Sioni tabu ya hawa watoto kugombea nafasi yeyote ndani na nje ya vyama vyao nao ni watanzania wenye haki sawa na mtanzania mwingine tusiwanyanyapae kwa sababu tu baba zao ni vigogo au mashuhuri au wanasiasa. Tuangalie je uchaguzi ulikuwa huru na haki. Je wazazi wao walilazimisha wao kushinda au walishinda kwenye mfumo huru??
Na sisi watoto wa akina pangu pakavu tusibweteke na kujiona wanyonge kwa kila kitu, jazeni form kwenye mifumo hii ya kisiasa serikali taasisi mbali mbali mshiriki badala ya kukaa pembeni na kupiga mayowe. Ninaushahidi wa kutosha kwamba watanzania wengi wanapenda kulalamika sana bila kushiriki. Sasa kama ninyi hamtaki kushiriki kwenye hizo chaguzi mnategemea nini?? Vigogo wanajitengenza na kazi ni kugombea tu. Ni vyema tukapigia kelele rushwa na kupendelea kuliko kuwawanyapapa hawa wototo kwa sababu tu baba zao wanamajina, wengine masikini zaidi ya majina ya baba zao choka mbaya.
Tushiriki kwenye mfumo wetu ili tuwe na kesi
Chief Mkwawa wa Karenga
No spinning
Chukua hatua madhubuti, tetea haki, wajibika, shiriki, kulalamika hakubadilishi nchi.