Asante wote kwa mawazo yenu. Wengi wameuliza anakuja weekend tu tunagombanaje sasa?
Ni hivi mfano mtoto anaweza kutaka kucheza mahali hatarishi mfano jikoni etc, mtoto anaweza kugoma kula na vitu kama hivyo so kuna saa inabidi umueleze na ikibidi uwe mkali for his own sake. Kama hizo zawadi jamani nanua sana nikipita nikiona kinachomfaa na kama nina pesa namnunulia. Mi sio mchapaji kwa kweli wala sijawahi kumchapa na fimbo kuna siku nilimfinya kidogo kwenye makalio baada ya kuwa hasikii anacheza na mpira ndani na kuna saa unapitiliza jikoni na kulikuwa na mafuta ya moto. Mimi sipo hapa kuchukua nafasi ya mamake wala siitaki, ila ndo hivyo tena. Inaniuma sana kuona kila nilifanyalo kwake halina wema, so why bother? Nihangaike na mwanangu tu nijitazamie mambo yanavyokwenda manake mama mtu pia anawapigia simu ndugu za mume wangu kusema mi namtesa mtoto. Acha nikae nae tu kama yai, anachotaka atapewa, sitasema kitu labda aje anifunue sketi yangu ndo ntasema! Mweeee! Kua uyaone!
Nashukuru mrsleo na wote mlochukua muda wenu kunishaurijamani pole, manake umeongea kwa uchungu mpaka nimesikia huruma, ila ukisema umuachie tu afanye anachokita mfano hilo swala la kucheza ndani mpaka jikoni na kuna kitu hatarishi mfano hayo mafuta ya moto ikitokea akaungua lawama zitarudi kwako na utawapa reason za kuona kweli humpendi, me nazani huyo bado mtoto mwenye kuhitaji msaada wa kumjenga kimaisha na kitabia hapo mbaya ni mama yake, sasa cha msingi kwa kuwa hili swala limefika mpaka kwa ndugu wa mume na mume mwenyewe, wewe itisha kikao awepo huyo mama yake na mtoto, mumeo, na baadhi ya ndugu wa mumeo ili uongee haya unayotumbia sisi na mengineyo yote yanayokukosesha amani kuhusiana na mahusiano yako na huyo mtoto, nazani hapo pekee ndo kutapatikana suluhisho
Malezi ya watoto wa kambo yamekuwa tatizo, wahanga wakiwa hao mama wa kambo. Mara nyingi wao wanatupiwa lawama, hata wajitahidi vipi, nimekuhurumia sana 64Bits kwa shida inayokupata katik malezi ya mtoto wenu.
Ninaamini mengi anajifunza au kuambiwa na mama mzazi. Hali inaweza kubadilika mkianza kuishi pamoja, kwa sababu mama hatakuwepo kumpa ushauri m'baya.
Lakini pia, kwa sababu ulijua kuwa mumeo ana mtoto hata kabla ya kuamua kuishi nae, huna budi kumlea huyo mtoto kwa malezi bora, kama mtoto wa tumbo lako. Omba busara, mshirikishe mume wako katika malezi ya huyo mtoto, kwa sababu akiharibika kuna uwezekano hata wadogo zake wakafuata njia hiyo.
Mwisho, mapenzi hayachagui, unaweza ku-fall kwa yeyote, lakini mtu mwenye mtoto aoe/aolewe na mwenye mtoto...single parents waoane...hii itapunguza matatizo kama haya..
Asante mkuu kwa mawazo yako na kuchukua muda wako kunishauriPole kwa yote unayokabiliana nayo, ingawa neno lenyewe 'mtoto wa kambo' ni mtihani, lakini ngoja nijaribu kutoa mchango wangu japo waweza kuwa haujanyooka sana. I have been through yote unayopitia na anayopitia huyo mtoto but amini you are in more better position to make things right kuliko huyo mtoto kama ifuatavyo;
1. 8 yrs old kid : Usisahau, uwe umemzaa ama hujamzaa, huyo ni mtoto tu ... hebu jaribu kuvuta pita kipindi ukiwa na umri huo, hali yako ilikuwaje. Jaribu kumchukulia kama mtoto kwa kumkanya kwa upendo na saa nyingine kumweleza ukweli i.e Madhara ya makosa anayoyafanya, kumbuka siku moja atakuwa mkubwa na atakukumbuka kwa yote ....
2. Jiamini, tenda haki and do it for you: Prove that you are not spoil na mob psychology na stigma dhidi ya watoto wanaokutwa kwenye mahusiano yenu(NDOA?!), very sory malalamiko siku zote huwa yanatokea kwa wakina mama na si wa baba wa kambo .. umewahi kujiuliza kwanini?!Fanya hivi, jiamini na tenda kama vile MUNGU anakuona, usimpendelee na kama kuna kazi za umri wake mpe, akifanya kosa mkanye kwa 'sauti' but sikushauri sana kuchapa coz that tend to bring more harm than good even kwa mtoto wakumzaa mwenyewe unless proven otherwise.
3. Re asess yourself : Ni muda mzuri sasa kujiuliza kama mama(wa NDOA), nini ufanye kuweka mambo sasa ... la kwanza umekuja kuomba ushauri hapa jamvini, ni sawa kabisa but now its your time kuchukua akili za mbayuwayu ukajumlisha na za zako kupata maamuzi sahihi ... usisahau na kumbuka, lolote utakaloamua na kulitenda litakuwa na malipo baadaye(when in need) either mazuri ama mabaya.
(Ni mtazamo binafsi)
Mtoto sio mbaya bali anapata ubaya kutoka kwa mama ake. Kuna baadh ya akina mama wanatabia ya kuwafundisha mambo mabaya watoto zao ili wawafanyie mama zao wakambo hali wao wameachika.
How is your relationship with his mother? I believe kids have pure and innocent hearts by nature unless we show them otherwise...
A child would always want to see his/her parents together.
Just give as much love and care as you can. Try to find better ways to corrent him when he is wrong...
Kim nana nilikuwa nikiyafanya haya na mengine ila saivi kwa kweli moyo wangu unakufa ganzi kila kukicha
Habari zenu wana MMU, wakubwa shikamooni.
Leo kuna jambo naombeni wenye uzoefu wanipe mawazo yao.
Mimi ni mama wa kambo kwa mtoto wa kiume wa miaka 8. Nilimkuta baba yake amesha achana na mama yake kabla hatujaanza mahusiano. Jamani mtoto huyu amekuwa mtihani kwangu, hata nimfanyie nini mimi mbaya tu kwake, nampenda, namjali namfanyia wema wote ambao mtoto anatakiwa afanyiwe lakini shukrani yake ni kunizulia uwongo wa kila aina. Najisikia kumtazama tu nimuache afanye analotaka nisimuonye... asofunzwa na ***** atafunzwa na ulimwengu. Halafu baadae nafsi inanisuta najirudi tena naambulia maneno tena. Jamani si kila mama wa kambo mbaya na si kila mtoto wa kambo mzuri... kuna wengine wanaweza kukukalia kooni ka mwiba wa samaki. Najuta akija weekend maanake sikai nae ila babake atamchukua tuishi wote soon. Wakubwa nipeni mawazo yenu naishije kwa amani nae? Kama kuna "mtoto wa kambo" humu ndani anaweza kushare experience yake labda itanisaidia kuelewa ni nini huwa kinapita kwenye akili zenu?
Kadiri mtoto wa kambo anavyokuwa ndio matatizo hayo yanavyokuwa...mi na miaka 21 now na mtoto wa kambo, amekuwa kama mume mwenzangu tukigombana na mamake wana side upande mmoja, vumilia tu dada ukipenda boga.
Jamani mtoto huyu amekuwa mtihani kwangu, hata nimfanyie nini mimi mbaya tu kwake, nampenda, namjali namfanyia wema wote ambao mtoto anatakiwa afanyiwe lakini shukrani yake ni kunizulia uwongo wa kila aina.
Hold on, hebu twende taratibu, wewe umri wako ni miaka 21 au tangu uolewe huu ni mwaka wa 21 na unaishi na mtoto wa kambo?
Binafsi umenchanganya sana na aina ya kauli zako! Naangalia umri wa mtoto, nafananisha na tuhuma zako, nakosa pa kushika! Daah, sijui lkn mtoto wa miaka 8, tena wa kukutana nae w.end hadi w.end, daaah!