadi. Tarehe 13 Juni 1958 Pata Seca alifariki akiwa na miaka 130 huku akiw ana watoto zaidi ya 200.

Pata Sec ani alama ya upiganiaji wa utumwa kwani alikuwa mstari wa mbele kusaidia sana watumwa kukimbia na kuwapeleka kwenye sehemu salama ambazo walizipatia majina ya quilombos. Pia Maisha yake ni ukumbusho tosha wenye huzuni na mateso makubwa wakati wa utumwa ndani ya nchi ya Brazili
1702379501368.png

Ukiachilia mbali kufanya kazi ya kubebesha mimba wanawake tu, pia Pata Seca alitumia nafasi yake kama baba kuwafundisha lugha Watoto wake, pia kusoma na kuandika lakini kubwa zaidi ni kuhusu mila na desturi za mtu mweusi.
1702379545417.png

Mji wa Santa Eudoxis Sao Carlos uliopo Brazili unadaiwa kuwa 30% ya wakazi wa eneo hili wanaonekana wana vinasaba kutoka kwa bwana mkubwa Pata Seca, sasa wakazi 254,484 hapo fahamu kuwa kuna watu zaidi ya 76345 ni sehemu ya uzao wa Pata Seca.

Rest Easy Papa Pata Seca! Rest Easy Roque José Florêncio!​
 
Asante sana mleta mada , kuna vitu vingi sana ambavyo hatuvifahamu , tunapopata bahati ya kujua kutoka kwa wanao jua wanaposhirikisha kile wanachokifahamu ili wasiofahamu wafahamu hatuna budi kurudisha shukurani, asante tena mleta mada.
 
Asante sana mleta mada , kuna vitu vingi sana ambavyo hatuvifahamu , tunapopata bahati ya kujua kutoka kwa wanao jua wanaposhirikisha kile wanachokifahamu ili wasiofahamu wafahamu hatuna budi kurudisha shukurani, asante tena mleta mada.
Tuendelee kujifunza kila wakati Mkuu
 
Back
Top Bottom