Makonda ametangaza kuwa watoto wote wa Dar waliotelekezwa na kwenda kwake watalipiwa Bima ya afya na ofisi yake.
Ni jambo jema, lakini ni vyema basi serikali iwe na uwazi na kusema fedha hizo ni za fungu gani au zinatoka wapi?
Sio jambo jema kusikia kama yale kuwa ofisi za Bakwata zinajengwa na fedha za Mkoa kisha Habari zinazagaa kuwa ukweli ni kwamba GSM ndio wafadhili wa mradi huo.
Hii ni namna Mpya ya corruption ambayo imeingia nchini ambayo tumekuwa tunasikia nchi kama Italy, Hispania, Israel nk wakuu wao walijikuta wakiingia kwenye kashfa ya rushwa kwa kukosa uwazi.