Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 943
- 4,458
Chama cha mapinduzi baada ya kuona siasa zinazalisha viongozi shupavu kutoka vyuoni kilikuja na mbinu yakukataa siasa kwa wanafunzi wa vyuo. Ili watimize lengo lao wakapiga marufuku siasa wakishirikiana na wakuu wa vyuo na maprofesa na madaktari waliosimamia Katazo hili wakapewa uteuzi.
Leo chuo kikuu cha DSM hakuna mwamko wa fikra kwa sababu siasa za vyuo zilijikita katika makongamano na midahalo ya wazi ukitumika sana ukumbi wa Chuo kujadili hoja.
Ilifika wakati hata wanasiasa wakubwa wakitaka kujadili hoja muhimu wanakwenda kutumia kumbi za vyuo na hivyo kutoa fursa ya kuulizwa maswali na wanafunzi. Leo hii vyuo vimekuwa kama primary school
Chuo cha SAUT mwanza wakati wa Padre Kitima mjadala wa kupata viongozi ulikuwa mkubwa; wanafunzi wake hata ukiwaona leo unaona upeo mkubwa wa maarifa. Leo hii SAUT wanafundishwa kukariri siasa za nje kuliko kujadili maisha halisi ya mtanzania
Kinachosikitisha ni kuruhusiwa kwa watoto wadogo ambao baba zao ni mawaziri na maraisi kufanya siasa za majukwaani lakini watoto wa wengine ni marufuku. Leo watoto wa Kikwete , Mwigulu nk wapo majukwaani wanapiga kampeni za baba zao. Hakuna anayekataza na wizara ya elimu hakuna Sehemu imekemea.
Tunadhani kuwaandaa watoto wetu kwa kuwakataza watoto wengine kufanya siasa ni sahihi? Huu ubaguzi unaofanywa na awamu ya sita unalenga kulijenga Taifa au kulibomoa?