Watoto waliotelekezwa kupatiwa bima ya afya

Watoto waliotelekezwa kupatiwa bima ya afya

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,610
Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wanawake waliotelekezwa na waume zao watakaofika katika ofisi yake iliyopo Ilala jijini hapa kuanzia kesho Alhamisi Aprili 12, 2018, watoto wao watapatiwa bima ya afya.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Aprili 11, 2018 wakati akizungumza na wanawake waliojitokeza kupata huduma ya kisheria na kusisitiza kuwa utaratibu huo utakuwa endelevu hadi wanawake wote wenye madai yao watakaposikilizwa.

"Serikali ikiwa inafanya utaratibu wa kuwasaidia watoto waliotelekezwa yupo mtu aliyeguswa, kuanzia kesho watakaokuja kupata huduma watakatiwa bima ya afya " amesema Makonda.

Amebainisha kuwa wapo wanaume waliopelekewa wito na kutakiwa kufika katika ofisi hizo, lakini wamekaidi na kusisitiza kuwa wote waliokataa watakamatwa.

“Wapo watu wanaopelekewa barua na kukaidi. Utaratibu tunaoutumia ni wa kawaida ikiwemo kupelekewa barua na kupigiwa simu. Atakayekaidi nitaenda kumkamata," amesema Makonda.

Mmoja wa wanasheria waliopo katika eneo hilo ameieleza MCL Digital kwamba idadi ya watoto hao ni 5,000 kutokana na idadi ya wazazi waliopatiwa kadi na kutakiwa kufika katika ofisi za mkuu wa mkoa kuanzia kesho na Ijumaa.

Chanzo: Mwananchi
 
Siasa nyepesi. Waliotelekezwa na mayatima na wapi wahitaji zaidi? Au kwa sababu mayatima hawana wazazi ambao wangekuwa mtaji kwa chama so hawana maana? Aite na mayatima aone kama Ilala patatosha kuwaweka.
 
Wafafanue hizo bima za afya ni kwa watoto wa umri gani? Kwani nini kusiwe na utaratibu wa matibabu bure kwa watoto? Je, zitalipiwa na nani? Why watoto waliotelekezwa; kwani hakuna watoto wenye mazingira magumu wenye wazazi na wanahitaji huduma hii???🙁🙁🙁🙁🙁🙁
Wanatuchanganya tu.......
 
Unawakamata je kama wamesingiziwa
Wanasema usikatae wito, kataa neno.
Ukiitwa kama una muda nenda, hayo ya kusingiziana utayasema ukifika.
Ila kama huna muda ni sawa tu kutokwenda, sababu hapa bongo kila mtu na ratiba zake za maisha. Sio lazima uende kwa muda ulioitwa, panga wewe muda wako ambao una nafasi uwaambie.
 
Anaangaika na watu ambao wana uwezo wakuwahudumia watoto wao ... Hakumbuki kuwa kuna watoto ambao wapo mitaan hawana baba wala mama (yatima) nao wanahtaj msaada mkubwa zaid.
 
Unikamate simply nimetuhumiwa na malaya wa kona bar, anawaamini vipi hao wanawake.
 
Unawakamata je kama wamesingiziwa
Mkuu ,muwe mnaelewa Kilichosemwa kabla ya kukoment.
Wametajwa, wanatakiwa kuitikia wito, wafike watoe maelezo kwamba hawahuski.
Kukataa kwenda ni kosa ki sheria, tayari hizo ni tuhuma ,Nakuhakikishia atakae kaidi atakamatwa tu, labda ajifiche, huwezi zuia dola kufanya kazi
 
Wafafanue hizo bima za afya ni kwa watoto wa umri gani? Kwani nini kusiwe na utaratibu wa matibabu bure kwa watoto? Je, zitalipiwa na nani? Why watoto waliotelekezwa; kwani hakuna watoto wenye mazingira magumu wenye wazazi na wanahitaji huduma hii???🙁🙁🙁🙁🙁🙁
Wanatuchanganya tu.......
Mlikua wapi kabla hili halijaibuliwa?, acheni unafiki, kama unampango kazi Weka hadharani watu waufanyie kazi, tumechoshwa na mazalia ya panya road
 
Mlikua wapi kabla hili halijaibuliwa?, acheni unafiki, kama unampango kazi Weka hadharani watu waufanyie kazi, tumechoshwa na mazalia ya panya road

Kabla hujamquote mtu hakikisha umesoma na kukielewa alichoandika la sivyo utaandika utumbo kwa kumjibu tofauti na alivyomaanisha.
 
Jamani tumieni Condom au withdrawal method au piga uani ili mimba isipatikane.. Piga mashine uani maana mimba ikipatikana ndio matatizo yote haya huanza.. Ruka ukuta au tumia Condom, maana tatizo sio starehe tatizo ni mtoto akizaliwa. Acheni kufanya ngono zembe bila kufikiri hata kidogo kama kuku
 
Ukinifuata na kunisisitiza kuwa unataka kunisaidia ukaona siitikii wito then ukaniwekea chambo/motisha(bima) ili unisaidie lazima nitafakari mara mbili?Hii Bima mbona sikuisikia tangia mwanzoni?

Hivi utaratibu wa kupata BIMA ya afya ukoje?
 
Makonda ametangaza kuwa watoto wote wa Dar waliotelekezwa na kwenda kwake watalipiwa Bima ya afya na ofisi yake.
Ni jambo jema, lakini ni vyema basi serikali iwe na uwazi na kusema fedha hizo ni za fungu gani au zinatoka wapi?
Sio jambo jema kusikia kama yale kuwa ofisi za Bakwata zinajengwa na fedha za Mkoa kisha Habari zinazagaa kuwa ukweli ni kwamba GSM ndio wafadhili wa mradi huo.
Hii ni namna Mpya ya corruption ambayo imeingia nchini ambayo tumekuwa tunasikia nchi kama Italy, Hispania, Israel nk wakuu wao walijikuta wakiingia kwenye kashfa ya rushwa kwa kukosa uwazi.
 
Back
Top Bottom