Watoto wa vigogo waiteka UVCCM!

Watoto wa vigogo waiteka UVCCM!

dah! wanataka kutuaminisha kwamba waliwaandaa watoto wao waje kuwa watawala kama wao au hizo nafasi sasa wameamua kuendeleza kale ka utaratibu ka kupeana nyuma ya mgongo wa uchaguzi
 
Mbna hawaendi kwenye ualimu, upolisi wote ni siasa tu na wakiingia huko wao hawakosi nafasi
 
Ujanga wa Kitaifa ndiyo imeifanya message zote kutufikia!

Mi tangu juzi nazipata!
 
nimetumiwa sms tatu zote zina maneno yanayofanana,maneno hayo yanahusu uteuzi wa watoto wa vigogo wa ccm kuteuliwa kugombea nec.je una sambazwa na nani?

hizo msg ungeziandika hapa watu wakuelewe...............
 
watz tubadilike cyo kila kitu kipo ccm, hebu tugeukie upande wa pili wa shilingi, cdm!
 
HATARI!

Angalia, watoto wa vigogo waliopita UVCCM Ngazi ya taifa.

1. DICKSON MEMBE
2. FREDY LOWASA
3. RIDHIWANI KIKWETE
4. ASHURA HUSSEIN MWINYI
5. BEN SAMWEL SITTA
6. DEBORA MWANDOSYA
7. IRENE PINDA
8. FELISTER NDUGAI
9. CHRISTOPHER NDEJEMBI
10. SHARIFA BILAL
11. HAWA KIGODA
12. JUDITH MUKAMA
13. JALOME MSEKWA
n.k
ndiyo sura halisi ya ccm
 
Sioni tabu ya hawa watoto kugombea nafasi yeyote ndani na nje ya vyama vyao nao ni watanzania wenye haki sawa na mtanzania mwingine tusiwanyanyapae kwa sababu tu baba zao ni vigogo au mashuhuri au wanasiasa. Tuangalie je uchaguzi ulikuwa huru na haki. Je wazazi wao walilazimisha wao kushinda au walishinda kwenye mfumo huru??

Na sisi watoto wa akina pangu pakavu tusibweteke na kujiona wanyonge kwa kila kitu, jazeni form kwenye mifumo hii ya kisiasa serikali taasisi mbali mbali mshiriki badala ya kukaa pembeni na kupiga mayowe. Ninaushahidi wa kutosha kwamba watanzania wengi wanapenda kulalamika sana bila kushiriki. Sasa kama ninyi hamtaki kushiriki kwenye hizo chaguzi mnategemea nini?? Vigogo wanajitengenza na kazi ni kugombea tu. Ni vyema tukapigia kelele rushwa na kupendelea kuliko kuwawanyapapa hawa wototo kwa sababu tu baba zao wanamajina, wengine masikini zaidi ya majina ya baba zao choka mbaya.

Tushiriki kwenye mfumo wetu ili tuwe na kesi
Chief Mkwawa wa Karenga
No spinning
Chukua hatua madhubuti, tetea haki, wajibika, shiriki, kulalamika hakubadilishi nchi.
 
acha kutetea vitu vilivyowazi, mchakato huru ni maneno ya kisiasa kuwabosheni watanzania, hivi unategemea kuna mtu ataweza kumchallenge riz1 hata km baba yake hajasema kitu? hiyo ndiyo tabia na sura halisi ya ccm kwa ngazi zote, mimi mwenyewe binafsi hilo suala limenikuta ccm nilijaribu kugombea ngazi ya chini uenyekiti UVCCM tawi, lakini mwenyekiti wa tawi akamuweka mtoto wake na kuniangusha kwa hila za kiunyekiti.
 
HATARI!

Angalia, watoto wa vigogo waliopita UVCCM Ngazi ya taifa.

1. DICKSON MEMBE
2. FREDY LOWASA
3. RIDHIWANI KIKWETE
4. ASHURA HUSSEIN MWINYI
5. BEN SAMWEL SITTA
6. DEBORA MWANDOSYA
7. IRENE PINDA
8. FELISTER NDUGAI
9. CHRISTOPHER NDEJEMBI
10. SHARIFA BILAL
11. HAWA KIGODA
12. JUDITH MUKAMA
13. JALOME MSEKWA
n.k
Chama cha magamba kina wenyewe na wenyewe hao ndiyo waliorodheshwa hapo juu.
 
Acheni wivu ni haki yako ya kichama kaulizeni viwanja vya mradi gezaulole nani walipewa vipaumbele na sasa hivi nikita uongozi nataja ukoo wa kigogo yoyote lili nami nitoke! Hahahal T taznzania
 
acha kutetea vitu vilivyowazi, mchakato huru ni maneno ya kisiasa kuwabosheni watanzania, hivi unategemea kuna mtu ataweza kumchallenge riz1 hata km baba yake hajasema kitu? hiyo ndiyo tabia na sura halisi ya ccm kwa ngazi zote, mimi mwenyewe binafsi hilo suala limenikuta ccm nilijaribu kugombea ngazi ya chini uenyekiti UVCCM tawi, lakini mwenyekiti wa tawi akamuweka mtoto wake na kuniangusha kwa hila za kiunyekiti.

Uligombea CCM kwasababu ulikubaliana na mfumo wa CCM. Ukikubali mfumo lazima ukubali matokeo. Wengi tunaamini mfumo wa CCM haufai na chama kimeoza kwa rushwa za aina zote.
 
HATARI!Angalia jinsi watoto wa Vigogo walivyopeta UVCCM .DICKSON MEMBE,FREDY LOWASSA,RIDHIWANI KIKWETE,ASHURA HUSSEIN MWINYI,BENNY SAMWEL SITTA,DEBORAH MWANDOSYA,IRENE PINDA,FELISTER NDUGAI,CHRISTOPHER NDEJEMBI,SHARRIFA BILLALY,HAWA KIGODA,JUDITH MUKAMA,NA JALOME MSEKWA.Nchi hii Imekwisha,inatia hasira,TUSIPOKUWA MAKINI TUTAENDELEA KUTAWALIWA HADI WAJUKUU ZETU.HIVI WATANZANIA TUNAELEKEA WAPI?
 
Wakuu,huu ujumbe umesambazwa kwenye simu mimi binafisi nimetumiwa zaidi ya mara 5 na watu tofauti.ccm ni janga la kitaifa na la kidunia pia
 
du hii ni balaa,wanajimaliza wenyewe au ni Mungu ameamu kuwapiga upofu?
 
Wakuu, Ni kweli ujumbe huu umesambaa sana kwenye simu, Sijui lengo kuu la ujumbe huu ni nini? Tuache kutumia mitandao ya kijamii kujenga hasira kwa watu. Hii ni hatari kwani mwisho wa siku, si mimi wala wewe, hatutacheka. Kila mtu atalia. Tutumie hoja za kujenga nchi kuliko hoja za kubomoa
 
Tatizo lako nini mkuu na wewe si ugombee huko Uvccm??
Kama na wewe unataka
 
Wakuu, Ni kweli ujumbe huu umesambaa sana kwenye simu, Sijui lengo kuu la ujumbe huu ni nini? Tuache kutumia mitandao ya kijamii kujenga hasira kwa watu. Hii ni hatari kwani mwisho wa siku, si mimi wala wewe, hatutacheka. Kila mtu atalia. Tutumie hoja za kujenga nchi kuliko hoja za kubomoa
Sasa unataka tukae kimya kwa kuogopa machafuko na kuwaacha wahujumu demokrasia hawa wakitufanya watz wajinga?Unaakili ya kitumwa sana wewe kama unaogopa kifo kaa kimya sisi hatuogopi kifo wala kuua maana tumeshazoea kuuawa na itafika zamu yao siku moja utashuhudia au kusimuliwa haki itakavyokuwa ikitendeka
 
Back
Top Bottom