Watoto wa vigogo waiteka UVCCM!

Ndio tumeshachaguliwa kelele mtapiga tu lakini sisi tutaendea kuwa juu jamani mwenye nacho huongezewa.

Sawa ndugu hongereni sana kwa kuchaguliwa ili kuendelea kula mema ya nchi ila kumbuka,HAKUNA IDUMUYO KAMA MILIMA YA SAYUNI.
 
HATARI!Angalia jinsi watoto wa Vigogo walivyopeta UVCCM .DICKSON MEMBE,FREDY LOWASSA,RIDHIWANI KIKWETE,ASHURA HUSSEIN MWINYI,BENNY SAMWEL SITTA,DEBORAH MWANDOSYA,IRENE PINDA,FELISTER NDUGAI,CHRISTOPHER NDEJEMBI,SHARRIFA BILLALY,HAWA KIGODA,JUDITH MUKAMA,NA JALOME MSEKWA.Nchi hii Imekwisha,inatia hasira,TUSIPOKUWA MAKINI TUTAENDELEA KUTAWALIWA HADI WAJUKUU ZETU.HIVI WATANZANIA TUNAELEKEA WAPI?
kwani hao ni wakuteuliwa? si mnawachagua wenyewe? kama mnawapigia kura mnadhani wakatae sababu tu ni watoto wa vigogo? tuwe serious jamani
 
yale yale ya syria kurirthishana urais madhara yake ndio hayo
Kongo nako hadi leo hakuna amani.
Uganda nako sio shwari(mwanae musseni na mkewe-vyeo vya kupewa
Tanzania tuanelekea kubaya kwa stahili hii CCM wanajimaliza wenyewe
 
Tatizo lako nini mkuu na wewe si ugombee huko Uvccm??
Kama na wewe unataka

Mkuu usiogope kufikiri, akili ni yako, umepewa uitumie, wala hujaiazima ya kuwa utadaiwa uirudishe kwa mwenyewe,
Hii nchi ni yetu sote si ya kikundi fulani au ukoo fulani,Mwalimu hakutufundisha hivyo,vinginevyo leo hii watoto wake wote wangekuwa vigogo.
 
Tuongee ki uhasilia kama ungelikuwa ww utaacha mwanao ateseke?.kwani kuna mtu anayependa mwanae apate shida?.
 
Jamani hivi tunaelekea wapi kama baba yako si kiongozi inamaa hakuna chako hata kwenye maofisi hivyo hivyo huna baba au ndungu hakuna chako sasa akili kichwani kwako 2o15
 
kwani hao ni wakuteuliwa? si mnawachagua wenyewe? kama mnawapigia kura mnadhani wakatae sababu tu ni watoto wa vigogo? tuwe serious jamani
Kumbuka kwamba fedha zilizofisadiwa za walipa kodi ndizo zilizotumika kuhonga ili kupata nafasi hizo. Si jambo la kujivunia na kuwakejeli maskini mliyowahonga wanaoishi chini ya $2 kwa siku.Jeuri na kiburi huponza.
 
Kumbuka kwamba fedha zilizofisadiwa za walipa kodi ndizo zilizotumika kuhonga ili kupata nafasi hizo. Si jambo la kujivunia na kuwakejeli maskini mliyowahonga wanaoishi chini ya $2 kwa siku.Jeuri na kiburi huponza.
mimi huwa nashangaa sana, huko kwenye vikao sipo. lakini kwani kura siyo siri ya mtu? kwani nikipewa hongo ni lazima nimchague mtu hata kama hafai?
 
No hii ni nzuri sana acha walundikane hukohuko ili CCM itakapopigwa chini 2015 wawe sandwitched hukohuko kwa hiyo 2015 itawaeliminate ccm, na kizazi chake chote, kuliko kwa mfano wangesambaa vyama vingine ingeweweza kuwa vigumu kuwa eliminate!
 
Inawezekana hata vijukuu vyao ambavyo havijazaliwa tayari vimetengewa nafasi tayari!


Sioni ajabu hata kido kwa sababu hata mimi nikitaka nafasi ya naipata tu. Ukiangalia waliopata uongozi chamani ambao sio watoto wa vigogo ni wengi zaidi kuliko hata watoto wa vigogo. Hata pale tunapolalamika CDM ni chama cha watu fulani wakati tumekunja mikono hatatuki kujiunga ni upuuzi wetu wenyewe, CDM wala CCM hawafukuzi watu kujiunga nao ila tumekuwa wa kulalamikia hata mambo yasiyo ya maana. Mtoto wa mwanasiasa kuwa mwanasiasa ni rahisi zaidi. Kuna mwl mmoja wa sheria yupo Moshi kaandika vitabu na mtoto wake, je nalo ni kosa? Watoto wa mawakili kuwa mawakili ni kosa? Tukumbuke watoto wa wanasiasa wanaona kila kinachoendelea kuhusu siasa unategemea wafanye kazi gani kama sio hiyo ya siasa wanayoiona? USA, Bush alimwachia mtoto, Clinton kdg amwachie mke wake, na akina Kenedy n.k kuna ubaya gani kwetu? tena hawajawania hata uraisi (ukiacha kwa Zenji). Jamani hizi hoja zingine tuwe tunafikiri kwanza kabla ya kuzileta. Mwenyewe ukiwa mkurugenzi wa kampuni yake inayofanya vema nadhani unaweza tamani mtoto wako pia aje awe mkurugunzi hapo na ama aipaishe zaidi kampuni yako. Tuwe na fikra kubwa tusifikiri vitu kiurahisi na kupiga kelele tu, tuingie baharini tuogelee tusikae kuangalia wengine wanaogelea ilihali nasi twatamani kuogelea. Hata maandalizi ya kuvaa life jacket ama kuvua nguo hatujafanya, ajabu sana!
 
Wakuu, Ni kweli ujumbe huu umesambaa sana kwenye simu, Sijui lengo kuu la ujumbe huu ni nini? Tuache kutumia mitandao ya kijamii kujenga hasira kwa watu. Hii ni hatari kwani mwisho wa siku, si mimi wala wewe, hatutacheka. Kila mtu atalia. Tutumie hoja za kujenga nchi kuliko hoja za kubomoa

kwa hiyo wewe unaona watoto kutumia fedha za baba zao viongozi(ambazo nyingi ni za kifisadi) na majina ya baba zao(ambao wengi sio waadilifu) kupata uongozi sio swala lla kitaifa wala sio hoja ya msingi? Ridhiwani na mama Salma kupita bila kupingwa ni sawa tu kwako??lengo la ujumbe ni kukutaka wewe na wengine wa aina yako mliolala muamke mjue kuwa nchi yetu sasa indirectly inaongozwa kifalme, na kama huna ndugu(mama au baba mume au mke) mwenye jina kubwa kisiasa kamwe huwezi kupata uongozi, this very serious issue!
 
Jamani habari hizi za kweli???? sijielewi

HATARI! Angalia, Watoto wa vigogo waliopita UVCCMngazi ya taifa; DICKSON MEMBE, FREDY LOWASA, RIDHIWANI KIKWETE,

ASHURA HUSSEIN MWINYI, BENY SAMWEL SITA, DEBORA MWANDOSYA,IRENE PINDA, FELSTER NDUGAI, CHRISTOPHER

NDEJEMBI, SHARIFA BILALY, HAWA KIGODA, JUDITH MUKAMA NAJEROME MSEKWA. Nchi hii imekwisha. Inatia hasira, wacha

watoto wa maskini tupambane kupitia mlango mwingine‘’CHADEMA’’ ili kutetea maskini wanzetu, wazazi na wadogo zetu! Vita hii

inaanza sasa!, Upatapo meseji hii, tuma kwa WAZALENDO wenzako.

 
Back
Top Bottom