64Bits
JF-Expert Member
- Aug 4, 2012
- 961
- 565
Habari zenu wana MMU, wakubwa shikamooni.
Leo kuna jambo naombeni wenye uzoefu wanipe mawazo yao.
Mimi ni mama wa kambo kwa mtoto wa kiume wa miaka 8.
Nilimkuta baba yake amesha achana na mama yake kabla hatujaanza mahusiano.
Jamani mtoto huyu amekuwa mtihani kwangu, hata nimfanyie nini mimi mbaya tu kwake, nampenda, namjali namfanyia wema wote ambao mtoto anatakiwa afanyiwe lakini shukrani yake ni kunizulia uwongo wa kila aina.
Najisikia kumtazama tu nimuache afanye analotaka nisimuonye... asofunzwa na ***** atafunzwa na ulimwengu.
Halafu baadae nafsi inanisuta najirudi tena naambulia maneno tena.
Jamani si kila mama wa kambo mbaya na si kila mtoto wa kambo mzuri... kuna wengine wanaweza kukukalia kooni ka mwiba wa samaki.
Najuta akija weekend maanake sikai nae ila babake atamchukua tuishi wote soon.
Wakubwa nipeni mawazo yenu naishije kwa amani nae?
Kama kuna "mtoto wa kambo" humu ndani anaweza kushare experience yake labda itanisaidia kuelewa ni nini huwa kinapita kwenye akili zenu?